Nini kilimfanya Benjamin Mkapa ashindwe kuchapa Taazia ya muasisi wa TANU Abdul Sykes katika magazeti ya chama?

Nini kilimfanya Benjamin Mkapa ashindwe kuchapa Taazia ya muasisi wa TANU Abdul Sykes katika magazeti ya chama?

Wakuu kina Pascall ,Nguruvi na wengine, ni kweli Mzee amekuwa "kichwa ngumu" kwa kurudia mara kwa mara hizi mada zake licha ya kwamba baadhi ya Watu wamekuwa wakimpinga na kumuhoji maswali ambayo huwa anakwepa.

Juzi hapa amekuja na uzi wa kumsema Gwajima, na kuna Mdau katika kujibu moja ya komenti yangu kwenye uzi ule alisema ingawa Gwajima ni kiongozi tu wa kikundi hapo Dar lakini anayoongea yasipuuzwe kwani huenda yakafika mbali...ni vivyo hivyo nionavyo kwa hizi nyuzi za Mzee Said.

Hivyo basi wenye nafasi na ufahamu wa mambo haya wawe wakitoa uafafanuzi wa yanayopotoshwa na Mzee Said kila pale mnapopata nafasi badala ya kumuachia tu ajinafasi na nyuzi zake....maana huenda ni wengi wanapita humu JF, na wengine huenda ndio kwanza wanakutana na uzi wake, wataishia kula matango pori kutoka kwa Mzee wetu huyu.
 
Miongoni mwa sifa za wasomi
1. Kukubali 'criticism '
2. Kutetea kazi zao kwa hoja.
Ni msomi gani aanayetetea ''thesis'' kwa kuwaambia wenzake waandike vitabu vyao?
Kumbe basi kwa miaka 10 hapa jamvini umeanisha watu kitu ulichokuwa huna ushahidi nacho hadi Prof Shivji na Saida walipoandika mwaka jana tu. Kitabu chako kina miaka zaidi ya 20
Yaani unasubiri kutetewa na si wewe kutetea kazi zako. Tulisema unaandika uongo! unaona sana

Prof Shivji na Prof Said hawa ni wasomi na tunawatumia salamu zetu kutoka JF kwamba, Abdul hakumpokea Nyerere Dar es Slaam. Nyerere alikuwa mkazi wa Dar na alifika kuanzia mwaka 1948. Tunao ushahidi wa kutosha.
Nyerere aliishi na Abdul Sykes baada ya kuacha kazi akitokea Pugu si Butiama au kwingine
.Hapana usiondoke kwenye hoja. Kwanza tukubaliane kuwa Abdul Sykes hakuwahi kumpokea Nyerere Dar es Slaam. Na kwamba, Nyerere aliishi kwa Abdul Sykes baada ya kuacha kazi Pugu.
Kwamba Nyerere alifika Dar es Slaam tangu mwaka 1948 na kwa nayakati mabali mbali kama Pascal Mayalla alivyodadavua kwa kina.

Wapi nimedai kuwa Nyerere hajaishi kwa Abdul. Tafadhali onyesha . Hizi ndizo njia za muongo, kutafuta mahali pa kutokea.
Nimeeleza kila mahali kuwa Nyerere aliishi kwa Abdul baada ya kuacha kazi. Pascal Mayalla kaeleza na tumesema wazi hilo halipingiki.
Tunachokueleza hapa ni kuwa Nyerere hakupokelewa na Abdul.
Nina uhakika unajua tofauti ya kuishi na mtu na kumpokea. Kama hilo hujui sina njia yakukusaidia

Kwa lugha ya stara hili tunaliita ''anachronism''. Kwa lugha isiyopendeza ni nonsense

Hatukukuuliza haya, hoja ilikuwa ni moja. Nyerere hakupokelewa Dar es Salaam na Abdul Sykes.
Huu ni ukweli ulioshindwa kuutetea ingawa unauzungumza. Unafanya hivyo ukijua kuwa uongo unaourudia kila mara sasa unageuka kuwa ukweli.

