Nini hasa kilisababisha vurugu za Mwembechai mwaka 1998?


Zahaki Rashidi
​
Zahaki Rashidi Ngai si jina geni katika masikio ya Waislamu wengi hapa nchini. Yeye ni mmoja kati ya wanaharakati wachache ambao wametajwa sana na masheikh, vyombo vya habari na hata katika vitabu maarufu vilivyoandikwa na waataaluma wa Kiislamu.

Umaarufu wa Zahaki umetokana na kutajwa shuhuda muhimu wa tukio la mauaji ya Mwembe Chai na dhuluma mbalimbali ambazo Serikali imewatendea Waislamu.

Kwa mara ya kwanza, Zahaki alitoa ushuhuda wake kwa mwanahistoria maarufu Muhammedi Saidi. Alifanyiwa mahojiano maalum kuhusu ukweli wa mauaji ya Mwembe Chai. Hapo aliyasema yote aliyoyaiona na aliyoyaamini.

Baada ya hapo, ushuhuda huo ulichapishwa katika kitabu maarufu cha Prof. Hamza Njozi, kilichoitwa, ‘Muslim and state in Tanzania’ .

Zahaki atajwa katika ujambazi

Akizungumza na gazeti la Imaan kabla ya kwenda polisi kuhoji kutajwa kwa jina lake katika taarifa zilizozagaa katika mitandao ya kijamii akitajwa kama miongoni mwa wahumiwa wa mauaji yaliyotokea kituo cha polisi Stakishari.

Alisema baada ya kupokea taarifa hizo za kuhusishwa na uhalifu huo, hatua ya kwanza aliyofanya ni kutaka kukutana na waandishi wa habari ili Waislamu wenzake wajue ukweli juu ya dhuluma ambayo jeshi la polisi linajaribu kumfanyia akiamini inatokana na historia yake ya kusema kweli kuhusu tukio la mauaji ya Mwembe Chai.

Alisema kinachotokea sasa ni matokeo ya chuki na kisasi cha muda mrefu kilichotokana na uamuzi wake ya kusema kweli katika tukio lile la mwaka 1998 ambalo lilipelekea kufukuzwa kazi ya polisi na kufedheheshwa baada ya kulikosoa jeshi hilo.

“Najua mtuhumiwa akishafika katika mikono ya polisi ni vigumu kukutana na waandishi wa habari na kuzungumza ukweli. Baada ya kuliona hilo nimeamua kukutana nanyi ili kuwaambia ukweli Waislamu wenzangu kuwa katika tukio hili mimi sihusiki hata kidogo na hata huyo anayetajwa kuwa kiongozi wa kundi simfahamu,” alisema Zahaki.

Alisema kutokana na matukio ya Mwembe Chai, Jeshi la Polisi lilikasirishwa na limekuwa likimfuatilia kila hatua ili ipatikane nafasi ya kumpa kesi ili wampoteze ulimwenguni.

“Ndugu waandishi wa habari, mimi miaka yote nipo hapa nchini, nina wake wawili ambao naishi nao. Ajabu ni kwamba Jeshi la Polisi linadai mimi nimerejea kutoka Ethiopia. Huo ni uzushi ambao wanajaribu kuutumia ili nionekane muhalifu wakati ni uongo mtupu”, alisema Zahaki.

Zahaki aliongeza: “Jeshi la polisi wawe wa kweli. Wafanye utafiti wao kwa makini badala ya kuvamia watu kwa kuwa shuku kwani hatua hiyo itafanya kukamatwa kwa watu ambao hawana hatia jambo ambalo halitamuathiri mtuhumiwa peke yake bali litaathiri maisha ya watoto, wake na wazazi wake”.

