Nini kilikuwa chanzo cha mapato ya Bwana Yesu?

Nini kilikuwa chanzo cha mapato ya Bwana Yesu?

Yesu hakuwa maskini alikuwa Tajiri mno fikiria alipigwa msalabani nguo.zikalowa damu lakini Askari wa kirumi ambao walikuwa walipwa mishahara walimua kugawana nguo zake!!

YESU alivaa nguo za maana za bei kiasi wale askari malofa waliomuua waligawana zikiwa na damu hivyo kila mmoja anasema nitaenda kifua!!! Wangekuwa na pesa za kununua nguo kama zile wasingegawana alipokufa
Ila ile kanzu aliokuwa nayo akiongezeka nayo inaongezeka na haikuwa na mshono wowote, waliipigia kura huyo aliyeichukua sijui ilikuwaje hakuwa anaota anapigwa mijeredi kweli?

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
 
Mi mgumu wz kuelewa ndo maana sijihusishi sana na mambo ya dini naogopa kuharibu;

'Mariamu aitwaye Magdalena'?!!!!!!!! Naomba msaada wa kuelewa tafadhali
Yesu-mnazareth, Nazareth ni sehemu alikotoka. Simioni-mkanaani, simoni aliyetokea kanaani(mwanafunzi wa Yesu) Joseph-Alimataya, alimataya sehemu alikotokea(huyu tajiri aliyetoa kaburi lake Yesu kazikwa). Mriamu huyu alitokea Magdalena sehemu pia.
 
Fuatilia mkuu itajua kuwa hiyo familia haikuwa masikini hata kidogo. Donor mkubwa wa mission ya Jesus alikuwa Lazaro. Ni yeye aligharamia vinywaji kwenye harusi ya Kana, ilhali Yesu alikuwa ameahidi kuchangia vinywaji, na ndio ukafuata ule muujiza wa kwanza.
Hii familia walikuwa half Jews kwa mama, na walikuwa ni decendants wa Royal family probably ubabani. Kwa hiyo walikuwa matajiri sana waliishi kwenye makasri. Lazaro na Martha walichagua kuwa wachamungu, Mary of Madgala (Maria Madgalena) alichagua "kujirusha".
Mkuu Bethania iko mkoa waYuda.
Kana iko mkoa wa Galilaya.
Hakukuwa na mawasiliano.

Wanaweza kuwa matajiri lakini kusponsor mambo ya Kana ni issue.

Hapa kuwa na uhusiano.
 
Hawakufuata nguo zake nyumbani waligawana zile zile aliizokuwa kazivaa

Zilikuwa na Jasho la damu pale alipoomba usiku kucha zile walizomvua wakagawana sababu walikuwa maskini .Yesu aliwazidi kwa kuwa na nguo nzuri kuliko wao waajiriwa wapokea mishahara Yesu angekuwa alikuwa akivaa nguo za kimaskini wasingegawana matambara ya maskini
Eti matambala au tuite midabwada kama ya koffi


Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
 
Yesu alikuwa rafiki wa matajiri.

Kisaikolojia hakuna urafiki wa matajiri na masikini.

Yesu aliheshimiwa akifika kwamatajiri anapewa siti nzuri nzuri.


Anakuwa mgeni rasmi. Hakunaga mgeni rasmi masikini.

Mfano
Kwa Simon Mkoma na Razalo
 
Fuatilia kwa miaka 3 aliyofanya kazi ya kueneza neno la Mungu hakufanya kazi nyingine zaidi. Alikuwa ni nenda huku au huku. Hakuishi kwao tena. Mpaka wazee wa familia (ndugu zao) wakamwita kumuambia achane na kuhubiri injili amtunze mama yake. Na ndio sababu ya muujiza wa Kana, maana hata nduguze walikuwa hawa mwelewi! Ule muujiza ulisaidia sana ndugu kuanza kuelewa kuwa huyu si binadamu kama wengine, na ana mission maalumu!

Wale thenashara na wafuasi wengine walikuwa wanaendelea na shughuli zao za kawaida muda mwingi. Alikuwa anakuwa nao "occasionally". Ila mara zote hakuwa pekee, alikuwa ana andamana na 2 au 3. Jaribu kuchimba zaidi utajua.
Ule muujiza wa kana ndiyo ulikuwa wakwanza kwa watu, mpaka alimwambia mama yake nina nini nawe? Muda wangu haujafika, ila ndiyo hivyo mama alishatoa amri kwa mtoto

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
 
Ndiyo maana alimwambia mtu mbweha wanamapango lakini mwana wa Adamu hana hata pakuweka kichwa.
Kwa hio Yesu hakua hata na gheto?
Alikua anaishi kwa kuungaunga kama Yahaya wa Jay Dee?
 
