Nini kilikuwa chanzo cha mapato ya Bwana Yesu?

Nini kilikuwa chanzo cha mapato ya Bwana Yesu?

Wewe hizo milioni 10 ulikuwa uzipate chini ya godoro. Ulipoomba ukute milioni 10 chini ya godoro ulipochungulia ukaona shilingi 200 ilitakiwa umshukuru Mungi kuwa zinakuja

Hiyo inaitwa Elijah theory ni hivi Eliya aliomba inyeshe mvua kubwa kwenye Biblia kipindi cha kiangazi alipoomba mtumishi wake akamwambia naona kwa mbali kiwingu kidogo sana angani kimetokezea

Eliya akamwabia mfalme kimbia mvua kubwa inakuja isikukute njiani.Na ilikuja kubwa mno.Hiyo 200 uliyoiona chini ya godoro ungeingia kwenye kushukuru Mungu na kumsifu kuwa anakuleyea milioni 10 ingezipata ilitangulia hugo mia 200 zingine zilikuwa zinakuja ni.kiwingu kidogo kilikuwa hicho
Nimeipenda hii.
Mleta mada pia asante. Leo nimepata kitu kipya kumbe Yuda alikuwa mtunza fedha! Na kumbe Yesu kuna kipindi aliagiza hela zikachukuliwe kwa samaki... Tumboni/mdomoni mwa samaki!!.
 
Hawakufuata nguo zake nyumbani waligawana zile zile aliizokuwa kazivaa

Zilikuwa na Jasho la damu pale alipoomba usiku kucha zile walizomvua wakagawana sababu walikuwa maskini .Yesu aliwazidi kwa kuwa na nguo nzuri kuliko wao waajiriwa wapokea mishahara Yesu angekuwa alikuwa akivaa nguo za kimaskini wasingegawana matambara ya maskini
Mkuu nakuelewa ila hii argument kuwa waligawana lile vazi sababu ya umaskini wao hivyo walitaka kwenda kulivaa ndio nina mashaka. Nadhani kugawana kwa kile vazi kulikuwa na maana nyingine maana ukumbuke kwanza lilikuwa lishachanika nankuchakaa kutokana na mijeledi ya maana ya hao hao askari.

Sasa vazi ambalo lishachakaa wangelitaka vipi kulivaa tena.? Kumbuka pia wale jamaa walikuwa ni askari wanaolipwa mshahara hivyo hawawezi kuwa maskini kihivyo.
 
kwa imani yangu, mafungu ya kumi na sadaka zilikuwa zinaenda kwenye masinagogi, havikua vinatolewa kwa mtu binafsi, hivyo sadaka wala mafungu hayakupelekwa kwa Yesu.

Yesu alizaliwa na kukulia kwenye familia ya selemala. hapo huwezi kusema hakuwa selemala, na huwezi kusema hakuwa anafanya kazi kupata kipato. pia, wanafunzi wa Yesu, mitume walikuwa 12, ila thenashara (wanafunzi wasio mitume) walikuwa 70. hawa wote walikuwa wanafanya shughuli zao binafsi, sio kwamba muda wote kuanzia asubuhi hadi jioni Yesu alikuwa anatangatanga akihubiri tu, hapana, alikuwa anafanya kazi zingine pia. wanafunzi wake wengine walikuwa wavuvi wakubwa tu. nakumbuka kuna siku moja aliwatembelea wanafunzi wake, akawauliza leo tuna chakula gani, wakamwambia Rabi, tumehangaika usiku kucha kuvua samaki hatujapata chochote, basi yeye akawaamuru warushe nyavu na wazivute, waliporusha tu wakapata samaki za kimiujiza hadi nyavu zilitaka zianze kukatika. wanafunzi wake wakashangaa mno. kumbe usiku wote wa jana yake wanafunzi wake ambao walikuwa wavuvi walishinda baharini wakivua, walikuwa na shughuli zingine pia kumbe, sio kwamba walikuwa wakizunguka kuhubiri tu.

pia, kama maisha ya Yesu, au Biblia ingeandikwa kila kitu, wala isingetosha, kuna mengi hayajaandikwa ambayo yalitokea enzi zake, na mengine yanayohusu maisha yake.
Fuatilia kwa miaka 3 aliyofanya kazi ya kueneza neno la Mungu hakufanya kazi nyingine zaidi. Alikuwa ni nenda huku au huku. Hakuishi kwao tena. Mpaka wazee wa familia (ndugu zao) wakamwita kumuambia aachane na kuhubiri injili amtunze mama yake. Na ndio sababu ya muujiza wa Kana, maana hata nduguze walikuwa hawa mwelewi! Ule muujiza ulisaidia sana ndugu kuanza kuelewa kuwa huyu si binadamu kama wengine, na ana mission maalumu!

Wale thenashara na wafuasi wengine walikuwa wanaendelea na shughuli zao za kawaida muda mwingi. Alikuwa anakuwa nao "occasionally". Ila mara zote hakuwa pekee, alikuwa ana andamana na 2 au 3. Jaribu kuchimba zaidi utajua.
 
Na Yesu alikuwa akivaa viatu vya uhakika vya thamani ya juu vya kufunga na kamba hadi Yohana akasema sistahili hata kugusa Ukiona filamu yeyote au picha yoyote ikimuonyesha Yesu yuko pekupeku miguuni hana viatu ujue imetengenezwa na wasiomjua Yesu wanaoamini Yesu alikuwa Maskini!! Yesu alikuwa na viatu vya nguvu

Marko 1:7​

YOHANA AHUBIRI

''Akahubiri akisema, Yuaja nyuma yangu aliye na nguvu kuliko mimi, ambaye mimi sistahili kuinama na kuilegeza gidamu ya viatu vyake.
 
