Nini kifanyike kuondoa wimbi la wanafunzi kufanya udanganyifu kwenye mitihani vyuoni?

Ushauli wangu mfumo wetu wa elimu ufumuliwe utoke kwenye kutafuta vyeti na ufaulu ili kuajiliwa na twendende kwenye mtu kua na uelewa,ubunifu na stadi za maisha ya kujikimu nje na ivyo kila mtu ataendelea kujipatia vyeti tu kwa njia atakayoijua
Sahihi 💯
 
Watu maskini atupendani kwakweli yaani tunachukiana masikini aliebahatika kuukwepa ufukara ataki wenzie nao waukwepe kama alivyokwepa yeye (UMO VYUONA HAO MA PRO NA WAHADHILI WOTE WAMEFANYA UDANGANYIFU ADI WAMEFIKA APO KUFUNDISHA MASIKIKINI WENZAO)
Kwahiyo Mkuu wewe unaona ni sawa?
 
Hasara wanapata wao.

Vyeti vimeshakuwa vingi, siku hizi waajiri wanaangalia ujuzi.

Kama unachukulia kirahisi mambo ya darasani hutomaliza ukiwa na ujuzi.
 
Watunga mitihani wabadilishe mifumo, watoe mitihani inayoruhusu wanafunzi kuingia na madesa
 
Ni kwa sababu ya wasimamizi kutokuwa serious. Wakiamua kuwa serious huwezi kuingia na simu ukasalimika. Siku hizi hata wahadhiri washaona havina haja kukamiana maana unamkamia mtoto wa watu, alafu mtaani anaenda na vyeti vyake hana cha kufanya. Lakini hizi ni mambo za ajabu; a University student entering an examination room with a phone for cheating ni upuuzi.
 
Watunga mitihani wabadilishe mifumo, watoe mitihani inayoruhusu wanafunzi kuingia na madesa
Wakati tunasoma kuna lecturer mmoja alitunga test akasema hii we njoo na simu, njoo na vitabu, njoo na madafutari chochote tu utakachoona kinafaa. Kweli bwana tukaruka na madafutari, wajanja walibeba simu it was ok. Lakini 2 zilitawala tu, milio kila kona. Lecturer mpaka anakwambia natoa open test unatafakari mara mbilimbili. Sahivi li gpt lishavuruga mchongo.
 
Ushauli wangu mfumo wetu wa elimu ufumuliwe utoke kwenye kutafuta vyeti na ufaulu ili kuajiliwa na twendende kwenye mtu kua na uelewa,ubunifu na stadi za maisha ya kujikimu nje na ivyo kila mtu ataendelea kujipatia vyeti tu kwa njia atakayoijua
Ni nzuri kabisa hii. Wenzetu niliona University of Nottingham, + Birmingham masters hakuna mambo ya UE, wala tests. Wana mfumo mzuri unapresent kile ulichokisoma wanafanya evaluation; ukiwa mzembe masters ni mwaka mmoja ila kama mzembe unaweza soma miaka mitano na husitoboe. Mfumo wao unazalisha watu smart kwa nyanja zotezote
 
Kwa jicho lingine ni ngumu kwasababu kila awamu serikali inataka ionekane viwango vya ufaulu vimeongezeka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…