Nini kilimfanya Benjamin Mkapa ashindwe kuchapa Taazia ya muasisi wa TANU Abdul Sykes katika magazeti ya chama?



Umeandika mambo mengine yasiyohusika kusudi ama kukwepa mada au kuonyesha eti wewe ni mjuzi wa Kiswahili, juu ya yote, kilichopo mbele yetu ni; Neno "Taazia" (Taa'ziyah) ni neno la kiarabu au neno la kiswahili lenye asili ya kiarabu??.

Narudia tena Taazia ni neno la kiarabu haswa, maneno ya kiswahili yenye asili ya neno hilo na yenye maana hiyohiyo ya neno hilo ni maneno haya; Tanzia na Tazia-- hayo maneno mawili yanatambulika na wazungumzaji wa kiswahili na yamo katika kamusi za kiswahili na hakuna shida na shaka juu ya jambo hilo, Neno "Taazia" halitambuliki katika jamii za waswahili, vitabu, Magazeti na kamusi za kiswahili. Naam, wapo Waswahili wachache mno hupenda kulitumia kwa mapenzi yao katika nafasi ya Tazia au Tanzia na hawakatazwi kwakuwa wanaongea "kiswa- Arabic" jinsi watu wengine wanavyongea "kiswanglish" ila wanatakiwa watambue kuwa maneno sahihi ni hayo mawili ambayo yamesanifiwa.

Unauliza neno "Mauti" ni la kiarabu??--- jibu ni NDIYO. hapa ningependa kuelezea kidogo, neno hilo Mauti pia linatumika katika kiswahili na ndiyo maana limo katika kamusi za kiswahili, vitabu, magazetini nk, ni neno tulilokopa zimazima kutoka kiarabu na hiyo sio dhambi katika lugha kukopa neno zima, chukua mfano maneno ya kiarabu: بامية Bamia, صابون Sabuni, كتاب kitabu nk, katika kijerumani Schule (sshule) ndiyo Shule katika kiswahili nk,

Unapokuja hapa jikite kwenye mada, na sio ku "diverge" mada na kuanza kuleta mada ya vitenzi, vihisishi, visigishi, alomofu, mofimo, visawe, sarufi, ngeli, Nahau nk--🤣 hayo hayatasaidia.
 
Mokaze na Jurjani
Mjadala wenu mzuri, nimeupenda.
Nina kamusi ya kiswahili ya kuna hayo maneno Tanzia/Taazia na Mauti.

Nimewahi kusikia kwamba neno Taazia asili yake ni kiarabu na msingi wake ni neno Azza na moja ya maana
zake kati ya nyingi ni kusikitika, kuhuzunika.

Mimi si mtaalamu nimejaribu kuweka ili nipate msaada zaidi kutoka kwenu.
 
May Day , una maswali mazuri sana. Napenda nichangie kidogo kwa uchechefu
Historia inaonyesha 're-branding' ya AA kuwa TAA na TANU. AA ilianzishwa na akina Mwl. C.Matola na Kleist Sykes.
Ukimsoma Mohamed Said vizuri, AA ilikuwa 'Mali' ya Ukoo wa Sykes kama ambavyo TAA ilivyokuwa kwa Abdul

Kuna ushahidi wa maandishi wa Mohamed Said ukionyesha Abdul Sykes kuwatandika wazee wake katika kinyang'anyiro cha umiliki wa Chama kilichotoka kwa Baba yake na kutaka kupoteza kiti cha enzi.

Sasa kuanzia AA hadi TAA ambavyo vilikuwa chini ya Ukoo wa Sykes, hakuna maendeleo makubwa yaliyofikiwa.
Hapa haina maana chama hakikupiga hatua, la hasha, kulikuwa na uchovu wa kifikra

Ujio wa Nyerere ulifanya transformation kubwa sana ya chama na kuhuisha ''re-branding'' kuwa TANU

Kuvia kwa AA na TAA kulichangiwa na mambo mengi, kubwa likiwa ni weledi wa mwenendo wa dunia ya wakati huo

Kleist alipata 'mental block' ya kukibadilisha chama , na Abdul Sykes akapata mental fatigue
Haya ni mambo yanayotokana na uzito wa kazi hasa za siasa katika mazingira magumu na ufinyu wa elimu

Ndipo unaweza kuona, ujio wa Nyerere uliambatana na weledi hasa wa mambo ya dunia.
Nyerere aliafiki wazo la re-branding kutoka TAA kuwa TANU.