Mkuu nakuelewa ila hii argument kuwa waligawana lile vazi sababu ya umaskini wao hivyo walitaka kwenda kulivaa ndio nina mashaka. Nadhani kugawana kwa kile vazi kulikuwa na maana nyingine
Lete hiyo maana ya zaidi ya kwenda kuvaa waligawana za nini? Kwanza mali ya marehemu ni mirathi ilitakiwa mali za marehemu Yesu ikiwemo hizo nguo ilitakiwa wakakabidhi kwa warithi.Wao wakaamua kugawana!!! Mirathi ya marehemu kabla haijafunguliwa.Kama hawakwenda kuvaa waligawana za nini?
 
Anaenda mgahawani, anaagiza mikate miwili na kikombe cha divai.
Yeye na wafasiri wake wanakula na hakiishi hadi watakapo Shiba.
 
Zaka na sadaka walikuwa wanakula wakina kayafa.

Yeye hekaluni alikuwa anakagua tu watoa sadaka. Akampenda sana bibi mmoja aliyetoa senti yote na kuwaponda matajiri waliokuwa wanatoa sadaka kwa mbwembwe.


Hakuwa kwenye payroll ya Hekalu
Ahahahah
 
Kuna mstari nakumbuka aliwaambia waende wakanunue vitu kwa ajili ya kalamu na walikuwa hawana kitu.
Akawaambia nendeni tu, Hii naonesha alikuwa na maisha ya kuunga unga tu. Na hakuwa mkwasi.
[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Hapa nadhani ni pale alipotaka Punda kuingia Naye Yeriko Kifalme. Aliwaambia mumchukue mkimkuta mwenye Naye akiwauliza wamwambie Yesu anamtaka.


Hapa nadhani alimrudisha na hakuwa na haja ya kumiliki punda wakati kesho yake anaanza suluba.
Ahahahah
 
Unajichaganya Yesu alikuwa na pesa nyingi wakati ule benki zilikuwa hazipo pesa zake akawa anaweka kwenye matumbo ya samaki wa eneo hilo ndio maana akamtuma mwanafunzi wake kuwa nenda kaburi samaki mmoja tu yeyote wa eneo hilo mpasue ndani utakuta kuna pesa
We jamaa usitupige kamba😆😆, ni wapi panaonyesha Yesu alikuwa anaweka pesa kwenye matumbo ya samaki!
 
We jamaa usitupige kamba😆😆, ni wapi panaonyesha Yesu alikuwa anaweka pesa kwenye matumbo ya samaki!
Angeenda kuchukua pesa kwenye hilo tumbo la samaki kama hakuweka? Alikuwa ana witdraw pesa yake aliyo deposit kwenye tumbo la samaki
 
Yesu alikuwa na Pesa nyingi sana kuliko watu wa dini wanavyotueleza.


Ushahidi.
1: Alikuwa na Muhasibu. MTU binafsi bila kampuni wala biashara kufikia hatua ya kushindwa kutunza kipato chako hadi Uwe na Muhasibu basi utakuwa na Pesa nyingi sana.

2: Aliwazuia mitume wasifanye biashara zao. Aliwakuta jamaa wakinapetro ni wakokozi na wavuvi nguli akawaambia waache alafu wamfuate.
Kulisha breakfast, lunch na dinner wanaume 12 wasio na Kazi miaka mitatu mfululizo inabidi Uwe na Pesa. Ushahidi Baada ya kufa Petro aliwashawishi warudi kwenye Biashara zao.

3: Hakuna kifungu Yesu kaishiwa Pesa au kashindwa kufanya muamala wowote kisha hana salio. Aliwahi kudaiwa kodi ya hekalu, akamtuma Petro akavue samaki aliyekuwa na Pesa tumboni.

4: Muhasibu wake alikuwa mwizi na mwenye uchu wa Pesa. Huku tunaona makampuni maduka Yenye wahasibu wezi huwa yanafirisika. Yuda hakuwahi kufirisi mkoba wa pesa za mwalimu wake Yesu.



Wakuu Yesu alikuwa yuko vzr kiuchumi.


Sasa najiuliza nini nilikuwa chanzo chake cha fedha ikiwa

Alikuwa hana biashara
Hakuwa na gawio LA sadaka masinagogini na hekaluni?


Je alikuwa anawafadhili?

Je alikuwa anakusanya Sadaka kwenye mihadhara yake?

Je Alikuwa anashushiwa kimiujiza.?
Baada ya kufa nani alilithi Mali zake?
 
Wakuu nawakumbusha Pesa nyingine alizipata kwa imani.

Aliwahi kusema unaweza kuuambia mlima ng'oka unang'oka.
Mkuyu ( Notes) ngoja zikatii.

Haishindikani kutamka Pesa za wevi na wanyanganyi wa wakati wake zing'oke na kuingia kwenye kibubu cha Yuda kimuujiza.

Niliwahi kupractice hiyo theory nikasema nikute 10M chini ya Godoro. Azing'oe popote kwa Ajili ya kusupoti Majengo ya kanisa nikakuta Tsh 200. Sikuelewa hapo Mungu alinifunisha nini.

Usicheke maana kama majini huwa yanawaambia wateja wao na wanakuta Pesa makaburini. Yesu ni zaidi.
Haa haa haa Mungu aliamua kukupa hiyo

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom