Mkuu!!!
Hivi ukishamfundisha mwanao adabu kwa kumchapa kisawasawa unadhani kuna haja ya kukaa nae mezani na kuanza kufanya mjadala mkijadiliana kwamba ilikuwaje,na kwanini?
Personally,serikali iko sawa na tuitunze amani kidogo tuliyo nayo haya mambo watu wanakaa hawafanyi kazi wanalalamika lalamika hovyo pasi na sababu za msingi wakiendelea kuchekewa chekewa tutashindwa kuwaona wajukuu zetu,ni kuwashugulikia tu plan A {negotiations} ikishindikana serikali i-skeep to Plan C even D ili tukae sawa.
Nazungumzia mtu au kikundi chochote,hapana kuchezea amani ya taifa.
Ngoja nikuambie kitu.
Hawa watu, Sudan wapo. Egypt, wapo, Pakistan, wapo. Hata Saudi penyewe wapo na kote huko hushikishwa adabu zao.
Huyu mzee hapa ka-'thrive' kweli kwa taarifa zake za upindishaji na kuwapata watu wanaomwona kama mtaalam sana. Ukimsoma vizuri utaona katika maandishi yake yoote, ni ya kupindishapindisha taarifa na kutafuta majina makubwa kuhalalisha anayoyaandika ili watu waamini anachoandika.
Akishabanwa na uongo wa maandishi yake unapogunduliwa, utaona anasogeza au anabadili msimamo kiaina. Siku hizi imembidi akubali uongozi wa Mwalimu Nyerere tokea huko nyuama. Ukimsoma alivokuwa akiandika juu yake huko mwanzo, tadhani Mwalimu hakufanya kazi yoyote katika uongozi wa kuleta Uhuru wa Tanganyika.
Anasimulia hadithi za kuambiwa na kuziongeza chumvi anavotaka yeye ili kuchota akili za watu wanaomtegemea katika upindishaji wa habari nyingi.
Akibanwa kwenye udini anaoutumia kwa maslahi ya kujijengea jina, utamwona akiruka na kukataa kuwa yeye huko hayupo. Ndio maana mimi namwita ni tapeli aliyekubuhu.
Misingi ya kidini anayoisimamia, ndiyo hiyo hiyo anayomlaumu Mwalimu Nyerere kuibaini na kuiondoshea mbali mapema kabisa; na ndio sababu kuu ya yeye na wanaomkubali huyu mzee kumchukia Mwalimu Nyerere. Na kama hali ile waliyoitaka, ya dini na siasa ziambatane isingestukiwa kungali mapema, nchi hii sasa hivi ingekuwa ni tofauti sana na ilivyo sasa.
Maajabu ni kwamba bado wanayo matumaini kwamba siku moja hali hiyo inawezekana kuletwa hapa Tanzania!