“Mimi nilikuwa Sajenti katika kitengo cha ‘Crime Stoppers Unit’ - Central Police. Tukio la Mwembe Chai lilivyotokea mimi nilikuwa ndio ‘in charge’. Nilitoa maelezo yangu kuhusu taarifa za tukio hilo lakini jeshi halikuridhika. Wamenifukuzwa kwa aibu na sasa wananishughulikia nje ya Jeshi la Polisi”. Alilalamika Zahaki huku machozi yakimlenga lenga.

Ujumbe kwa Waislamu

Zahaki amewataka Waislamu wenzake kumuombea dua kwa mtihani huo ambao ameupata huku akiwahakikishia kuwa hajahusika katika uhalifu huo uliotekelezwa katika kituo cha Stakishari.

“Wa Llaah wa Billaahi sijahusika na uhalifu wa Stakishari, Mwenyezi Mungu anajua zaidi. Nitakwenda kuwahoji kwa nini wametaja jina langu na kulihusisha na mauaji yale, na pia kwa nini wanadanganya umma wa Watanzania kuwa mimi nimerejea kutoka Ethiopia wakati nipo hapa nchini? Wana ajenda gani ya siri” alisema Zahaki.

Aidha, Zahaki alisema anataka Waislamu wajue ukweli wote hata akiwa ameshikwa na Jeshi la Polisi ama kuuliwa katika mazingira ya kutatanisha, wajue kilichomuua ni chuki kutokana na kusema kweli katika kadhia ya Mwembe Chai.

Aibukia Jeshi la Polisi, akamatwa

Kama alivyoahidi kwa waandishi wa habari kuwa angekwenda kuhoji Jeshi la Polisi juu ya jina lake kuhusishwa na mauaji ya Stakishari, Zahaki kweli alifanya hivyo . Lakini taarifa ambayo Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam ilIitoa kwa waandishi wa habari ilisema mtuhumiwa huyo alijisalimisha.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema Mtuhumiwa Zahaki Ngai amejisalimisha kwa Jeshi la Polisi akiwa na wake zake wawili na kusema kuwa wale ambao bado hawajapatikana msako bado unaendelea.

Maneno hayo ya Kamishna Kova ni kama mwiba kwa Zahaki ambaye alishatangaza kuwa anaenda kuhoji kwa nini jina lake limetajwa na sio kujisalimisha. Kama alivyotabiri, inaonekana kama polisi wameendelea kupotosha umma.

Akizungumza na gazeti Imaan, Mwanasheria wa mtuhumiwa huyo alisema wanashangazwa na upotoshaji wa Kamanda Kova kwa umma wa Tanzania kwani Zahaki hakwenda kujisalimisha bali alikwenda kuuliza ukweli wa tetesi anazozisikia katika vyombo vya habari.
Kilindo alisema upotoshaji huo unakera na unaudhi kwani matamshi ya Kamishna wa polisi ni sawa na kuthibitisha kuwa ana uhakika Zahaki ni mhalifu na hivyo kupewa kesi hiyo wakati yeye hakuhusika na kadhia hiyo.

Katika tukio ambalo polisi wanadai Zahaki alihusika, majambazi kadhaa yalivamia kituo cha polisi cha Stakshari na kuua watu saba majira ya saa 5 usiku, Julai 12, 2015. Mpaka sasa tayari watuhumiwa tisa wanahojiwa kuhusiana na tukio hilo.

(Makala kwa hisani ya gazeti la Imaan Agosti 31 - Septemba 6, 2015)
uchunguzi
 
Kilichosababisha mwembechai kinuke mwaka 1998.
Ingawa nilikuwa mdogo, lakn kiasi nilikuwa na uelewa wa kuangalia taarifa ya habari na kusimulia kwa ufupi nini kimeelezwa.

Ikumbukwe kuwa mwaka 1998 vuguvugu la vurugu la udini lilitaka kuitawala Tanzania na Afrika mashariki na dunia kwa ujumla kwa kujithibishia kuwa dini IPI ni bora na ina nguvu kiasi gani.

Ni kipindi ambacho dini moja ilikuwa inamikutano ya kutafuta waumini kwa kuita mihadhara ya hoja na kualika msemaji kutoka dini nyingine kubishana kwa hoja. Mihadhara hii ilifanyika sana karibu kila kiwanja cha wazi kilichopo karibu na nyumba ya ibada maeneo km mwananyamala...magomeni...manzese ...kigogo...kinondoni mtambani nk n jambo LA kawaida kukuta mihadhara ya dini na kina Dr sule wakihutubia kipindi hicho.

Ikumbukwe pia ni kipindi hikihiki cha mwaka 1998 ndicho kulizuga propaganda nyingi sana za udini hata ikafika mahali ndani ya sehemu ya nyumba ya ibada kunakuwa na mawaidha ya kuhubiriana kuwa dini Fulani INA viongozi wengi serikalini kuliko sisi kwahyo wanatutawala na hatuna maamuzi katika nchi yetu.

Mwaka 1998 kama ulikuwa na akili timamu ndio kipindi ambacho kila nyumba ya ibada nilikuwa na mafunzo ya karate kwa vijana wa dini kwa lengo LA kujilinda. Self defence ukiniuliza walikuwa wanajilinda nini ? Sina jibu.

Na ndio mwaka huo kulikuwa waliibuka viongozi wa dini wenye ushawishi mkubwa kwenye mimbari..kwa Tanzania na Afrika mashariki. Watu km shekh Rogo kule Mombasa...kulikuwa na connection na shekh mmoja alikuwa Mwanza kwa Tanzania na wengne walikuwa visiwani.

Serikali kwakuona hatari ya mbele ikapiga BAN mihadhara yoyote ya dini. Hapo ajenda za ajabuajabu zukapita kupitia nyumba za ibada kuwa wanatunyanyasa umma.

Na mengne meng ambayo huwezi kuandika hapa kwa usalama wa nchi na kuibua tena hasira za wafia dini na kuchafua nchi. Naishia hapa kwa machache baada ya upande mmoja kushindana serikali ya Ben kipindi hicho.
 
Nilikuwa nakuja likizo toka Morogoro, Abood ikatushushia Mwenge badala ya Magomeni. Lakini, mwenye majibu mazuri ni Mwenyekiti wa Kanda wa Chama cha Ufipani. Wenye hicho chama walimtuhumu sana kabla hajawa mwenzao kuwa ndio aliwatuma waliotumwa.
 
Unachokisema bw Pohamba ni kweli kupata haki hadi uumie.
 
Muislamu kuelezea hili tukio ,lazima atie chumvi nyingi kuvutia upande wake ili ionekane waislamu walionewa.

Na uhakika hicho kitabu asilimia kubwa kinaonesha Waislamu walionewa.
 
Muislamu kuelezea hili tukio ,lazima atie chumvi nyingi kuvutia upande wake ili ionekane waislamu walionewa.

Na uhakika hicho kitabu asilimia kubwa kinaonesha Waislamu walionewa.
Hata wakristu walioshuhudia tukio wanakiri waislamu walionewa issue ya Mwembechai
 
Aslamwalekhum

Serikali ni kichwa dini ni masikio na sio kinyume chake. Masikio yanapotaka kuzidi kichwa haitaleta picha nzuri,
Dini ibaki kuwa dini, na hakuna sababu ya kuleta uwiano sawa wa serikali katika watu wa dini.

