Mama Debora
JF-Expert Member
- Aug 30, 2018
- 1,481
- 2,609
Sikumbuki exactly but kilichoshangaza waliokamatwa walikutwa wakristo wengi sana
So mostly inaonesha kulikuwa na kilio tu cha watu kudai uhuru wa kuandamana
na uhuru wa kupinga hiki au kile...
Msikiti wa mwembechai ulitumika tu kwa raia wengine kujiunga kwenye madai hayo
Ndani ya tukio hili niliwaona live polisi wa vituo vidogo vya polisi pale friends Corner,Tandale,CCM Manzese,Manzese mpakani wakivikimbia vituo vyao baada ya raia kuvivamia na kuwaachia waliopo ndani ya vituo hivyo na kuchoma makaratasi,kuchoma moto magari yenye namba za serikali ila walishindwa kukivamia kituo cha polisi pale urafiki,polisi walikilinda,kiza kilipoingia maeneo ya manzese wahuni wakaanza kula kula,FFU walikuwa wanaishia Morogoro road wakiingia ndani wanakutana mawe na kukimbia
Nalog off
Japo nilikua mdogo kama miaka 4 hivi lakini sitasahau yale mabomu ya machozi asee tulipata tabu sana wakazi wa Manzese hilo tukio hadi leo lipo kichwani. Ikapelekea mzee kujenga fasta vyumba viwili Tabata Kisukuru tukahamia ingawa kulikua bado porini kweli kweli.
Sijui sababu ilikua nini dah.
ITV kwenye taarifa ya habari walionyesha clear and everything. Nakumbuka kuona waandamanaji wakirusha mawe. Polisi walikuwa kwa mbali wanalenga na bunduki zao. Sauti ikatoka piga yule, ala unaogopa. Risasi zikarindima. Tahamaki baadhi ya waandamanaji wakawa wamelala kwenye madimbwi ya damu. Nakumbuka mmoja alifariki huku akiwa bado ameshikilia jiwe mkononi. Chanzo cha vurugu zile ni kukamatwa kwa viongozi wao. Hao viongozi walikuwa wanatuhumiwa kufanya dini ya siasa kali. Walipokamatwa ndiyo wenzao wakakinukisha kushinikiza waachiwe.
Bado wanaendelea kuonewa au walishapata haki zao?Kwa kweli waislamu walionewa sana masikini!
Sijui kwa kuwa uongozi wa juu uliokuepo walikua wakristo. Na ukijumlisha na Nyerere (mkatoliki) alikua bado hai ndio kabisaaa
Bado wanaendelea kuonewa au walishapata haki zao?
bahati nzuri haya majibu ya maswali yako yote wanayo PEOPLE'S POWER ..WAZEE WA VIDOLE VIWILI[emoji23]Aslamwalekhum
Serikali ni kichwa dini ni masikio na sio kinyume chake. Masikio yanapotaka kuzidi kichwa haitaleta picha nzuri,
Dini ibaki kuwa dini, na hakuna sababu ya kuleta uwiano sawa wa serikali katika watu wa dini.
Yaliotokea yameyokea lakini tujifunze mipaka yetu mashekh wenzangu, ya kaisari yabaki kwa kaisari na ya mungu tumuachie mungu
Mimi kama muislam swafi hadhia ya mwembe chai chanzo kilikua sis wenyewe waislam ukweli ambao hatuutaki kuusikia (mtanisamehe kwa hili)
Tunatumia nguvu katika kuaminisha uislam ni dini ya kweli na haki, mihadhara isiyo na tija na tunajisahau kwa maneno ya kashfa katika dini za wenzetu tunafika mbali hadi kuingiza itikadi zetu kitaifa (hili taifa haliamini katika dini )
Mafunzo ya karate na Kong fu tunajilinda na nani? Kwani jeshi la kulinda nchi halipo? Hayo mafunzo yapo katika misingi gani? Mafunzo ya karate katika nyumba za ibada tunaabudu mungu au tunaandaa jeshi? Kwanini mafunzo ya karate yanakua kama ya lazima kuna ajenda gani? (Hapa kuna maswali mengi yasiokua na majibu)
Takbil..
TulipangaKwahiyo nyumba yenu ya magomen mkaiuza? Ama mlikua mmepanga
Zile zilikua 'kubadhi' mkuu, sio yebo yeboNia yako nini?
Na pili Raisi wa Wakati huo ni mstaafu unaweza kwenda kumuuliza kama askari ndio waliokuwa na makosa au waliosababisha hizo vurugu n.k
Au una lako Jambo ndio maana unataka kumchokoa "pweza"
Chanzo kilikuwa Paroko Lwambano kwenda Sehemu Nyeti kusema kuwa ndani ya Msikiti wa Mwembe chai Yesu alikuwa anatukanwa
Enzi hizo kusema Muhammad sio Mtume haiku warm kosa
Kusema Ng’ombe sio mungu haikuwa kosa
Kusema mizimu sio Mungu pia haikuwa kosa
Kosa lilikuwa kusema Yesu sio Mungu ni kosa kubwa kuliko kukutwa na Kete za Bhange
Baada ya watu kukubali kufa, kujeruhiwa na kufungwa hatimae baadae Mahakama Kuu ikatangaza rasmi kuwa sio kosa na aliefungwa kwa kosa hilo aachiwe huru na Ndugu Hamis Dibagula akaachiwa huru
Kuna baadhi ya haki hazipatikan kwa kutoa press release wala kuitisha Makongamano ya kudai bali lazima uumie kuipata
Pohamba acha uongo. Hakuna mkristo wa ukweli. Atakayelalamika ukisema Yesu si kitu, au Yesu si mtume au si Mungu. Mkristo hasa hawezi kukupiga au kulalamika for that case. Coz wewe au mimi nikisema hivyo it doesnt change anything.
Hata leo hii Yesu akitukanwa Mkristo halisi hawezi kulalamika kwa hilo. Why alalamike?
Ni wafuasi wa Allah ndio walisababisha hii turmoil
Sijasema Lwambano alikuwa Mkristo wa kweli au laa, mie hiyo sio sehemu yangu
Basi kwa taarifa yako hakuna anayeweza lalamikia hilo. Waislamu walitaka kutest mitambo...wakakuta ipo ok.hawakutamani tena. Wajinga kadhaa walikuwa wanadanganywa na Ghadaffi. From there nadhani haya Wakristo nao hawakuwahi kutaka fikiria upumbavu wa namna hiyo.