Mpelekea salam Prof Shivji na Prof Saida , kwamba, kama wanaweza waje hapa tuongee nao na kuwathibitishia kuwa Nyerere hakupokelewa na Abdul Sykes Dar es Salaam hata siku moja.
Kilichotokea ni Nyerere kuishi kwa Abdul Sykes baada ya kauacha kazi Pugu.

Hayo maneno yoote hayana maana katika mjadala, yamekusudia kufunika aibu ya uongo ambao huwezi kuutetea bali kujificha ficha nyuma ya maandishi mengi yasiyoulizwa wala yasiyojibu hoja.

Wanajamvi, nadhani mnaouona UONGO wa Mohamed Said kwa macho yenu.

Hapa lengo lake ni moja, 'kumpa Nyerere jina baya'' kama majina mabaya ya mbwa ili kujenga ''uhalali wa kumuua''

Hiyo hadithi ya Daisy imelenga kuonyesha Nyerere alikula mayai kwa Abdul Sykes.
Huyu bwana Mohammed said janja janja sn.... Anajaribu kutumia janja yake kuondoa watu kwenye mjadala wa msingi baada ya kuona hauna mashiko.... lkn anachemka vibaya......
 
Sir...
Nakusoma naihisi hamaki katika jambo lisilo hamakisha:

HISTORIA YA ALI MSHAM NA JULIUS NYERERE 1955

Kuna picha ya Mtaa wa Jaribu Magomeni iliyowekewa maelezo kuwa ni Mtaa wa Congo.

Picha hii imekuwa ikizunguka sana mitandaoni.

Picha iko hapo chini.

Huu si Mtaa wa Congo wala si mwaka wa 1920.

Huu ni Mtaa wa Jaribu Magomeni Mapipa miaka ya katikati 1950s na hapo ni nyumbani kwa Ali Msham aliyehamia Dar es Salaam kutokea Kilwa, aliyefungua tawi la TANU nyumbani kwake mwaka wa 1954 kupigania uhuru wa Tanganyika.

Picha hii ilipigwa siku chache Februari, 1955 kabla Mwalimu Nyerere hajakwenda UNO na siku hiyo Ali Msham na wanachama wa TANU walikusanyika hapo kufanya kisomo na dua kumwomba Allah ajaalie safari njema yenye mafanikio kwa lile walilokuwa wanalipigania.

Ali Msham alikuwa fundi seremala na akifanya shughuli zake Mtaa wa Kariakoo na Kibambawe.

Mimi naishi jirani na hii nyumba.

Watoto wa marehemu Ali Msham ni jirani zangu hapa Magomeni Mapipa na walisikia siku moja nafanya kipindi Radio Kheri kuhusu TANU ndipo waliponiletea picha na wakanieleza historia ya baba yao Ali Msham na Mwalimu Nyerere wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Baba yao marehemu Ali Msham alifungua tawi la TANU nyumbani kwake na tawi hili lilikuwa na wanachama wengi hasa wanawake.

Mwalimu Nyerere alipohamia Magomeni mwaka wa 1955 Ali Msham alimfungulia Mama Maria kijiduka kidogo hapo kwake cha kuuza mafuta ya taa.

Mama Maria alikuwa pia akiwa dukani kwake akifuma sweta.

Siku moja Ali Msham alikwenda ofisini kwa Mwalimu Nyerere pale New Street akakuta samani alizokuwa akitumia Mwalimu ni duni sana.

Ali Msham alisikitishwa na hali ile.

Ali Msham alitengeneza samani mpya kiwandani kwake na akanunua na saa ya ukutani kwa ajili ya ofisi ya Rais wa TANU na akamuomba Mwalimu Nyerere wamkabidhi samani zile kwenye tawi lake la TANU Magomeni Mapipa Mtaa wa Jaribu katika sherehe maalum.