Kubwa lililobadilisha siasa za Tanganyika ilikuwa kuandika mwongozo wa chama kwa maana ya katiba.
Kuanzia 1929 hadi Abdul anashindwa uchaguzi chama kilikuwa hakina katiba.

May Day, muulize Mohamed Said akuonyesha katiba ya chama kabla ya ujio wa Nyerere! Hakuna, nada!

Kukosekana kwa muongozo ndicho chanzo cha mizozo na vurugu kama lile sakata la Abdul Sykes kuongoza genge la vijana na kwenda kuwatia adabu wazee. Yes , kwasababu zozote Abdul alikuwa sahihi, hakukuwepo mwongozo.

Jambo la pili kubwa alilofanya Nyerere ni kukihamisha chama kutoka Tandamti na kidongo chekundu na kukisambaza sehemu nyingine za nchi kwa kasi na nguvu kupitia mikutano.

Katika maandishi ya Historia, nguli wa tasnia Mohamed Said ameandika '' Nyerere alipokelewa na akina Sheikh Chembera , Sheikh Yusuf Bad na Masheikh wengine alipokwenda mikoa ya kusini''

Lakini pia bingwa huyo wa simulizi za hisia zenye mtazamo wa historia anabainisha jinsi Mwl Nyerere alivyopokelewa na akina Yusuf Ngozi na Selengia kanda ya kaskazini kama ilivyotokea kanda nyingine.

Kwa maneo hayo ya Sheikh Said Abdul Sykes hakuwahi kuzipeleka siasa nje ya mitaa maarufu ya Kariakoo.

Hili pia linadhahirishwa na maandishi ya Mbobezi Mohamed Said pale ambapo anaeleza kuwa ukiachilia safari ya kinyemela kule Ukerewe, hakuna mahali Abdul alikwenda kueneza chama nje ya viunga vya kariakoo.

Hapa tunafika mahali pagumu sana, kukiri kuwa ujio wa Nyerere ulibadili mwelekeo wa siasa za Tanganyika.

Kukubali hoja hiyo ni kufifisha na kudunisha sifa za Abdul Sykes, mtu ambaye kwa mintaaafu ya Mbobezi wa simulizi Mohamed Said yeye na Baba yake ndio walioleta jitihada za Tanganyika huru.

Ndipo tunaporudi kwenye nukuu maarufu aliyoukumbusha Sheikh Ramadhan Dau katika Taazia ya Mkapa, akisema '' If you want to kill a dog give it a bad name'', na Nyerere lazima apewe jina kwanza!

Ndipo unasikia haya '' Abdul.... ukiachilia mbali kumpokea Mwl Nyerere'' na kadha wa kadha ambayo hatuna haja ya kuyarejea. Inatosha kusema hatua za mwanzo ni 'kumpa jina baya ' na hilo limefanyika siku nyingi

Kama utakumbuka kuna wakati jina la Nyerere liliitikiwa kwa maneno ''laanatulah''.
Hizi zote ni jitihada za kumpa jina baya kwanza halafu ''kummaliza''

Kwa bahati mbaya au nzuri, historia haitungwi wala kufumwa. Historia inanukuliwa haiandikwi au kusadikishwa.

Historia ni mtiririko wa matukio kadri yalivyojidhihiri na si simulizi zenye Hisia au tenzi na ngano

Nyerere atabaki kuwa Nyerere na zama zake, na Abdul Sykes atabaki kuwa Abdul na zama zake.
 
Shukrani kwa msaada kaka,hili limeisha sasa.
 

Wenzako tunaandika Elimu wewe unaleta makisio.

Pili, sijakwepa mada, ndiyo maana huwa nakwambia una tatizo la kutokuwa makini, nimekupa kazi ya kutuwekea kitenzi cha tamko "Tanzia" ili uone kama neno la asili ni lipi, na je ni la Kiarabu au vipi ?

