Nini hatma ya miradi ya Chato?

Nini hatma ya miradi ya Chato?

Hii Miradi ambayo haijapitishwa na Bunge Rais wa sasa asiipitishe
ni wapi tuiiona Bajeti ya Reli ya SGR toka Mwanza, mara Daraja la Busisi hivi ni kwanini lisijengwe daraja ya Bagamoyo hadi Zanzibar, huko kwenye kupitisha Mbuga za wanyama kwa awamu hii iliyobaki pasipelekwe tena fedha kwani hazitalipa chochote
 
Badala uwaze maombi wewe wawaza Mali za duniani naomba utuache tuko na msiba mnene mpendwa wa taifa kaondoka niko na majonzii.
Mpendwa wa taifa!?

You can't be serious [emoji3]
 
Upinzani dar Wana majimbo gani Hadi dar iwe upinzani?
Kwani mwaka 2020 tulikuwa na uchaguzi au kubandika majibu yaliyoandaliwa? Mama amesema tuweke yote nyuma tuanze upya kwa mshikamano. Anajua maana yake.
 
Badala uwaze maombi wewe wawaza Mali za duniani naomba utuache tuko na msiba mnene mpendwa wa taifa kaondoka niko na majonzii.
Tumalize msiba kwanza.
Tungemuaga uwanja wa Mkapa kama ilivyokuwa kwa Nyerere na Mkapa.
 
Hiyo miradi bora imaliziwe itumiwe na wakazi wa maeneo hayo na jirani, jengo kama lile la hospitali ya Rufaa kuliacha bila kumaliziwa itakuwa ni dhambi kubwa sana, ila kwa miradi mingine ambayo ilikuwa bado haijaanza kama ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu hiyo inaweza kusitishwa ujenzi wake kwasababu sio ya muhimu sana.
Una maana aliamua jambo lisilo muhimu?
 
Hiyo miradi bora imaliziwe itumiwe na wakazi wa maeneo hayo na jirani, jengo kama lile la hospitali ya Rufaa kuliacha bila kumaliziwa itakuwa ni dhambi kubwa sana, ila kwa miradi mingine ambayo ilikuwa bado haijaanza kama ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu hiyo inaweza kusitishwa ujenzi wake kwasababu sio ya muhimu sana.
Chamuhimu hapo Ni hiyo hospitali vingine avikaushie
 
Jamaniiii huyu baba ameniumaaaaaa, achilia mbali mambo ya siasa huyu ni mtoto wa mtu, ana mama jamani, mama yake ni mzeee sana[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24] mama yake atalia sana, huyu sio Rais tu bali ni mtoto wa mtu. Ana familiya ana watoto.

Sasa kama mimi nalia hivi huko familiya yake wana hali gani? Kifo ni fumbo. Mungu mpokee huyu mtoto kama sisi tulivyozaliwa.
Akung'ate kabisa. Asikuume tu.
 
Nimeshindwa kulala hadi nalia machozi. Hivi nyie mnajua mtoto wa mtu anauma kiasi gani? Mama yake ataambiwa nini yule mzee??
Kulia umependa, msiba wa Mama Janeth kule Chato, wewe uko Tandahimba au Tunduru unajiliza. Unajifanya una machungu so ajabu hata hujui kesho utapata wapi japo mlo mmoja wa familia yako.
Fanya yanayokuhusu.
 
List ya miradi na pesa zake Chato

IMG_20210319_200201.jpeg
 
Kuendelea si issue bali safari zitakuwepo na zitalipa?
Uwanja wa Chato ni muendelezo wa uwanja wa Mwanza. Ili uwanja wa Mwanza uwe na uwezo kupokea ndege kubwa za masafa marefu, lazima kuwe kuna uwanja jirani unaoweza kupokea ndege kama zikishidwa kutua Mwanza. Kama ilivyo viwanja vya (Kilimanjaro na Arusha) au (Dar na Zanzibar).

Kujibu swali lako, kiwanja cha Chato kinauwezo wa kujiendeleza na kuleta faida kama vilivyo viwanja vya Arusha, Songwe, Mwadui, na Kigoma. Kiko kwenye ukanda tajiri, pamoja kuwa karibu na nchi zaidi ya tatu.
 
Back
Top Bottom