Simba wa yuda alikuwa na pesa sababu alikuwa anatoza kodi huyu yuda yeye kazi ni mikopo mikopo kwenda mbele
 
Kwa hio Yesu hakua hata na gheto?
Alikua anaishi kwa kuungaunga kama Yahaya wa Jay Dee?
Gheto lilikuwa kwao, ila huko alikokuwa anahubili angeweka vipi gheto, leo mbagala kesho gongo la mboto, asubuhi anaamkia tegeta atajenga magheto mangapi hapo!

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
 
Yesu alikuwa rafiki wa matajiri.

Kisaikolojia hakuna urafiki wa matajiri na masikini.

Yesu aliheshimiwa akifika kwamatajiri anapewa siti nzuri nzuri.


Anakuwa mgeni rasmi. Hakunaga mgeni rasmi masikini.

Mfano
Kwa Simon Mkoma na Razalo
Kwasababu za kisiasa. Hata wewe leo ukionekana una influence kubwa sana ya watu kukubalika na kupendwa lazima MATAJIRI na Wenye nguvu ya madaraka watataka ukariku na wewe.

Hata Yesu kuuawa Ni siasa zilihusika. Ilionekana anapendwa sana na watu, wanamfuata na kumuita Mfalme Mfalme wakati huo tayari kama eneo lilikuwa na Mfalme wao ( Herode )

Kwahiyo, hisia zilikiwepo tu kuwa huyu mtu anatishia madaraka yangu.

Kumbuka, tangu Yesu anazaliwa ziliposikika habari kuwa kazaliwa Mfalme basi Wenye madaraka waliua sana watoto wa kiume ili kuepusha Hilo tishio la madaraka.

Hapo ndio utajua siasa Zina laana aisee.
 
Yesu alikuwa na Pesa nyingi sana kuliko watu wa dini wanavyotueleza.


Ushahidi.
1: Alikuwa na Muhasibu. MTU binafsi bila kampuni wala biashara kufikia hatua ya kushindwa kutunza kipato chako hadi Uwe na Muhasibu basi utakuwa na Pesa nyingi sana.

2: Aliwazuia mitume wasifanye biashara zao. Aliwakuta jamaa wakinapetro ni wakokozi na wavuvi nguli akawaambia waache alafu wamfuate.
Kulisha breakfast, lunch na dinner wanaume 12 wasio na Kazi miaka mitatu mfululizo inabidi Uwe na Pesa. Ushahidi Baada ya kufa Petro aliwashawishi warudi kwenye Biashara zao.

3: Hakuna kifungu Yesu kaishiwa Pesa au kashindwa kufanya muamala wowote kisha hana salio. Aliwahi kudaiwa kodi ya hekalu, akamtuma Petro akavue samaki aliyekuwa na Pesa tumboni.

4: Muhasibu wake alikuwa mwizi na mwenye uchu wa Pesa. Huku tunaona makampuni maduka Yenye wahasibu wezi huwa yanafirisika. Yuda hakuwahi kufirisi mkoba wa pesa za mwalimu wake Yesu.



Wakuu Yesu alikuwa yuko vzr kiuchumi.


Sasa najiuliza nini nilikuwa chanzo chake cha fedha ikiwa

Alikuwa hana biashara
Hakuwa na gawio LA sadaka masinagogini na hekaluni?


Je alikuwa anawafadhili?

Je alikuwa anakusanya Sadaka kwenye mihadhara yake?

Je Alikuwa anashushiwa kimiujiza.?
Daaah hii kiboko
 
Yesu alikuwa rafiki wa matajiri.

Kisaikolojia hakuna urafiki wa matajiri na masikini.

Yesu aliheshimiwa akifika kwamatajiri anapewa siti nzuri nzuri.


Anakuwa mgeni rasmi. Hakunaga mgeni rasmi masikini.

Mfano
Kwa Simon Mkoma na Razalo
Hata mazishi yake alizikwa na Tajiri Bilionea Yusuf wa Alimataya kwenye kaburi la matajiri.Hakuzikwa na malofa

mafuta tu ya kujipaka Yesu alikuwa akijipaka ya bei mbaya hadi Yuda Iskariote akashangaa, Maria Magdalena alipokuwa akimpaka yale mafuta akasema mafuta ghali haya Yesu unapaka loo.Yesu akamwambia mwache anipake wewe yuda iskariote kama umezoea kujipaka mafuta ya nazi utajijua akaendelea kujipaka
 
Back
Top Bottom