Tamko mauti si tamko la Kiarabu bali ni tamko lenye asili ya Kiarabu, sababu hili "Mauti" linasomeka kwa mujibu wa Waswahili kwahiyo haliingii tena kwenye kanuni za lugha ya Kiarabu.

Hakuna tamko la Kiarabu linalo andikwa "Taazia", tuwekee tamko hilo, kijana unauelewa mdogo sana. Unatakiwa usome.

Kijana hili nilikwambia tangu awali kwamba huliwezi, na huliwezi kweli. Unavyoendelea kujitutumua ndiyo unazidi kuonyesha ujinga wako.

Hili limeisha.
 
Maelezo mazuri sana, Kuna mdau aliwahi kuandika humu kuna tofauti kati ya historia na histohisia.

Hivyo ni vyema kuwa makini na hayo maneno hasa tunapoangalia historia ya Uhuru wa Tanganyika na mchango wa hawa wazalendo wawili (Abdul na Nyerere).
 
Mkuu maandishi yako hayana jipya.
Bado umeegemea Maandishi ya Mohamed Said
Ulichofanya ni kukopi na kuweka ufafanuzi wa makisio yako.
Maandishi yake yamesaidia wengi kuanzia wale
wanaomkubali na wanaompinga.

Kabla ya kitabu chake taarifa za harakati za Uhuru wa Tanganyika
zilimtambua Nyerere peke yake. Lakini sasa wanatajwa Kina Abdul Sykes,
na wazee wengi ambao kabla ya kitabu cha Mohamed Said hawakutajwa kamwe.

Tuendelee kumpinga lakini tukubali kitabu chake kimebadilisha sana
dhana ya harakati za Uhuru wa Tanganyika. Kwa hili amesaidia sana
kuweka ukweli ambao hatukuujua hapo mwanzoni.

Tumshukuru Mohamed Said ameweka alama katika historia ya nchi
ambayo haitafutika kama ambavyo wengine wanavyofanya jitihada ya kupotosha.

Kinachofurahisha hata wanaompinga sasa wanalazimika kuwataja kina Sykes na wengine
ambapo hapo awali hawakutajwa kabisa, japo kwa kuongezea na chumvi zao.

Kingine kwamba wakati kitabu chake kilipozinduliwa Nyerere bado alikuwa hai
na alipelekewa kitabu akisome.

 
Nguruvi...
Ukiondoa lugha kali umeleta hoja nzuri ambazo mimi nimeshazieleza kwingi.

Abdul alifikia mahali hakuweza kusogea mbele khasa pale aliposhindwa kumshawishi Chief Kidaha Makwaia kujiunga na TAA waunde TANU.

Hili la katiba huwa kila nikisoma si kwako tu hata katika Wasifu wa Julius Nyerere hujiambia Mwingereza atapitisha katiba gani ya maana kwa chama cha Waafrika.

Wengi hawajui kuwa hata hiyo TANU katiba yake ilinakiliwa kutoka katiba ya Convention People's Party (CPP)ya Kwame Nkrumah...Earle Seaton huyo.

Na hii katiba si kama ilimsubiri Nyerere afike ndiyo itafutwe.

Lakini kinachonifariji ni kuwa Abdul Sykes aliyefutwa katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika leo karudi anazungumzwa.

Muhimu ni ukweli kuwa Nyerere alipopanda jukwaani hali ya siasa Tanganyika ilibadilika.

Siku zote nasikitika kwa mimi kutopewa shajara za Abdul Sykes kuzisoma.

Naamini ndani ya shajara zile kuna mengi.
 


Hicho ndicho kilichohitajika kutoka kwa huyo ndugu, sio maneno tu, shukrani.
 
Kleist Abdallah Sykes, Muasisi wa Harakati na Mtu wa Fikra: 1894 - 1949

Historia ya ukoo wa akina Sykes inarudi nyuma kiasa cha zaidi ya miaka mia moja hivi.

Katika miaka hiyo yote ukoo huu umeweza kuhifadhi historia yake kupitia kwa Kleist Sykes mwenyewe ambae yeye alijifunza historia ya kabila lao kutoka kwa mlezi wake, Affande Plantan.

Katika kutaka kupata koloni la Kijerumani katika Afrika ya Mashariki huku wakikabiliwa na upinzani kutoka kwa Waarabu katika pwani, pamoja na upinzani kutoka kwa machifu wa huko bara, Chancellor Otto von Bismarck alimchagua Harmine von Wissman akakomeshe upinzani dhidi ya Ujerumani na kuweka amri moja.

Affande Plantan alikuwa chief wa Kizulu katika kijiji cha Kwa Likunyi Inhambane, Mozambique ambae Herman von Wissman aliwekanae mkataba wa kujanae Tanganyika na kikosi cha askari mamluki wa Kizulu kuja kuwasaidia Wajerumani katika vita vyao na Mtwa Mkwawa na Bushiri bin Salim Al Harith.

Katika jeshi hili alikuwamo Sykes Mbuwane baba yake Kleist ambae alifariki dunia mwaka wa 1894 wakati anarudi vitani baada ya kumshinda Chief Mkwawa na huu ndiyo mwaka aliozaliwa Kleist.

Kleist akawa ndiyo mtu wa kwanza katika ukoo huo kuandika historia hii kabla hajafariki akiacha historia hiyo kama mswada na ukieleza yote aliyoyatenda katika uwanja wa siasa kuanzia kuasisi African Association mwaka wa 1929 na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika mwaka wa 1933.

Mswada huu wa Kleist ukachapwa kama sura ya kitabu kilichohaririwa na John Iliffe mwaka wa 1973 baada ya kuchapwa kama ‘’seminar paper,’’ Chuo Kikuu Cha Afrika ya Mashariki Idara ya Historia iliyoandikwa na mjukuu wake Aisha ‘’Daisy’’ Sykes, mwaka wa 1968.

Wajerumani walihisi kuwa ikiwa Wazulu walikuwa wamewasimamisha Wareno katika vita wakashindwa kupata ushindi kwa urahisi watu wa Tanganyika hawataweza kufua dafu mbele ya mbinu za Wazulu za vita.

Hii ilikuwa mwaka wa 1894.

Baada ya kuwashinda wananchi wa Tanganyika, Wissman alitunzwa na serikali yake na akafanywa Gavana wa German East Africa kati ya mwaka wa 1895 na 1896.

Wazulu nao kwa kuwa walichangia katika ushindi huo na wao hawakutoka mikono mitupu, Wajerumani waliwatunza.

Kleist alipelekwa kusoma shule ya Wajerumani akajifunza Kijerumani, kupiga chapa na hati mkato, ujuzi adimu na wa thamani sana kwa Mwafrika enzi zile.

Katika nyumba ya Affande Plantan, Kleist alilelewa pamoja na watoto wa Affande Plantan mwenyewe, Schneider Abdillah, Ramadhani Mashado Plantan na Thomas Sauti Plantan mtoto wa ndugu yake wa mbali kidogo.

Watoto hawa wote walipata elimu nzuri ambayo iliwawezesha kuwa watu muhimu katika mji wa Dar es Salaam.

Baada ya kumaliza shule Kleist na Schneider waliingizwa katika jeshi la Wajerumani na wakapigana Vita Kuu ya Kwanza wakiwa askari chini ya Von Lettow Vorbeck.

Katika mswada wa maisha yake Kleist ameandika kitu mfano wa Shajara ya Vita (War Diary).

Shajara hii itamsaidia mtafiti yeyote kujua vita vilikwendaje baina ya Wajerumani na Waingereza pale vita vilipoanza kwa Waingereza kuvuka mpaka kuingia Tanganyika wakitokea Kenya na kukutana na batalioni aliyokuwamo Kleist na Schneider ikitokea Dar es Salaam.

Vikosi hivi viwili vilikutana Mwakinyumbi Tanga ambako Waarabu walingia pia vitani upande wa Waingereza kulipa kisasi cha kuuawa Abushiri.

Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ndipo Kleist akaanza kujihusisha na harakati za Waafrika akiwa muasisi wa African Assocaition mwaka wa 1929 kama katibu kisha akaasisi Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika akiwa katibu muasisi vile vile.

Akiwa Katibu wa African Association akaweza kujenga ofisi ya chama Mtaa wa New Street na Kariakoo kati ya mwaka wa 1929 na mwaka wa 1933.

