Nini kilikuwa chanzo cha mapato ya Bwana Yesu?

ila habari za Mohammad zipo sio za kusadikika ?.

Wavaa vibaragashia utawajua tu. Wapo kwenye ule Uzi wa Russia na Ukraine na kwambia ni kumfagilia Putin si mchezo .
Kumbe wana reasons behind kwamba US na NATO wamewaua sana ndugu zao katka imaaan .
 
Nimecheka kifala saana [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Yesu alikuwa seremala alitengeneza meza sturi masofa vibubu... nk hakutegemea madhabau km hawa manabii fake wanaotegemea zaka na sadaka..
 
Yesu alikuwa seremala alitengeneza meza sturi masofa vibubu... nk hakutegemea madhabau km hawa manabii fake wanaotegemea zaka na sadaka..
Ukimuongelea Yesu usimfananishe na yeyote awe wewe, mchungaji wako,padri wako,nabii wako'mtume wako,mwinjilisti wako,Mwalimu wako au dini yako au yeyote umjuaye.Yesu anabaki kama alivyo hakuna awezaye kumfikia sifa zake.Duniani hayupo.Halinganishwi na kitu chochote wala yeyote
 
Yesu aliweza zalisha hela kwa namna mbalimbali,sababu alikuwa genius, biashara yoyote kama angefanya au alifanya angefanya au alifanya kwa mafanikio makubwa.
Kuna mfano mmoja anautoa kuhusu mtu aliyeachiwa talanta kadhaa na bosi wake na akazitunza tu bila kuzizalisha ,anasema angemuazima hata mkopeshaji ili Ile hela izae kuliko kuifukia tu chini.
Pia Yesu angeweza pata hela kwa Imani tu,kama alivyoamuru ikachukuliwe kwa samaki atayevuliwa
 
Ukijiua unaenda mbinguni?
Biblia ipo wazi kuwa.
Baada ya Yesu kufa alienda kuzimu, napo alipofika aliwahubiria injili wale ambao walikuwa kule..

Na ukiona calculation za ki mbingu, Yuda kama alitengenezwa kumsaliti Yesu na kusudi apate kutubia ikabidi ajiue kitendo cha kujiua akawa amejitanguliza kuzimu na probably Yesu alivyofika kuzimu ni lazima Yuda aliiomba toba na akawa mmoja ya waaminio wapya kutoka kuzimu.

Sent from my TECNO RC6 using JamiiForums mobile app
 
Hatujui maana alijinyonga mwenyewe, kwahiyo hapo niyeye na YESU watajua walikopelekana

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
Biblia ipo wazi kuwa.
Baada ya Yesu kufa alienda kuzimu, napo alipofika aliwahubiria injili wale ambao walikuwa kule..

Na ukiona calculation za ki mbingu, Yuda kama alitengenezwa kumsaliti Yesu na kusudi apate kutubia ikabidi ajiue kitendo cha kujiua akawa amejitanguliza kuzimu na probably Yesu alivyofika kuzimu ni lazima Yuda aliiomba toba na akawa mmoja ya waaminio wapya kutoka kuzimu.

Sent from my TECNO RC6 using JamiiForums mobile app

Sent from my TECNO RC6 using JamiiForums mobile app
 
Naona
Unaanza kumfitini Yesu.
Yesu aende kuzimu kutubisha watu enzi za Yuda alafu sisi huku tukidedi tunapambana na hali zetu.


Hapana

Yesu alikuwa amenyooka
Angebaki huko huko hadi Leo ili kuonyesha consistency.
 
Unataka uthibitisho gani kwamba Yesu aliwahi kuwepo duniani?
 
Naona

Unaanza kumfitini Yesu.
Yesu aende kuzimu kutubisha watu enzi za Yuda alafu sisi huku tukidedi tunapambana na hali zetu.


Hapana

Yesu alikuwa amenyooka
Angebaki huko huko hadi Leo ili kuonyesha consistency.
Unasoma biblia ya wapi wewe??
Baada ya Yesu kufa, mission yake ya pili ilikuwa kwenda kuzimu yes kuzimu haswa kutangaza habari za wokovu huko kuzimu.

Maana wale watu wa kuzimu wakiwa duniani hawakupata neema ya wokovu... Ili mradhimu Yesu ashuke hadi kuzimu na kuwahubiria.

Wapo ambao walimpokea na walitolewa kuzimu hapa ndipo nakuja na hoja. Nadhani Yuda ki vyovyote vile alimpokea Yesu huko kuzimu. (Kumbuka Yuda alitangulia kuzimu kabla ya Yesu,na kilichomtanguliza ilikuwa ni kuona anayo hatia dhidi ya mashihi).