Angalia picha hapo chini Ali Msham ni wa kwanza kulia na Mwalimu Nyerere amekaa kwenye meza.

Picha ya sherehe hii na nyingine za harakati za baba yao katika TANU watoto wa Ali Msham wamezihifadhi kuanzia mwaka wa 1955 hadi leo.

Nilichofanya mimi niliaandika historia ya Ali Msham na nikaiweka katika blog yangu mohamedsaidsalum.blogspot.com pamoja na picha zile.
Ila Mohamed sasa naona unaleta story za kwenye vijiwe vya kahawa magomeni.... 😂😂

Mwalimu Nyerere alipohamia Magomeni mwaka wa 1955 Ali Msham alimfungulia Mama Maria kijiduka kidogo hapo kwake cha kuuza mafuta ya taa.

Mama Maria alikuwa pia akiwa dukani kwake akifuma sweta.

Siku moja Ali Msham alikwenda ofisini kwa Mwalimu Nyerere pale New Street akakuta samani alizokuwa akitumia Mwalimu ni duni sana.
 
Ila Mohamed sasa naona unaleta story za kwenye vijiwe vya kahawa magomeni.... [emoji23][emoji23]

Mwalimu Nyerere alipohamia Magomeni mwaka wa 1955 Ali Msham alimfungulia Mama Maria kijiduka kidogo hapo kwake cha kuuza mafuta ya taa.

Mama Maria alikuwa pia akiwa dukani kwake akifuma sweta.

Siku moja Ali Msham alikwenda ofisini kwa Mwalimu Nyerere pale New Street akakuta samani alizokuwa akitumia Mwalimu ni duni sana.
Jile...
Ikiwa huamini mimi sikulazimishi uniamini lakini hii ndiyo historia ya TANU na tawi la TANU la nyumbani kwa Ali Mshamu Magomeni Mapipa ni moja katika matawi ya mwanzo Dar es Salaam.

Nitaweka hapa picha za tawi hilo In Shaa Allah.
 
Kama ambavyo Mzee Said amekuwa anarudi jukwaani na nyuzi zake potofu...basi na mimi nitajaribu kurudia yale yale ninayoyafahamu juu ya mambo kadhaa...ni dhahiri kuwa kila Mtu anayesoma nyuzi za Mzee atakuwa anashtuka kuwa Mzee kuna ajenda anayojaribu kuisukuma kwa bidii bila hata kujali kama anapotosha ama la.

Kwa mfano hili la kusema Abdul ndiye muasisi wa TANU halina ukweli wowote maana TANU ilianzishwa kama "transformation" ya chama kilichokuwepo cha TAA, na alichofanya Abdul na Wenzake ni kupendekeza jina ambalo lilipitishwa na Wahusika kati ya majina kadhaa yaliyopendekezwa.TAA ilibadilishwa kuwa TANU chini ya uongozi wa Mwalimu.

Mzee Said mara zote hutaka kuonyesha ya kuwa Mwalimu aliwategemea sana kina Sykes kufanya kazi zake za siasa hapa Dar, hii si kweli.

Mwalimu alianza siasa tangu akiwa Chuoni Makerere na alianzisha Chama kabla ya baadae kushauriana na Wengine waliopo Dar (Mwalimu anamtaja Mzee mmoja wapo kwa jina la Mwangosi, wala sio kina Sykes) kwamba kwa nini asiendeleze tu harakati zilizopo tayari...ndipo alipoanzisha tawi la TAA na kuwa katibu pale chuoni.

Mwalimu alishajipanga kuwa atafanya kazi ya Ualimu kwa muda fulani na baadae aingie mazima kwenye siasa. Baada ya kuwa tayari na baada ya kuulizia viongozi wa TAA ndipo mmoja wa Wazee (Kasela Bantu) akampeleka kwa kina Sykes na Wenzake...kutoka hapo ndio ukaribu wa Mwalimu na kina Sykes ukaanza.

Kwa Mtu makini atagundua ya kuwa kulikuwa na Watu wengi wanaofahamiana na Mwalimu kabla hata ya kina Sykes. Kuna wale ambao Mwalimu huwataja kama "Wazee wa Dar"...Mwalimu ameshaeleza mengi namna walivyoshirikiana na Wazee hawa katika harakati zake, mengine yalihusisha hata duwa na imani zilizokuwa tofauti kabisa na imani ya Mwalimu lakini ilibidi akaze roho mambo yaende...walimpeleka hata makaburini kwa imani za Wazee wale....hii inaonyesha kina Sykes walikuwa na nafasi yao lakini bado kulikuwa na nafasi ya Wazee wengine wengi tu..na Mwalimu asingekwama hata kama kina Sykes wasingekuwepo.

Mwalimu ameelezea namna Wazee wa Dar walivyojenga imani kwake ndani ya muda mfupi, na anapowataja Wazee sio kina Sykes kwani wao wakati huo hawakuwa Wazee.

Hivyo huenda kweli kina Sykes walikuwa na mchango kwa Mwalimu lakini sio kwa asilimia 100 kama anavyotaka tuamini Mzee Said, huenda ni asilimia 30 tu na asilimia 70 zote kulikuwa na Wazee wengine. Mzee Said mara zote amekazana kuonyesha kuwa kila kitu kilianza baada ya Mwalimu kukutana na kina Sykes.

Kuna wakati Mzee Said atakwambia kina Sykes walilazimika "kumuachia" Mwalimu kiti kwenye chama...sasa Mtu yeyote mwenye akili timamu lazima tu utajiuliza huyo Mwalimu alikwa na nini cha mno?. Mwalimu hakuhitaji kuaminika na kina Sykes pekee kufanya kazi yake kuwa rahisi bali kulikuwa na kundi kubwa sana nyuma yake na walionyesha kumuhitaji Mwalimu ndani ya muda mfupi tu.
 
Kama ambavyo Mzee Said amekuwa anarudi jukwaani na nyuzi zake potofu...basi na mimi nitajaribu kurudia yale yale ninayoyafahamu juu ya mambo kadhaa...ni dhahiri kuwa kila Mtu anayesoma nyuzi za Mzee atakuwa anashtuka kuwa Mzee kuna ajenda anayojaribu kuisukuma kwa bidii bila hata kujali akama anapotosha ama la.

Kwa mfano hili la kusema Abdul ndiye muasisi wa TANU halina ukweli wowote maana TANU ilianzishwa kama "transformation" ya chama kilichokuwepo cha TAA, na alichofanya Abdul na Wenzake ni kupendekeza jina ambalo lilipitishwa na Wahusika kati ya majina kadhaa yaliyopendekezwa.

TAA ilibadilishwa kuwa TANU chini ya uongozi wa Mwalimu.

Mzee Said mara zote hutaka kuonyesha ya kuwa Mwalimu aliwategemea sana kina Sykes kufanya kazi zake za siasa hapa Dar, hii si kweli.

Mwalimu alianza siaa tangu akiwa Makerere na alianzisha Chama kabla ya baadae kushauriana na Wengine waliopo Dar (Mwalimu anamtaja Mzee mmoja wapo kwa jina la Mwangosi, sio kina Sykes) kwamba kwa nini asiendeleze tu harakati zilizopo tayari...ndipo alipoanzisha tawi la TAA na kuwa katibu.

Mwalimu alishajipanga kuwa atafanya kazi ya Ualimu kwa muda fulani na baadae aingie mazima kwenye siasa. Baada ya kuwa tayari na baada ya kuulizia viongozi wa TAA ndipo mmoja wa Wazee (Kasela Bantu) akampeleka kwa kina Sykes na Wenzake...kutoka hapo ndio ukaribu wa Mwalimu na kina Sykes ukaanza.