Mwaka wa 1933 akiwa Katibu wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika akaweza kujenga shule kwa ajili ya watoto wa Kiislam, shule ambayo ilikuwa ikisomesha masomo ya Kisekula pamoja na masomo ya kuujua Uislam.

Kleist akawa mfanyabiashara mkubwa katika jamii ya Waafrika wa Tanganyika na kama mjumbe wa Kamati ya Maulidi na kiongozi wa Waafrika waliokuwa waajiriwa wa Tanganyika Railwways nafasi hizi zilimpa sauti kubwa katika siasa za Dar es Salaam.

Nafasi hizi alizokuwa ameshika na muunganiko viongozi wa African Association na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika ndiyo uliojenga nguvu kubwa ya Waislam ndani ya TANU kiasi cha kuifanya TANU kuchukua sura ya chama cha Waislam.

Mashado Plantan aliajiriwa kama askari akiwa na cheo kilichomtabulisha kama askari anaezungumza Kiingereza na baadae alikuja kuwa mhariri wa magazeti aliyoyamiliki mwenyewe.

Gazeti lake la kwanza likiitwa, ‘’Dunia,’’ na wakati wa Vita Vya Pili Vya Dunia akaanzisha gazeti lililoitwa ‘’Zuhra.’’

Gazeti la Zuhra lilichapa habari muhimu katika jamii ya Waafrika.

Thomas Saudtz alikuja kuwa mwalimu wa shule Mpwapwa na Dar es Salaam na Schneider Abdillah Plantan alikuwa mwanachama shupavu wa TAA na aliungana na Sheikh Hassan bin Amir kama katibu wa Daawat Islamiyya fi Tanganyika (Mwito kwa Waislam) Mwenyekiti akiwa Sheikh Hassan bin Ameir mwenyewe.

Kleist aliwashinda ndugu zake wote.

Alikuwa mtu wa fikra na akaweza kuasisi taasisi nyingi na akaacha nyaraka za picha ambazo ndizo zilizokuja baada ya miaka mingi kupita kusaidia watafiti wa historia ya Tangayika kuijua historia ya African Association kwa ukamilifu wake.

Jina la Kleist likahusishwa na harakati za watu wa Tanganyika katika kupinga dhulma ya ukoloni,

Ikumbukwe kuwa Kleist alikuwa kutoka katika kizazi cha pili katika Tanganyika kutumika katika majeshi kama askari kwanza wazee wake waliomtangulia wakiwa katika jeshi la Wajerumani lililovamia Tanganyika chini ya Herman von Wissman kisha yeye akiwa sehemu ya jeshi la Wajerumani akalitumikia jeshi hilo kupigana na Waingereza chini ya Paul Von Lettow Vorbeck.

Tutaangalia kwanza vipi msingi huu alioacha Kleist Sykes ulivyowafanya Waislam na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika kuwa sehemu ya chama cha TAA na kwa ajili hii kuwa sehemu ya nguvu ya kupambana na ukoloni wa Waingereza chini ya chama cha TANU kikiongozwa na Julius Nyerere.

Pili tutaangalia vipi wanae Kleist, Abdulwahid na Ally kwa kushughulika katika harakati za kupinga ukoloni na wao pia wakawa na kumbukumbu, nyaraka na picha nyingi ambazo zimesaidia sana katika kuhifadhi historia ya uhuru wa Tanganyika kati ya mwaka 1945 hadi 1961 uhuru ulipopatikana.

Bwana Nguruvi,
Unae mtu yeyote hata Nyerere mwenyewe ambae ana historia kama hii?
Hapa sizungumzii kuhusu vielelezo vya nyaraka na mapicha.
 
Nguruvi3 nimekubari uchambuzi wako.👏
 

Unae mtu yeyote hata Nyerere mwenyewe ambae ana historia kama hii?

Mzee Said sidhani kama hapa kuna jipya uliloleta zaidi ya kuhadithia histori mbayo ipo tu na ingehadithiwa au kusomwa wakati wowote.

Na hii ndio imekuwa mbinu yako ya kutumia kalamu au nukuu kutaka kupenyeza ajenda zako, na hapa ndipo haswa kunapoleta upinzani kwa kazi zako.

Alichokifanya Kleist sio cha ajabu sana kwani karibu kila jamii ilifanya harakati zake kupambana na ukoloni pamoja na kuanzisha vyama...nimewahi kukuwekea hapa jukwaani mfano wa harakati za chama cha ushirika kule Upare kilichokuwa pia kinakabiliana na uonevu wa Wakoloni...kulikuwa na vyama Uchagani, Meru sambamba na harakati ambazo zote zina Waanzilishi na historia zao.

Hata Dar kulikuwepo na vyama vingine tofauti na AA, TAA n.k. na haswa sababu ya kuwajadili kina Sykes ni kwa sababu Mwalimu alijiunga na TAA, hali ingekuwa tofauti kama Mwalimu angejiunga na Chama/Wanaharakati wengine.

Labda tofauti iwe kwamba Kleist alikuwa anaandika mapito yake huku kwa wengine waliwekeza zaidi kwenye vitendo na hawakujali kuweka kumbukumbu za kimaandishi.

Wajerumani walihisi kuwa ikiwa Wazulu walikuwa wamewasimamisha Wareno katika vita wakashindwa kupata ushindi kwa urahisi watu wa Tanganyika hawataweza kufua dafu mbele ya mbinu za Wazulu za vita.
Hii ilikuwa mwaka wa 1894.


Sanasana kipya nilichokipata hapa ni kuunganisha dots kwa hili la Askari wa Kizulu na kile kilichotokea Mkoani Kilimanjaro...na ndio unatuambia kuwa Ndugu zako hao walibebwa kuja kuwauwa Babu zetu huku.

Mangi Meli fought two wars with the Germans, in the first war of June 1892 fighting for 2 days he defeated them include murdering a german governor and military leader in Kilimanjaro Von Bulow and expel them completely from Kilimanjaro, they returned after 1 year and 2 months in August of 1893 with mercenery Nubi souldiers from Sudan and other Zulu soldiers from South Africa with more advanced machine guns and fought him the second war which also took two days and defeated him.

Mangi Meli alipigana vita mbili na Wajerumani, vita ya kwanza ilikuwa Mwezi wa sita mwaka 1892, vita vilipiganwa kwa siku mbili na kuwashinda, walimuua Gavana na Kiongozi wa Askari wa Kijerumani Von Bulow na hivyo kufanikiwa kuwafukuza Wajerumani kutoka Kilimanjaro.
Wajerumani walirudi baada ya mwaka mmoja na miezi miwili, Mwezi wa nane mwaka 1893 wakiwa na Askari Mamluki(mercenaries) Wanubi kutoka Sudan na Wazulu kutoka Africa ya Kusini, sambamba na silaha zaidi na za kisasa. Wakati huu Wajerumani walimshinda Mangi Meli.

Mzee Said uwe unajibu hoja zinazoletwa na si kuleta mada mpya tofauti kabisa na mjadala uliopo.
 
Nimeona hapo juu unahoji ni kwa vipi Mwalimu alisema alikuta mambo yamesinzia...hivi kweli Mzee Said unataka kulinganisha mtazamo wako na wa Mwalimu?..huenda kile unachoona wewe kinaenda sawa sivyo atakavyoona Mwalimu.

Na hebu sema ukweli ni tofauti gani ilitokea baada ya Mwalimu kujiunga na TAA?.

Nani alikuwa Mtu maarufu zaidi Dar na nje ya Dar ndani ya muda mfupi kati ya kina Sykes na Mwalimu ingawa huwa unasisitiza kuwa wao ndio walikuwa wanamtambulisha Mwalimu.

Je mikoani waliwafahamu kina Sykes au Mwalimu?.
 
May Day,
Ikiwa unataka mimi nifanye mjadala kwa namna utakavyo wewe utanipa shida.
Moja ya namna yangu ya mjadala ni kukwepa ubishi kwani ubishi hauongezi elimu wala kusomesha.

Nimefurahi sana umeniwekea historia ya Wachagga.

Hivi sasa naandika kitabu cha Rajab Ibrahim Kirama (1843 -1962) naamini hili jina hujapata kulisikia katika historia ya Wachagga.

Huyu ndiye aliyeingiaza Uislam Uchaggani na historia ya ukoo huu wake wa Njau kama Majemadari wa Vita inarudi nyuma miaka 300 na imehifadhiwa kwa kumbukumbu za kichwa na kwa ushahidi wa nyaraka zinazokwenda nyuma kiasi cha miaka 100.

