Nini kilikuwa chanzo cha mapato ya Bwana Yesu?

Nini kilikuwa chanzo cha mapato ya Bwana Yesu?

Yesu alikuwa na Pesa nyingi sana kuliko watu wa dini wanavyotueleza.


Ushahidi.
1: Alikuwa na Muhasibu. MTU binafsi bila kampuni wala biashara kufikia hatua ya kushindwa kutunza kipato chako hadi Uwe na Muhasibu basi utakuwa na Pesa nyingi sana.

2: Aliwazuia mitume wasifanye biashara zao. Aliwakuta jamaa wakinapetro ni wakokozi na wavuvi nguli akawaambia waache alafu wamfuate.
Kulisha breakfast, lunch na dinner wanaume 12 wasio na Kazi miaka mitatu mfululizo inabidi Uwe na Pesa. Ushahidi Baada ya kufa Petro aliwashawishi warudi kwenye Biashara zao.

3: Hakuna kifungu Yesu kaishiwa Pesa au kashindwa kufanya muamala wowote kisha hana salio. Aliwahi kudaiwa kodi ya hekalu, akamtuma Petro akavue samaki aliyekuwa na Pesa tumboni.

4: Muhasibu wake alikuwa mwizi na mwenye uchu wa Pesa. Huku tunaona makampuni maduka Yenye wahasibu wezi huwa yanafirisika. Yuda hakuwahi kufirisi mkoba wa pesa za mwalimu wake Yesu.



Wakuu Yesu alikuwa yuko vzr kiuchumi.


Sasa najiuliza nini nilikuwa chanzo chake cha fedha ikiwa

Alikuwa hana biashara
Hakuwa na gawio LA sadaka masinagogini na hekaluni?


Je alikuwa anawafadhili?

Je alikuwa anakusanya Sadaka kwenye mihadhara yake?

Je Alikuwa anashushiwa kimiujiza.?
Yaani una Question Uwezo wa Mungu ?
Yaani Mungu aliyekuumba wewe, aliyeumba Mbingu na Nchi
Hizo si ni Mali zake Pia
Nikuombe angalia sana usije ukakufuru.
Yesu Ni Mungu katika Umbo la Binadamu.
Hupaswi kabisa ku question Uwezo wa Mungu
 
Yesu hakuwa na pesa.

Kwanza pesa ya Nini?

Maana walikuwa wanatembea kwa miguu mwanzo mwisho.

Walikuwa wanakula kwa wafuasi ( kualikwa nyumbani kwa watu )

Ukitaka kujua hakuwa na pesa, Kuna siku Yesu alidaiwa Kodi akawa Hana na hata wanafunzi wake hawakuwa na kitu.f

Akaamua kumtuma mwanafunzi wake aende mtoni akatupe ndoano, samaki was kwanza atakayetoa amcheck mdomoni atakuta sarafu. Hiyo sarafu ndio alilipa Kodi.

Hakuma sehemu inayoonesha kiwa Yesu alikuwa na wahasibu kwaajili ya kutembea na pesa
Unajichaganya Yesu alikuwa na pesa nyingi wakati ule benki zilikuwa hazipo pesa zake akawa anaweka kwenye matumbo ya samaki wa eneo hilo ndio maana akamtuma mwanafunzi wake kuwa nenda kabvue samaki mmoja tu yeyote wa eneo hilo mpasue ndani utakuta kuna pesa
 
Luka 8:2-3
[2]na wanawake kadha wa kadha ambao walikuwa na pepo wabaya na magonjwa wakaponywa; nao ni Mariamu aitwaye Magdalene aliyetokwa na pepo saba,
And certain women, which had been healed of evil spirits and infirmities, Mary called Magdalene, out of whom went seven devils,
[3]na Yoana mkewe Kuza, wakili wake Herode, na Susana, na wengine wengi, waliokuwa wakimhudumia kwa mali zao.
And Joanna the wife of Chuza Herod's steward, and Susanna, and many others, which ministered unto him of their substance.
Mi mgumu wz kuelewa ndo maana sijihusishi sana na mambo ya dini naogopa kuharibu;

'Mariamu aitwaye Magdalena'?!!!!!!!! Naomba msaada wa kuelewa tafadhali
 
Na mimi nichangie Baadhi ya siri za utajiri wa Yesu

Moja Utajiri wa Yesu uliikuwa kwanza wa kurushi
Yesu alizaliwa kwenye ukoo wa kifalme sio wa maskini walahoi .Alikuwa wa ukoo wa mfalme Daudi ni ukoo uliokuwa na uwezo.

