Nini hasa kinafanya gharama za kuchimba kisima kuwa mil 8, 10, 12? What is so special?

Nini hasa kinafanya gharama za kuchimba kisima kuwa mil 8, 10, 12? What is so special?

Hao wenye mashine na wao wamejaa tamaa sana,yani ni kweli uchimbaji wa visima ni ghali mno hakuna uhalisia yani tunapigwa sana sisi watanzania
Hem toa tathmini yako, unadhani gharama kiasi gani ni affordable kwa mtanzania!
Wakati wa kutoa tathmini angalia vigezo kama;
1. Gharama ya mtaji wa drilling machine. Fanya consideration ya repair and service.
2. Umbali maji yalipo(water table)
3. Gharama za vifaa kama bomba, wire za umeme, pump etc.
4. Kulipa wafanyakazi nk nk.
 
Katika vitu ambavyo Kila nikifikiria nakosa majibu ni gharama ya kuchimba kisima na Ile mitambo yao kiujumla, Sote tunajua kuwa katika mitambo inayouzwa bei ghali ni mitambo ya kutengeneza Barabara na ya migodini, ikiwemo Wheel loader, Excavator, Bull dozer(mashine ya kipekee ambayo ukiwa Dar unaweza kuiwasha kuweka mafuta na kuweka gia na kuielekezea Mwanza Kisha ukapanda ndege na baada ya muda litafika tu Mwanza lenyewe maana Kila mahali linapita). Sasa hii mitambo gharama ya kukodisha Kwa siku ni kati ya laki 8 Hadi milioni.

Sasa twende huku kwenye visima vya maji, wao wanakuambia Kwa MITA 50,000 Hadi 85,000 hivyo mpaka kisima unamaliza ni milioni 10+.

Sasa je ni Nini hasa kinachokuwa gharama kwao mpaka kupelekea gharama ishoot milioni 10 Kwa kisima, maana haiingii akilini, Nilielewa hii nitakaa kimya
Gharama ya kuchimba kisima inategemea aina ya kisima, kina (urefu kwenda chini), aina ya mwamba eneo la kisima (geology), aina ya mashine itakayochimba na mabomba yatakayotumika.

VISIMA VIFUPI
Visima hivi huchimbwa kwenye michanga/udongo

1. Kisima kifupi aina ya ring well ndiyo bei rahisi kuliko vyote kwani uchimbaji wake ni wa mikono. Bei ni kama laki tano na kushuka chini.

2. Kisima kifupi aina ya tube well inaweza kuchimbwa kwa mashine ya mkono au ya mafuta (diesel/petroli). Kina cha kisima ni chini ya mita 20. Bei ni kama 2 milioni inategemea kina na mabomba yatakayotumika.

VISIMA VYA KATI
Visima hivi huchimbwa kwa mashine (rig) kwenye mchanga (Maeneo ya pwani na mabonde/mbuga na miamba laini)
Visima vya aina hii hufikia kina cha mita 50. Bei yake hufikia milioni 5.

VISIMA VIREFU

Visima hivi huchimbwa kwa mashine kubwa (rig) kwenye michanga, miamba laini na miamba migumu. Kwa Tanzania visima hivi hufikia kina cha mita mpaka 300. Bei ya kuchimba kisima hufikia hadi zaidi ya milioni 20.

Sababu kubwa ya bei ya visima kuwa ghali ni kwa kuwa vifaa vya kuchimbia ni kubwa. Vifaa hivyo ni Rig, mabomba ya chuma, mabomba ya kuweka ndani ya kisima, bits za kuchimbia, hammer, bentonite (matope ya kuchimbia), diesel na mafuta mengine kama hydraulic oil nk.
 
Gharama ya kuchimba kisima inategemea aina ya kisima, kina (urefu kwenda chini), aina ya mwamba eneo la kisima (geology), aina ya mashine itakayochimba na mabomba yatakayotumika.

VISIMA VIFUPI
Visima hivi huchimbwa kwenye michanga/udongo

1. Kisima kifupi aina ya ring well ndiyo bei rahisi kuliko vyote kwani uchimbaji wake ni wa mikono. Bei ni kama laki tano na kushuka chini.

2. Kisima kifupi aina ya tube well inaweza kuchimbwa kwa mashine ya mkono au ya mafuta (diesel/petroli). Kina cha kisima ni chini ya mita 20. Bei ni kama 2 milioni inategemea kina na mabomba yatakayotumika.

VISIMA VYA KATI
Visima hivi huchimbwa kwa mashine (rig) kwenye mchanga (Maeneo ya pwani na mabonde/mbuga na miamba laini)
Visima vya aina hii hufikia kina cha mita 50. Bei yake hufikia milioni 5.

VISIMA VIREFU

Visima hivi huchimbwa kwa mashine kubwa (rig) kwenye michanga, miamba laini na miamba migumu. Kwa Tanzania visima hivi hufikia kina cha mita mpaka 300. Bei ya kuchimba kisima hufikia hadi zaidi ya milioni 20.