Sasa kwa kuwa unasema sina jipya naona nikupe kitu kipya na ni katika haya haya tunayojadili hapa.

Nakuunga mkono katika historia ya Mangi Meli na nakuonyesha kitu kutoka kitabu ninachoandika.
Nimempa Mangi Meli jina kwa utanashati wake na jinsi alivyojaliwa sura jamili.

Nimempa jina ''Handsome Boy.''

Hivi nahangaika kutafuta jina kama hili kwa Kichagga.

Karibu:

''Mwaka wa 1890 Herman von Wissman baada ya kumaliza vita na Abushiri na kumnyonga alielekeza jeshi lake kaskazini na akamshambulia Mangi Sina katika vita vikali ambavyo jeshi la Sina lilionyesha uhodari mkubwa wa mapambano.

Vita hivi vilinyanyua haiba ya Sina na Wajerumani wakanyoosha mkono wa urafiki na huo ndiyo ukawa mwisho wa uhasama baina ya Mangi Sina na Wajerumani.

Juu ya haya Rindi aliungana na Hermann von Wissman dhidi ya Sina na na hii ikapelekea kwa Sina kushindwa vita mwaka wa 1891.

Fitna na usaliti ukawa sasa ni moja ya silaha zilizowapa Wajerumani ushindi.

Sina alifariki mwaka wa 1899 akiwa kaacha sifa ya ushujaa wa vita mbele ya Wajerumani kwani peke yao hawakuweza kumshinda hadi ulipopitika usaliti dhidi yake.

Kunyongwa kwa Mangi Meli Old Moshi mwaka wa 1900 pengine yeye Muro Mboyo akiwa shahidi wa mauaji yale ulikuwa ujumbe tosha kuwa nyakati zimebadika.

Meli kama ilivyokuwa kwa Abushiri na yeye alisalitiwa pia na wale aliokuwa akiwapigania.

Kadhalika kama ilivyokuwa kwa Abushiri kuwa adui wa kweli hakuwa Mjerumani peke yake bali pia nduguze katika ukanda wote wa pwani ambao walikuwa tayari kujiuza kwa Wajerumani.

Haikuwa tabu sana pia kwa baadhi ya watawala wa Uchagani kutambua kuwa adui wa kweli pia hakuwa mtawala jirani yake aliye Kibosho au Machame chini ya Mlima Kilimanjaro bali Mjerumani kutoka mbali.

Hali hii ilikuwa na manufaa makubwa kwa Wajerumani.

Lakini usaliti huu haukuwa uko katika siasa za Wachagga peke yao kwa watawala kufitiana na kusalitiana.

Wajerunani na wao waliucheza mchezo huu kwa mafanikio makubwa kwa kuwaghilibu askari wa Kinubi kutoka Sudan na Wazulu waliowachukua kutoka kijiji kinachojulikana kama Kwa Likunyi, Imhambane Mozambique.

Wissmann alipofika katika kijiji hiki alifanya mazungunguzo na Chifu Shangaan kiongozi wa Wazulu waliokimbia vita vya Chaka na kuingia Mozambique kutafuta hifadhi.

Mkataba alioweka Wissmann na Chifu Shangaan ambae baada ya kufika Tanganyika akajulikana kwa jina la Affande Plantan ilikuwa baada ya kushinda vita Wajerumani na Wazulu wataitawala Tanganyika kwa pamoja.

Jeshi hili la mamluki chini ya Wissmann walipigana dhidi ya Waafrika wenzao kwa tamaa kuwa na wao watakuja kuwa watawala kama Wajerumani baada ya ushindi.

Lakini baada ya Ujermani kushinda vita vyake na kuanza kutawala kwa utulivu hawakutimiza ahadi waliyoweka ingawa walirejesha hisani kwa kuunda jeshi waliloliita Germany Constabulary na mkuu wa jeshi hili alikuwa Affande Plantan.

Hili jeshi liliwekwa ndani ya kambi Dar es Salaam hadi mwaka wa 1918 baada ya Ujerumani kushindwa katika Vita Vya Kwanza Vya Dunia huu ndiyo ukawa mwisho wa jeshi hili Tanganyika.

