Nini kilimfanya Benjamin Mkapa ashindwe kuchapa Taazia ya muasisi wa TANU Abdul Sykes katika magazeti ya chama?

Washakufa wote hao
 
We mzee,
Baada ya kugundua hila ovu katika maandishi yako, nayapuuza. Huwa nakuja hapa kuwatahadharisha wasio tambua hila zako.

Hapo ulivyomuovu unasubiri kwa watu usiowapenda wafe uendelee na hila zako! Uombe mungu wako safari hii usife wewe kwanza!
 

Abdul alikutana na Nyerere akiwa amekaa Dar kitambo, na kwenye TANU alikuwa ameshafanya kazi muda mrefu. Wazee walivutiwa sana na jinsi mwalimu alikuwa na uwezo kujieleza na kujenga hoja. Pia kuweka mipango makini kwa ajili ya chama na mapambano ya kudai uhuru.


Ukweli utakuweka huru daima.
 
Hili huliwezi.

Kazi yangu, nimemaliza. Ila nimecheka sanna.

Nipo ....
 
Haya uliyo tuandikia tunayapata wapi kama ushahidi, ili nasisi tupate chu kuelezea hili huku tulipo.
 
Umemaliza. Mzee wngu Marehemu Sheikh Aman Thani alisema Ukweli Ni Huu...

Sent from my ANE-LX1 using JamiiForums mobile app
 

Anyway, haya makala yana politics zake. Ngoja nitafute pesa nimfadhili mwanafunzi makini aje na utafiti juu ya "The politics of freedom fighters: Who did what, by whose hand and resource, and for what outcomes"
 
Mzizi...
Baada ya uhuru zilipoanza kauli ya kukashifu TAA na yeye mwenyewe Abdul kuwa hakuwa anaongoza chama cha siasa mmoja wa marafiki zake aliyekuwa anaumizwa na maneno yale alikuwa Ahmed Rashad Ali.

(In Shaa Allah nitaweka historia ya Ahmed Rashad hapa kwa faida yetu sote).

Ahmed Rashad akawa anamuomba Abdul aeleze historia ya TANU kuanzia jinsi baba yake alivyoanza harakati kupitia African Association mwaka wa 1929.

Abdul Sykes alikataa akimwambia kuwa kama tatizo ni nani kaunda TANU yeye hilo halimshughulishi na hakika Abdul hakufungua kinywa chake hadi anaingia kaburini.

(In Shaa Allah nitakuwekeeni hapa yale aliyoandika Daisy kuhusu vipi baba yake alikabiliana ni fitna hii katika kipindi hiki).

Nilipokuwa nasafiri kuwatafuta hawa wazalendo ilikuwa tukimaliza mazungumzo nataka kunyanyuka kuondoka wananambia nisubiri tupige fatha, yaani tufanye dua.

Wakisema kuwa hili jambo nililokuwa nalifanya ni kubwa sana linahitaji msaada wa Allah.

Baadhi ya wazee hawa wengi walifariki kabla kitabu hakijatoka na wengine nilibahatika kuwapa nakala ya kitabu kwa mkono wangu ingawa kilikuwa kwa Kiingereza na wasingeweza kukisoma.

Moyoni walikuwa wanasononeka kuwa mchango wao katika kupigania uhuru haukuzaa matunda waliyotegemea.

Leo nafarajika ninaposoma jina la Abdul Sykes lililofutwa katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika lilivyorejea na sasa limekuwa maarufu watu wakibishana kuhusu yeye.

Kleist Sykes mtoto wa Abdul Sykes alikuja ofisini kwangu Tanga kunishukuru baada ya baba yake na baba yake mdogo Ally Sykes, kutunukiwa Medali ya Mwenge wa Uhuru kwa mchango wao katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Kleist alinipa mkono huku akibubujikwa na machozi.

Leo ninaposona lugha za "We mzee," lugha za dharau na kejeli na wakati mwingine vitisho sikasiriki.

Wale wazee waasisi wa TANU walinambia hii kazi niliyoamua kufanya ni nzito.