Mariamu alipokuwa na mimba yake pesa wazazi wake walikuwa nazo pesa za kulipia kulala nyumba ya wageni bahati mbaya ikawa imejaa akazaliwa nje kwenye hori la ng 'ombe Uwezo wa kulipia nyumba ya wageni ulikuwepo.Tatizo ilikuwa imejaa

Pili utajiri wa Yesu aliupata toka kwa mamajusi matajiri wa kimataifa waliokwenda kumsalimia
Wale walimpa mafurushi ya Fedha na dhahabu kama zawadi ya happy birthday. Akitaka chochote anachota kwenye fuko la pesa alizopewa na mamajusi na akiona vipi anachukua sehemu ya dhahabu aliyopewa na mamajusi anauza na kupata pesa ndio maana hata waliokuwa wakakimbia kwenda Misri nauli ya kwenda na kurudi hawakupitisha harambee ya mchango wa jumuiya
 
Mi mgumu wz kuelewa ndo maana sijihusishi sana na mambo ya dini naogopa kuharibu;

'Mariamu aitwaye Magdalena'?!!!!!!!! Naomba msaada wa kuelewa tafadhali
Mariam aka Magdalena

Ni sawa na kusema Nassib aka Diamond platinum
 
Wakuu nawakumbusha Pesa nyingine alizipata kwa imani.

Aliwahi kusema unaweza kuuambia mlima ng'oka unang'oka.
Mkuyu ( Notes) ngoja zikatii.

Haishindikani kutamka Pesa za wevi na wanyanganyi wa wakati wake zing'oke na kuingia kwenye kibubu cha Yuda kimuujiza.

Niliwahi kupractice hiyo theory nikasema nikute 10M chini ya Godoro. Azing'oe popote kwa Ajili ya kusupoti Majengo ya kanisa nikakuta Tsh 200. Sikuelewa hapo Mungu alinifunisha nini.

Usicheke maana kama majini huwa yanawaambia wateja wao na wanakuta Pesa makaburini. Yesu ni zaidi.
 
Yaani una Question Uwezo wa Mungu ?
Yaani Mungu aliyekuumba wewe, aliyeumba Mbingu na Nchi
Hizo si ni Mali zake Pia
Nikuombe angalia sana usije ukakufuru.
Yesu Ni Mungu katika Umbo la Binadamu.
Hupaswi kabisa ku question Uwezo wa Mungu
Hii tabia ndio inasababisha tunawapiga makanisani.

Ukristo ni kuhoji.
Mungu ameruhusu sio tu kuomba bali kuhojiana naye.

tuhojiane, elezamambo yako yote.


Yesu katika msafara wake alikuwa na Muhasibu wa mapato yake. Alikuwa na mfumo wa fedha. Na sisi tumeambiwa tumuige. Kabla hatujaonekana wezi au wavivu lazima tujue hizo Pesa zilizowekwa humo alikuwa anazipata kwa means zipi ili tumuige.


Mimi Yote ninayojibiwa humu nitapractice.

Nampenda sana Yesu maana anataka tumuige alafu tuwe thinkers kama yeye.
 
Wakuu nawakumbusha Pesa nyingine alizipata kwa imani.

Aliwahi kusema unaweza kuuambia mlima ng'oka unang'oka.
Mkuyu ( Notes) ngoja zikatii.

Haishindikani kutamka Pesa za wevi na wanyanganyi wa wakati wake zing'oke na kuingia kwenye kibubu cha Yuda kimuujiza.

Niliwahi kupractice hiyo theory nikasema nikute 10M chini ya Godoro. Azing'oe popote kwa Ajili ya kusupoti Majengo ya kanisa nikakuta Tsh 200. Sikuelewa hapo Mungu alinifunisha nini.

Usicheke maana kama majini huwa yanawaambia wateja wao na wanakuta Pesa makaburini. Yesu ni zaidi.
Wewe hizo milioni 10 ulikuwa uzipate chini ya godoro. Ulipoomba ukute milioni 10 chini ya godoro ulipochungulia ukaona shilingi 200 ilitakiwa umshukuru Mungi kuwa zinakuja

Hiyo inaitwa Elijah theory ni hivi Eliya aliomba inyeshe mvua kubwa kwenye Biblia kipindi cha kiangazi alipoomba mtumishi wake akamwambia naona kwa mbali kiwingu kidogo sana angani kimetokezea

Eliya akamwabia mfalme kimbia mvua kubwa inakuja isikukute njiani.Na ilikuja kubwa mno.Hiyo 200 uliyoiona chini ya godoro ungeingia kwenye kushukuru Mungu na kumsifu kuwa anakuletea milioni 10 ingezipata ilitangulia hugo mia 200 zingine zilikuwa zinakuja ni.kiwingu kidogo kilikuwa hicho
 
Hauwezi ukakosa pesa au sponsor, wakati unauwezo wa kutenda miujiza
 
Kwahiyo Yesu hakuwa Masikini kama tunavyoaminishwa?
Yesu hakuwa maskini alikuwa Tajiri mno fikiria alipigwa msalabani nguo.zikalowa damu lakini Askari wa kirumi ambao walikuwa walipwa mishahara walimua kugawana nguo zake!!

YESU alivaa nguo za maana za bei kiasi wale askari malofa waliomuua waligawana zikiwa na damu hivyo kila mmoja anasema nitaenda kifua!!! Wangekuwa na pesa za kununua nguo kama zile wasingegawana alipokufa
 
Hapa nadhani ni pale alipotaka Punda kuingia Naye Yeriko Kifalme. Aliwaambia mumchukue mkimkuta mwenye Naye akiwauliza wamwambie Yesu anamtaka.


Hapa nadhani alimrudisha na hakuwa na haja ya kumiliki punda wakati kesho yake anaanza suluba.
Inaonekana alikuwa ameshaongea na mwenye punda
 
Yesu hakuwa maskini alikuwa Tajiri mno fikiria alipigwa msalabani nguo.zikalowa damu lakini Askari wa kirumi ambao walikuwa walipwa mishahara walimua kugawana nguo zake!!

YESU livaa nguo za maana za bei kiasi wale askari malofa waliomuua waligawana zikiwa na damu hivyo kila mmoja anasema nitaenda kifua!!! Wangekuwa na pesa za kununua nguo kama zile wasingegawana alipokufa
Mkuu hebu jaribu ku-fact check hii argument yako.

Wale askari waligawana mawazi mengi ya Yesu ama ilikuwa ni lile lile moja ndio waligawana?
 
Kuna mstari nakumbuka aliwaambia waende wakanunue vitu kwa ajili ya kalamu na walikuwa hawana kitu.
Akawaambia nendeni tu, Hii naonesha alikuwa na maisha ya kuunga unga tu. Na hakuwa mkwasi.
Si kweli ndugu, maji aliweza kuyageuza divai katika harusi ya kana,Samaki 2 na mikate 3,Petro alipo tumwa kuvua samaki walijaa mpaka nyavu kuchanika, Yeye hakuwa na shida na vitu vya duniani hata kidogo
 
Mkuu hawa walikuwa masikini wanaishi Bethania Jerusalem kijijini huko nje ya ukuta.

Masponsor nadhani walikuwa wale

Simon Mkoma,Tajiri
Zakayo Mzee wa TRA ya uyahudi
Yusuphu wa armathaya huyu alisponsor Kaburi LA matajiri. Yesu alizikwa makaburi ya matajiri wa kubwa sana.

Hakuzikwa kwa makapuku huku kwetu kwa mnyamani graves.
Fuatilia mkuu utajua kuwa hiyo familia haikuwa masikini hata kidogo. Donor mkubwa wa mission ya Jesus alikuwa Lazaro. Ni yeye aligharamia vinywaji kwenye harusi ya Kana, ilhali Yesu alikuwa ameahidi kuchangia vinywaji, na ndio ukafuata ule muujiza wa kwanza.
Hii familia walikuwa half Jews kwa mama, na walikuwa ni decendants wa Royal family probably ubabani. Kwa hiyo walikuwa matajiri sana waliishi kwenye makasri. Lazaro na Martha walichagua kuwa wachamungu, Mary of Madgala (Maria Madgalena) alichagua "kujirusha".
 
Mkuu hebu jaribu ku-fact check hii argument yako.

Wale askari waligawana mawazi mengi ya Yesu ama ilikuwa ni lile lile moja ndio waligawana?
Hawakufuata nguo zake nyumbani waligawana zile zile aliizokuwa kazivaa

Zilikuwa na Jasho la damu pale alipoomba usiku kucha zile walizomvua wakagawana sababu walikuwa maskini .Yesu aliwazidi kwa kuwa na nguo nzuri kuliko wao waajiriwa wapokea mishahara Yesu angekuwa alikuwa akivaa nguo za kimaskini wasingegawana matambara ya maskini
 
Back
Top Bottom