Kwa Mtu makini atagundua ya kuwa kulikuwa na Watu wengi wanaofahamiana na Mwalimu kabla hata ya kina Sykes. Kuna wale ambao Mwalimu huwataja kama "Wazee wa Dar"...Mwalimu ameshaeleza mengi namna walivyoshirikiana na Wazee hawa katika harakati zake, mengine yalihusisha hata duwa na imani zilizokuwa tofauti kabisa na imani ya Mwalimu lakini ilibidi akaze roho mambo yaende...walimpeleka hata makaburini kwa imani za Wazee wale....hii inaonyesha kina Sykes walikuwa na nafasi yao lakini bado kulikuwa na nafasi ya Wazee.

Mwalimu ameelezea namna Wazee wa Dar walivyojenga imani kwake ndani ya muda mfupi, na anapowataja Wazee sio kina Sykes kwani wao wakati huo hawakuwa Wazee.

Hivyo huenda kweli kina Sykes walikuwa na mchango kwa Mwalimu lakini sio kwa asilimia 100 kama anavytaka tuamini Mzee Said, huenda ni asilimia 30 tu na asilimia 70 zote kulikuwa na Wazee wengi tu. Mzee Said mara zote amekazana kuonyesha kuwa kila kitu kilianza baada ya Mwalimu kukutana na kina Sykes.

Kuna wakati Mzee Said atakwambia kina Sykes walilazimika "kumuachia" Mwalimu kiti kwenye chama...sasa Mtu yeyote mwenye akili timamu lazima tu utajiuliza huyo Mwalimu alikwa na nini cha mno?. Mwalimu hakuhitaji kuaminika na kina Sykes pekee kufanya kazi yake kuwa rahisi bali kulikuwa na kundi kubwa sana nyuma yake na waliomuhitaji Mwalimu.
May Day,
Ikiwa hiyo ndiyo historia yako ya TANU ilivyoasisiwa mimi sina tatizo.

Nakuwekea hapa historia ya kuasisiwa kwa TANU kama ninavyoifahamu mimi:

WASIFU WA JULIUS NYERERE: YALIYOMO NDANI YA HOTUBA YA KUAGA NA HALI ILIVYOKUWA

Kila ninapoisoma hotuba ya Nyerere ya kuaga nakuwa na maswali mengi sana kiasi huwa najiuliza hivi Abdul Sykes alipata kumweleza Nyerere historia yake yeye mwenyewe binafsi na historia ya TAA kabla hawajaunda TANU 1954?

Najiuliza swali hili kwa pale Nyerere anaposema TAA ilikuwa "inasinziasinzia," yeye ndiyo akaiamsha mwaka wa 1953 alipochaguliwa kuwa President.

Ukiingia katika Nyaraka za Sykes utakutana na mambo makubwa yaliyofanywa na TAA kuanzia 1950 wakati wa uongozi wa Dr. Kyaruzi na Abdul Sykes.

Kulikuwa na TAA Political Subcommittee iliyopeleka mapendekezo ya katiba kwa Gavana Edward Twining.

TAA katika mapendekezo yake muhimu walilopendekeza ni kuchaguliwa kwa kura kwa wajumbe wa Baraza la Kutunga Sheria badala ya kuteuliwa achilia mbali kuundwa kwa Kamati Ndogo ya Siasa ndani ya TAA.

Hilo la kwanza.

Pili namna Abdul Sykes alivyomwingiza rafiki yake, Wakili Earle Seaton ndani ya TAA kukishauri chama vipi waliendee suala la Tanganyika kama nchi chini ya udhamini UNO kuanzia 1950 na jinsi alivyoshirikiana na Seaton na Japhet Kirilo akiwa kiongozi wa Meru Citizens Union katika Meru Land Case.