Yaliotokea yameyokea lakini tujifunze mipaka yetu mashekh wenzangu, ya kaisari yabaki kwa kaisari na ya mungu tumuachie mungu

Mimi kama muislam swafi hadhia ya mwembe chai chanzo kilikua sis wenyewe waislam ukweli ambao hatuutaki kuusikia (mtanisamehe kwa hili)

Tunatumia nguvu katika kuaminisha uislam ni dini ya kweli na haki, mihadhara isiyo na tija na tunajisahau kwa maneno ya kashfa katika dini za wenzetu tunafika mbali hadi kuingiza itikadi zetu kitaifa (hili taifa haliamini katika dini )

Mafunzo ya karate na Kong fu tunajilinda na nani? Kwani jeshi la kulinda nchi halipo? Hayo mafunzo yapo katika misingi gani? Mafunzo ya karate katika nyumba za ibada tunaabudu mungu au tunaandaa jeshi? Kwanini mafunzo ya karate yanakua kama ya lazima kuna ajenda gani? (Hapa kuna maswali mengi yasiokua na majibu)

Takbil..
 
Kaaa kimya wew usilo lijua ni sawa na usiku wa giza

Katika hili taifa Kuna meng na ndio maana hawataki hata kuliongelea swala mwembe chai na Wala kugusia ila muulize prof lipumba na tawala zilizopita wanajua ya mwembe chai na zanzibar.

Mfumo ulitengezwa nje ya mfumo ili kupatikana mfumo ila ikafeli na mfumo haukupatikana

Nalog off
 
Harakati hazikamiliki kwa Siku moja ya kufa kwa shekh Rogo. Kufa kwake mwaka 2012 na kumfanya maarufu Afrika Mashariki hakumfanyi kuwa yeye alianza harakati wakati wa umauti wake.
Alishaweka mitandao kwa tao LA Afrika Mashariki mpaka huo mwaka was 2012
Kifo cha shekh Rogo mwaka 2012 na kusikika umaarufu wake kwa mwaka huo haimaanishi kuwa harakati zake zilianza mwaka huo wa 2012.
Mpaka kufikia mwaka was 2012 alishaonekana hatariii kwa Afrika Mashariki kwani alishakuwa na mtandao mkubwa. Nikikumbuka jina shekh mmoja aliyekuwa Mwanza aliyekuwa na ushawishi mkubwa ambaye naye kifo chake n utata ntakutajia ambapo ndipo Mara nyingi mawasiliano yalifanyika kwakile ambacho wao walikiamini.
Kwa bahati Serikali iliwawahi na kuzima vuguvugu baya kabla ya kukomaa
 
Mkuu mimi sitakaa kimya labda uanze wewe kukaa kimya
Masikio yasizidi kichwa, waislamu sisi huwa tunavuka mipaka yetu wewe ulishasikia chokochoko za wenzetu wakristu, kila siku sisi tunaona kama tunaonewa sasa. Sasa swali tunaonewa vipi ili hali kuna Uhuru wa kuabudu wa kutosha tu??

Tumekuwa watu wa kulalamika sana,!! Tumuabudu mungu katika imani
 
Mfano hili la mwembechai watu wanasema yao tu mmewasikiliza waislam
Serikali si jinga hadi kutumia silaha ya moto. Wacha kulialia humu. Ilikuwa ni sahihi kutuliza ile ghasia kwa mtindo ule.
Spirit ile ile ndo ilikuwa ikiunda kikundi chenye mwelekeo wa uamsho (Tanzania), alshabab (pembe ya africa), Tuareq (central africa) na bokoharam (west africa). Tanzania ikashindikana kwa sababu serikali ilikataa kulea uhuni, ingawa walitaka kuchomoza tena kupitia Amboni Tanga na Mkiru. Hawa watu si wa kucheka nao hata kidogo.
 
Katika jambo ambalo tulikuwa vizuri n pamoja na usalama wa Taifa wa miaka ile ambapo jambo linazimwa kabla halijakomaa. Interconnection ya idara ya usalama na kujaa makachero ambao hata mke hajui unafanya nin.
Kuna mzee mmoja alikuwa anajulikana kama kichaa akipita mitaa ya kawe na mikocheni...utimamu wake was akili ulijulikana wakati was maziko.
Vitu vya udini sio vya kufurahia hata sekunde ukidetect kuwa mwelekeo sio.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…