Nini kifanyike kuondoa wimbi la wanafunzi kufanya udanganyifu kwenye mitihani vyuoni?

Nini kifanyike kuondoa wimbi la wanafunzi kufanya udanganyifu kwenye mitihani vyuoni?

Kwa jicho lingine ni ngumu kwasababu kila awamu serikali inataka ionekane viwango vya ufaulu vimeongezeka
Nadhani kwa vyuoni hiki kitu hakiapply au nimekuelewa vibaya Mkuu?
 
Kama uliyaona kwa macho unaambiwa vingine vipi hiyo Historia wanayosoma huko potelea mbali kwao.

Maisha yenyewe tu yamejaa Uongo mwingi.
Na kwa shule hizi za kwetu ni Assembly line factory ya Ombaomba.

Kama bibi yao haoni aibu kudanganya acha wajukuu waishi humo.
 
Duh Mkuu,

Hatuwezi kufika kwa Style hii aisee na hapo hatujengi bali tunaendelea kubomoa
 
Duh Mkuu,

Hatuwezi kufika kwa Style hii aisee na hapo hatujengi bali tunaendelea kubomoa
Unapotaka wewe kuanza kujenga ni juu na hilo ni kaburi.
Anza na mwanao kama tatizo la kaya kabla hayajaungana na kuwa matatizo ya Kitaifa.
 
Mtihani uwe mmoja nchi nzima kwa kufuata mtaala wa kozi husika, yaani mfano wanaofanya mtihani wa shahada ya sheria tunakuwa na mtihani wa Taifa wa kada hiyo, hii itaenda kwa kozi zote zenye ufanano kama HR, Social Work, Public Administration etc. Hii iende kwa kozi zote as per TCU/NACTE guidelines.

Mamlaka ya kuandaa mtaala na kutunga mitihani yawe chini ya taasisi ya Serikali kama vile TCU na wahadhiri na vyuo wabaki kuwa wafundishaji tu kama ilivyo kwa elimu za Msingi na Sekondari. Hivyo walimu na vyuo watakuwa hawajui kwa uhakika maswali ya mtihani kwakuwa haupo ndani ya mamlaka yao. Maana wahadhiri na ofisi za mitihani mara nyingi ndiyo huwa watuhumiwa wa kuvujisha mitihani.

Hii itasaidia kufanya uwiano wa wahitimu na kuwa na product moja inayokidhi mahitaji ya Taifa, tofauti na hali ilivyo sasa kwa vyuo kujiamulia mambo. Hii itapunguza vitendo vya rushwa vyuoni, unyanyasaji wa kingono na baadhi ya wahadhiri kujikuta miungu watu.

Pia vyombo vya Ulinzi na Usalama vihusishwe kwenye kutunga, kuhifadhi, kusafirisha, usahihishaji na usimamizi na upangaji wa matokeo wa mitihani hiyo. Hii itapunguza mwanya wa mitihani kuvuja na kuepuka vitendo vya udanganyifu ndani ya vyumba vya mitihani.

Jitahada hizi ndizo zinaweza kubadili mwelekeo wa elimu yetu kwa kupunguza uholela wa kupata wahitimu wasio na viwango. Maana ni hatari kupata Daktari, Mhandisi, Mwalimu ama Mkemia aliyeweza kuhitimu kwa hisani ya Chatgpt na udanganyifu katika safari yake ya kitaalamu.

Tukiendekeza uzembe wa kusimamia upatikanaji wa wataalamu wetu, kwa hakika tunaenda kulichimbia kaburi na kulizika Taifa letu kwa mikono yetu wenyewe.
 
Habari zenu Wadau wa JamiiForums

Siku hizi kumekuwa na wimbi kubwa la wanafunzi nyakati za mitihani kuingia na simu za mkononi katika chumba cha mtihani. Hizo simu zinawasaidia kujibu maswali watakayoulizwa katika mtihani huo.

Unaweza ukakuta robo ya watahiniwa wameingia na simu chumba cha mtihani. Hili swala nì baya sana lakini naona limeshamiri katika vyuo vingi!

Siku hizi hata vyuo vikubwa nchini hii tabia ipo, je, nini kifanyike kupambana na hili jambo?

Teacher Foffana
Mitihani ifutwe itafutwe njia nyingine itakayokuwa rafiki na kuongeza ubunifu kwa wanafunzi, kwani hata hiyo mitihani inawafanya waone GPA kubwa kama ndio major goal na siyo skills, unakuta mtu ana A ya somo ambayo kwenye field hana input inayofanania A yake au GPA yake.
 
Mitihani kuwepo ni muhimu Mkuu
 
Back
Top Bottom