Nini hasa kinafanya gharama za kuchimba kisima kuwa mil 8, 10, 12? What is so special?


Duuh mita 35 unapata maji? Si unakunywa maji machafu? Mimi mkoani nimechimba mita 150m ,ilinicost milioni 9.
 
Mkuu niki arusha. Naweza pata kampuni arusha. Pil
Duuh mita 35 unapata maji? Si unakunywa maji machafu? Mimi mkoani nimechimba mita 150m ,ilinicost milioni 9.
Mkoa gani
 
Yaani unajisifu kwa kunywa vinyesi na mikojo yako!
Maji yakipita kwenye udongo yanapitia natural filtration, yaani 35m sidhani kama anakunywa maji machafu, ajaribu kuyapima kujua kama yana shida au la ila ninachojua udongo kwa ujumla ni filter nzuri sana ya maji.
 
Hivi unaweza kuchimbiwa kisima cha kutosha kumwagilia shamba la heka 8 kila siku bila kukauka?
 
Cha msingi ukishachimba chukua sample uwapelekee Idara ya Maji wakayapime kabla ya kutumia. Tunatumia sana maji ya visima ila sina uhakika kama ni salama kwa matumizi kwa kuwa huwa hatuna utaratibu wa kupeleka sample maabara ya maji.
 
Tofautisha kuchimba Dar kwenye michanga na bara kwenye miamba migumu ya mawe, lazima bei ziwe tofauti. Dar unachimba kwa mashine ndogo ambazo watu wawili wanaweza ku-operate lakini bara unatumia drill rig inayohitaji si chini ya watu watano ku-operate. Dar unaweza kuwekewa bomba za class B za bei rahisi lakini bara lazima utumie bomba za class C au D za bei kubwa.

Dar unachimba visima vifupi kwa bei ndogo kukwepa chumvi kwani kadri kinavyokuwa kirefu ndiyo uwezekano mkubwa wa kukuta maji ya chumvi. Bara unachimba visima virefu kwa bei kubwa ili kupata miamba iliyopasuka na kuhifadhi maji.

Kwa kifupi kuna vitu vingi vinavyofanya bei kutofautiana kutegemea aina ya uchimbaji na mabomba yatakayotumika.
 
Maji yakipita kwenye udongo yanapitia natural filtration, yaani 35m sidhani kama anakunywa maji machafu, ajaribu kuyapima kujua kama yana shida au la ila ninachojua udongo kwa ujumla ni filter nzuri sana ya maji.
Amesema kisima chake kimechimbwa kwa jembe! Je unaweza kuchimba mita 35 kwa jembe?
 
Ok, Leo ndio nimeona huu Uzi hata sikuangalia tarehe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…