Sababu kubwa ya bei ya visima kuwa ghali ni kwa kuwa vifaa vya kuchimbia ni kubwa. Vifaa hivyo ni Rig, mabomba ya chuma, mabomba ya kuweka ndani ya kisima, bits za kuchimbia, hammer, bentonite (matope ya kuchimbia), diesel na mafuta mengine kama hydraulic oil n
Bila shaka mkuu wew ni driller ama hydrogeologist
 
Mkuu inategemea na water table ya maji, kuna mahsli maji yanapatikana 200m huwezi kamwe kuchimba hata kwa 5m
Waongo Hao mkuu, Wana kuambia maji yako mbali Sana ili wapige pesa
 
Kampuni Ipo Wapi?
Watumia Gari Ama
Mkuu mental case huyo.Pole sana,japo Dodoma inasemekana mwamba wa maji upo juujuu sana,lakini kwa 350,000/= sidhani.Ngoja waje wakazi wa Dodoma,wakudaeavulie.Ila laki 3 na nusu,sidhani.
 
Filter wapi wachina wanadawa zao wanamwagia kwenye kisima sema inatakiwa wiki 1 kisima kisitumike toka muda walipoweka dawa..baada ya apo ukikutana na chumvi sijui magadi niite mbwa..mimi nilishawai kumchukua senior graduated kutoka chuo cha maji aje anipigie survey kabla ya kuchimba akasema apa maji yapo kuanzia mita 100 na kuendelea..kuna jamaa yangu akaniletea survey wa iyo kampuni ya kichina MR LIU akasema apa tunachimba mita30 tu maji yapo ya kumwaga..
Magraduate wengine jau sana,halafu unakuta wanalalamika eti oooh! kazi hatupewi wazawa..... jinga kabisa.
 
Sio kam nakupinga ila jua jao wanaofanyq survey sio kama wanaona huko chini bali wanafanya predictions kutokana na data walizopata kwahiyo huwa zinatofautiana kulingana na composition ya mwamba husika unaweza jua ni data zinazoashiria uwepo wa maji kumbe ni uwepo wa composition flan ya mwamba.

By the way survey ya maji ni kama betting
sawa mkuu,
sio hilo la visima tu hata bwawa.
Jamaa fulani na jina na mkumbuka aliaminiwa akapewa fedha na shirika moja hivi linaitwa karitas.

Yule jamaa hakua na utaalamu wowote uchimbaji bwawa, kwasababu ya pesa alikusanya mafundi ujenzi wengi na alikua na kile kikatapila kidogo ki1, Lori alikua anakodi kwa wajenzi wa barabara.
Maji alikua ana tank ambalo lilikua kwenye gari lake Land cruzer 24/7.

Kilichotokea kajenja ukingo eti kuzuia maji mikondo miwili mikubwa mno, kitua ambacho kilisababisha maji kujaa kwenye bwawa na kwasababu halikua na kina maji yalianza kurudi kumeza kijiji na baada ya muda mfupi hata mvua hazikua kali kingo ilichimbwa kwa chini bwawa likapasuka hata halijaanza kutumika,

Kulitokea uharibifu mkubwa mno wa mazingira, mpaka wa leo mmomonyoko unaendelea kukimomonyoa kijiji kile kutokana na uharibifu ule.
Yule jamaa alitokomea pasipojulikana na mpaka wa leo kijiji kile, shida ya maji ni kali mno kila mwaka kuanzia April-dec mvua zinapoanza kunyesha.

Ndugu zangu,
Nilikua mdogo nikiyaona hayo ya kawaida yakitendeka, leo hii nimekua mkubwa.
Mwaka wa2025, ile kitu muhimu zaidi naomba kutoka kwako ni MAOMBI basiii!!!!
hizi mambo nyingine niachieni nitafanya mwenyewe kwa Baraka na Neema za Mungu, ili kusudi nikawakomboe wale ndugu zangu wasio na mtetezi, wasio na mtu wa kuwafuta machozi, wasio na mtu wa kusikiliza kilio chao, wakiteseka zaidi sana na shida ya Maji safi na salama, uhaba wa huduma bora za afya na Elimu.

Haina maana kwamba masuala ya kilimo, biashara, ufugaji, miundombinu, Michezo n.k. hakuna tatizo,
la hashaa ni vipaumbele tu kulingana na uhitaji wao ...
Asante sana kuniombea na Mwenyezi Mungu akubariki sana.....
 
Mkuu mental case huyo.Pole sana,japo Dodoma inasemekana mwamba wa maji upo juujuu sana,lakini kwa 350,000/= sidhani.Ngoja waje wakazi wa Dodoma,wakudaeavulie.Ila laki 3 na nusu,sidhani.
Nimekuelewa
 
Back
Top Bottom