Ahsante sana.
Nimepata kusoma kitabu chake bwana Stephen hawking,mzee huyu yupo vyema katika ubongo wake.
Kama hukupata kusoma somo la fizikia (physics) katika level ya secondary na A-level yawezakuwa kwa sababu za msingi au zisizo za msingi au mazingira ya Elimu yetu haswa ya sayansi kitabu hiki kidogo kitakupa taabu walau kuna urahisi kwa mtu aliyesoma A-level physics ama kama unajishughulisha sana na usomaji binafsi.
Stephen Nadhani mwaka "2014" kama kumbukumbu yangu ipo sahihi alijitambulisha kama Atheist.kitabu kipo vizuri kinakufungua ubongo na kinakupa hali ya udadisi wa Ulimwengu wetu huu na n.k
Kuhusu hatima ya dini, dunia ya kwanza dini ipo inakata pumzi watu wengi wanawajabika vizuri katika maisha yao hakuna cha "ipo siku yangu" au "yote yanapangwa na muumba"
Hatima ya dini bara la Africa naona bado kunasafari ndefu kilakukicha(makanisa na ufanano kama huo unaongezeka),watu wanapata pumziko Lao la ugumu wa maisha katika dini,inabidi watu wajifunze kuwajibika kwa changamoto zote za maisha yao kwanza.
Wakati ni sasa pakua kitabu hicho.