Hiyo picha ni siku watoto wa Abdul Sykes waliponiita nikaione Medali aliyotunukiwa baba yao (posthumous) katika kumbukumbu ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika.

Aliyevaa nguo nyekundu ni Daisy na kushoto wa kwanza ni Kleist.

 
Hili huliwezi.

Kazi yangu, nimemaliza. Ila nimecheka sanna.

Nipo ....


Lipi lisilowezekana??!; unashangaza kwelikweli!!!. Taazia au kitu kingine??

Kusoma na elimu hupatikana kwa unyenyekevu, "inna ilm minal llah".

Utakaa na kujigamba na kujitapa kwa kibri; inna kibri minak shaitwan.

Maam, Ukipingana na Qur'an basi wewe wampinga Mungu, mimi sikuwezi kwakuwa wampinga Mungu.
 
Hakuna mtu anayeumia na Historia, watu wanaumia na uongo
Unataka kusema nini !
Mag3 njoo huku kuna lingine.
Yaani huyo Mohamed Said asivyokuwa na aibu, hata sina muda wa kuzijibu upuuzi wake. Inaonekana ndivyo alivyolelewa, kuishi kwenye uongo. Uongo unaonekana umemnufaisha kwa kiwango kwamba bila uongo hawezi kumudu maisha.

Bahati mbaya anao wawezeshaji, ambao kwa makusudi wanameza hizi ngano zake za kutunga akiamini akizirudiarudia zitakuwa za kweli. Siku hizi nikiona mada yoyote humu imeanzishwa na huyo anayejiita Mohamed Said hata sisumbuki kuisoma...sina muda huo!
 
Nafikiri hata imani yake imejengwa kwa misingi ya uongo, kukaririshwa na kurudiarudia uongo amabao miaka mingi unakuja kuonekana ukweli. Imani imemuathiri karithi mbinu za uasisi wake!
 
Mkuu si kwamba nimekualika kuna jambo jipya, la hasha.
Nimekualika kwa 'new development''. Sina shaka unajua ngano marejeo uongo. Labda nikupe geni kidogo.

Nimefuatilia nyuzi zake baada ya kifo cha Mkapa nijue kuna lipi jipya katika ngano.

Ukisoma Tanzia utagundua tatizo si Mkapa, huyo ametumika tu kupumua (vent) chuki zake dhidi ya Nyerere.

Kaandika Mohamed ''... achilia mbali kwamba Abdul Sykes ndiye aliyempokea Nyerere Dar es Salaam''

Katika maandishi hayo kwa mtu asiyeweza kupambanua mambo au mgeni wa mada ni rahisi kuamini ujio wa Nyerere Dar ni matokeo ya kazi ngumu sana aliyofanya Abdul Sykes mwana wa Kleist Mbuwane.

Pascal Mayalla kamtembeza Mohamed jinsi na mara ngapi na kwanini Nyerere alikuja Dar, akishadidia hoja yangu kuwa mwaka 1948 katibu wa Tawi la TAA Tabora alikuja Dar, na ni wendawazimu kuamini hakuna mtu wa makao makuu akiwemo Sykes aliyemjua Julius Nyerere, mmoja wa wasomi wachache sana Tanganyika na katibu wa Tawi.

Mohamed akaja na majibu yafuatayo
1. Andikeni vitabu mueleze historia yenu. Of course tumemuelimisha kuwa hatuwezi kudurusu kazi za kisomi kwa kuandika vitabu, kama hilo linatokea duniani basi kila mwenye hoja lazima aandike kitabu!

2. Akasema watu wengi wanajua Abdul amempokea Nyerere.
Tumemjibu hayo ni majibu ya vijiweni, msomi hathubutu kuandika hivyo.
Ilimradi watu wengi wanasema basi kwake ni proof, tena akiwa ameandika vitabu!!

3. Akaja na hoja kuwa Prof Shivji na Prof Saida wameandika hivyo.
Tumemueleza kuwa kitabu chao cha wasifu wa Mwalimu kina mwaka tu.