Wakati wa utawala wao Wajerumani walijenga shule na wakawasomesha watoto wa hawa askari kwa kiwango ambacho watoto wa raia wa kawaida hawakukipata na baada ya kumaliza shule darasa la sita walitoka shule wakiwa wanakisema Kijerumani vizuri na wakiwa na ujuzi mbalimbali na wengi wao waliingizwa jeshini kama askari katika Germany Constabulary.''

(Shule hizi za Wajerumani iliyojengwa Dar es Salaam na shule nyingine zilizojengwa kwengineko huko bara na wamishionari ndizo zilizokuja kuwatoa Waafrika ambao waliacha alama katika historia ya Tanganyika watu kama Joseph Merinyo, Paul Njau kutoka Kilimanjaro, Kleist Sykes, Schneider Plantan, Mashado Plantan kutoka Dar es Salaam, Martin Kayamba kutoka Tanga na wengine wengi ambao walikuja kuutumikia utawala wa Mfalme George wakati wa utawala wa Waingereza na ghilba waliyofanyiwa baba zao na Wissmann ni sehemu ya historia ya wazazi wao.

Hii leo haya ni sehemu ya simuliza katika historia ya Tanganyika vipi wazee wao walifika Tanganyika zaidi ya miaka 100 iliyopita na kuwa sehemu ya utawala wa kikoloni na pia baadae kuwa sehemu ya msingi ya kudai uhuru wa Tanganyika).

Tanbihi: Muro Mboyo ndiye baba yake Rajab Ibrahim Kirama.

 
May Day,
Ilikuwa baada ya TANU kuundwa na Nyerere kupanda jukwaani sasa ndipo TANU ikajulikana kote Tanganyika na Nyerere akawa ndiyo kiongozi wa harakati za kudai uhuru wa Tanganyika.

Haya nani maarufu nani hajulikani sidhani kama yana maana sana.

Lakini haya yote na jinsi Mwalimu alivyopokelewa na watu kama Sheikh Hassan bin Ameir yamo katika kitabu cha Abdul Sykes ingefaa ukisome.
 
Hadithi za kale hizi hazina maana yoyote.

Watu wanahitaji maji safi, makazi bora, chakula, ajira, elimu safi, miundombinu na huduma zote muhimu!

Mambo ya Tanu sijui abdul sykes yananisaidia nini mimi?
 
Anataka mababu zake akina Skyes wapewe utakatifu katika Historia ya Tanzania kwa sababu bila wao Nyerere angekuwa homeless alipofika Dar [emoji16][emoji16][emoji16]
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]
We jamaa sijui huwa unawazaga nini ndani ya mukichwa yako..
You're very funny.... [emoji4]
 
[emoji3]
 
Umeingia katika mjadala kati kati. soma kuanzia mwanzo utaelewa tunazungumzia nini

Halafu elewa hoja imekuwepo lini na Maprofesa wameandika lini.

Nadhani utulie kidogo ujifunze, hapa ni pakubwa kwa kimo.

Ahsante
[emoji3]
 
Mkataba alioweka Wissmann na Chifu Shangaan ambae baada ya kufika Tanganyika akajulikana kwa jina la Affande Plantan ilikuwa baada ya kushinda vita Wajerumani na Wazulu wataitawala Tanganyika kwa pamoja.
Hili la Mangi sina kusalitiwa na Rindi nalifahamu.

Pointi haswa niliyotaka ichukuliwe ni kuwa ni vizuri kuisikia hiyo historia ya Kleist lakini sio kwamba alifanya jambo ambalo halikufanywa na Wengine....harakati zilikuwepo karibu kwenye kila jamii ila sio jamii zote zilifanikiwa kuhifadhi kumbukumbu kimaandishi hivyo huenda zimepotea.

Kuna pia yule Mama wa Singida, ingawa habari zake wanazihusisha na mambo ya kusadikika nisiyoyaamini..ila cha msingi kulikuwa na upinzani na kulikuwa na wanaoratibu.

Kingine ni kupitia kukumbuka na kufahamu kupitia andiko kuwa kina Sykes ni Mamluki waliokuja kuzidhulumu roho za Babu zetu kwa tamaa labda ya pesa, madaraka, ardhi au mali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…