Biblia ipo wazi kabisa kuhusu hilo swala la Yesu kwenda kuzimu na kuhubiri.

Sent from my TECNO RC6 using JamiiForums mobile app
 
HUDUMA YA YESU ILIKUWA IKIBEBWA NA WATU WAKUBWA SAAANA KUTOKA KWENYE SERIKALI YA KIRUMI WATU HAO WALIKUWA WAKIMFUATA YESU KWA SIRI MNO NA WENGINE WALIKUWA NI MAAFISA SERIKALINI LAKINI NI WANAFUNZI WA YESU KWA SIRI
WAWEZA KUPITIA MAANDIKO HAPA CHINI 👇🏾👇🏾👇🏾

Luk 8 (SUV)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
² na wanawake kadha wa kadha ambao walikuwa na pepo wabaya na magonjwa wakaponywa; nao ni Mariamu aitwaye Magdalene aliyetokwa na pepo saba,
³ na Yoana mkewe Kuza, wakili wake Herode, na Susana, na wengine wengi, waliokuwa wakimhudumia kwa mali zao.
 

Mkuu tuwekee andiko la biblia linaloeleza kuwa Yesu alishuka kuzimu na kuhubiri injili huko
 
Uko sahihi kutengeneza pesa alikuwa anajua sana mfano siku moja mvuvi mzoefu Petro alikesha usiku kucha kakesha kuvua samaki akauze apige pesa ndefu hakupata hakupata akamwendea Yesu akamwelezea Yesu akamwambia ngoja nikuelekeze eneo la kuvua mchana kweupe utapata mzigo wa samaki wa kutosha mchana kweupe jua linawaka wa kupata pesa nyingi akamwambia vua hapa eneo hili tweka kilindini nyavu zako .Petro alipata samaki wengi hadi ikabidi aite vyombo vingine vya kuja kusaidia kubeba alipata utajiri mkubwa ghafla hadi akachanganyikiwa kwa wingi wa samaki wale.Yesu alijua ukitaka kupata pesa nyingi utapata wapi hadi eneo anakuonyesha like paleee!!

Sema tu watu siku hizo sababu hawaelewi Yesu vizuri utasikia ohh Mungu kanionyesha kuna mtu humu kanisani kuna mtu ana dhambi!!! Badala ya kuomba Mungu awaonyeshe wapi watapata pesa wanakaa kutaka kuonyeshwa nani ana dhambi Sadaka na mafungu ya Kumi kutoa wagumu hao ukiwahimiza kutoa wanasema kanisa limekalia kudai pesa pesa tu kumbe malofa hawana kitu mfukoni!!! Ni wakali kali sana kujifanya wa kiroho sana !!! Ila utoaji pesa sifuri iwe sadaka fungu la Kumi au chochote
 
Mkuu nahisi zamani mtoto alikuwa anarithi taaluma afanyayo baba ake na mtoto wa kike kwa mama hivyo hivyo. So kuna asilimia kubwa bwana Yesu nae alikuwa seremala.
Zamani WAYAHUDI waliwafundisha watoto wao skills za mikono.

Hata Mtoto wa tajiri mkubwa utakuwa anajua skills ndogondogo ambao lengo zimsaidie ikitokea uchumi umeporomoka.


Ndio maana hata Paulo alikuwa Mtoto wa tajiri tena kasoma Shule sawa na Feza boys au IST kwa DSM lakini aliponza mambo ya Yesu na jamaa zake kumchenjia Alikuwa anashona vikapu na mikeka na kujipatia vipato huko efeso


Mfuasi wa Yesu sio kila kitu utegemee Fundi. Unatakiwa kujua abcd za mambo madogomadogo
 
Mkuu tuwekee andiko la biblia linaloeleza kuwa Yesu alishuka kuzimu na kuhubiri injili huko
1petro 3:18-20

18 Kwa maana Kristo naye aliteswa Mara moja kwa ajili ya dhambi,mwenye haki kwa ajili yao wasio na haki,ili atulete kwa Mungu; mwili wake akauawa,Bali roho yake akahuishwa,
19 ambayo kwa
hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, akawahubiri; 20watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji.

hapo tunaona mission
ya Yesu baada ya kwenda kuzimu,alihubiri injili kuanzia watu waliokuwa tangu kipindi cha nuhu hadi ambao siku anakufa..

baada ya hapo injili imefungwa na tumebakiwa na kipindi cha neema pekee. Means kwamba hivi SASA injili tunaipata kabla ya umauti tukishakufa hatuwezi kupata injili Tena.!
 
JESUS IS GOD!

The true meaning of the name Jesus is "Jehovah Saviour"


After all hili bandiko liko vizuri

Yesu ni Bwana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…