Kuanzia 2010 Mohamed ameaminisha umma, leo anatumia kitabu miaka 9 baada ya kuhubiri uongo! Tukamwambia hata maprofesa tunawaalika hapa, ukweli utabaki kuwa hivyo!

4. Kilichonishtua na kukualika ni hoja kuwa, Abdul Sykes alimpokea Nyerere kutoka Pugu kuja mtaa wa Stanley Dar es Salaam. Kwamba, Pugu haikuwa sehemu ya Dar

Mohamed hana habari na East province , na kwamba barua kwenda St Francis zilikuwa na address ya Dar es Salam. Mohamed haelewi lini Dar es Slaam iliondolewa na kuwa cost region na Pugu kuwa kisarawe.

Sasa utetezi kama huu baada kushindwa kufinyanga uongo ni ushahidi wa wazi kwamba, mzee wetu anatengeneza majungu na kuayaita historia.

Haiwezekani Hisia zikawa sawa na historia na historia haindikwi kwa majungu.

Ukimsoma zaidi hana majibu, yeye anachotaka ni kupoteza mada na kuendelea kupotosha umma.

Kinachochagiza upotoshaji ni mahaba yasiyo na kifani kwa Abdul Sykes na chuki iliyotitia dhidi ya Nyerere.

Mkuu ni hayo tu, nikasema nikujulie hali mkubwa
 
Ila Nguruvi3 huyu mzee ana siri gani na Abdul Sykes? Sijawahi kuona akiandika kitu bila kumtaja Sykes.. inaboa mno.
Mohamed hawezi kuwaongelea wazee wake wenyewe bila kumtaja Abdul Sykes.
MS anaamini aliyeleta Uhuru wa Tanganyika ni Abdul Sykes na ndiye aliyepaswa kuwa Rais wa Tanganyika huru.

Mohamed hakubali ukweli kuwa aliyefanya 'transformation' ya siasa za barazani na kuzipa uelekeo ni Nyerere.
Tafuta mahali popote duniani uonionyeshe nyaraka kama muongozo au katiba ya chama aliyosimamia Abdul.

Hii haina maana wazee wa Dar es Salaam na Tanganyika hawakufanya jambo, la hasha. AA ilikuwepo 1929 Nyerere akiwa na miaka 7. Watu kama akina Cecil Matola wanapotezwa na jina la Kleist makusudi tu .

Kuna jitihada za kum 'overrate' Abdul Sykes ili kupitia yeye lijengwe Daraja kuelekea anakotaka

Chuki ya Mohamed kwa Nyerere ina mambo mengi ikiwemo dini, na hawezi kuijenga chuki hiyo ikatitia mioyoni mwa watu isipokuwa kupitia kwa jina la Abdul Sykes.

Kuna mengi tuachie hapo
 
Haswaa.
 
Hili huliwezi.
 
Udini mbaya sana ...sana sana..
 
Tena mtu wa ajabu sana huyu Pascal Mayalla

Na halafu ni namna hii hii ndivyo alivyomsababishia matatizo Eric.

Halafu Eric alipoachiwa akajifanya kumshukuru Mheshimiwa rais magufuli for that.

Huyu jamaa ni chatu na mdini haswa.
 
Nguruvi,
Ikiwa ni historia ya TANU lazima Abdul Sykes atajwe vinginevyo haitakuwa historia ya TANU.

Huwezi kueleza historia ya Azimio la Arusha bila ya kumtaja Nyerere.

Chuo Cha CCM Kivukoni wameandika historia ya TANU bila kumtaja Abdul Sykes.

Balaa lake ndiyo hili tuko hapa karibu miaka 10 tunamzungumza Abdul Sykes.

Abdul Sykes mwenyewe hakutaka kuwa rais na nimeeleza katika kitabu cha maisha yake jinsi alivyojitahidi kumshawishi Chief Kidaha Makwaia ajiunge na TAA wampe urais kisha waunde TANU na Chief Kidaha aongoze mapambano ya kudai uhuru.

Ungekuwa unafanya utafiti angalau kidogo kabla hujaandika.
 
Msikilize Mzee Waikela.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…