Haya matatizo ya ardhi ya Wameru yalimalizikia kwa Kirilo kuhutubia UNO 1952 Seaton akiwa mkalimani wake.

Tatu Abdul Sykes alivyofanya mkutano wa siri na Jomo Kenyatta na viongozi wenzake wa KAU Nairobi mwaka wa 1950.

Waingereza walitaka kumnyima Kirilo pasi ya kusafiria na Abdul Sykes alikuja juu hadi serikali ikampatia Kirilo pasi na kumwezesha kusafiri kwenda New York.

Nne kulikuwa na juhudi kuanzia mwaka wa 1950 za Abdul Sykes kutaka kuunda TANU Chief David Kidaha Makwaia wa Siha akiwa Territorial President.

Mazungumzo baina ya Abdul Sykes na Chief Kidaha yalikwenda kwa kiasi cha miaka miwili lakini hayakuwa na mafanikio.

Mwalimu kaeleza kuwa alichaguliwa kuongoza TAA katika mkutano Ukumbi wa Arnautoglo mwaka wa 1953.

Ukweli ni kuwa uamuzi wa yeye kukabidhiwa uongozi wa TAA ulifanyika nyumbani kwa Hamza Mwapachu, Nansio Ukerewe na waliofanya uamuzi huo ni Mwapachu, Abdul Sykes na Ali Mwinyi Tambwe.

Uchaguzi wa Arnautoglo ulikuwa ni kukamilisha taratibu za demokrasia.

Bahati mbaya Mwalimu hakueleza aligombea na nani nafasi ya urais wa TAA.

Nyerere aligombea nafasi ile na Abdul Sykes.

Nyerere akachaguliwa rais na Abdul Sykes makamu wake.

Inaelekea Mwalimu hakuwa anayajua haya ndiyo maana akasema TAA ilikuwa usingizini.

Yapo ya katiba, safari zake majimboni baada ya kuundwa TANU ambazo Mwalimu anazichanganya si kuwa alianza kwenda wapi na alizungumza na nani bali hata maudhui ya mazungumzo anayaweka sipo.

Lakini kuna suala la kupokewa ambalo yeye kaweka umuhimu mkubwa kwa wazee ambao kwa bahati mbaya hawajulikani kwani hakuwataja majina.

Nyerere hakupokewa na wazee Nyerere alipokewa na Abdul Sykes 1952 na aliishi nyumbani kwa Abdul Sykes 1955 alipoacha kazi na mipango yote ya TANU siku za mwanzo ilikuwa ikifanyika nyumbani kwa Abdul.

Hii ndiyo sababu kadi ya Abdul Sykes ya TANU ni no. 3, Ally Sykes no. 2 na ya Rais wa TANU ni no. 1.

Wazee walimjua Nyerere kupitia kwa Abdul Sykes kwa maana ya Baraza la Wazee wa TANU baadae baada ya TANU imekwishaundwa na sasa mambo yako wazi hadharani si ya kujifichaficha tena.

Siwezi kueleza yote lakini haya niliyoeleza yanatoa picha ya mambo yalivyokuwa wakati ule kuelekea kuundwa kwa TANU na siku zake za mwanzo.
 
Agenda behind ni
Udini tu mtaniambia
Someni mada zake zote mada ni hiyo hataongelea jingine
Mzee ni bingwa wa kukwepa hoja ya msingi pale unapombana.

Mzee humtaja Mzee Waikela, lakini ukileta hoja uliyoitoa kwa huyo huyo Mzee Waikela Mzee Said anaipotezea.

Ukimfuatilia Mzee Waikela kwa makini utagundua ya kuwa pamoja na kwamba TAA iliasisiwa na Wafanyakazi wa serikali wa wakati huo ila Viongozi wake walikuwa na ajenda zao tofauti....huenda ni tangu mwanzo walipoanzisha chama au baadae chama kikiendelea na shughuli zake.

Nimewahi kumuhoji Mzee Said namna ambavyo TAA ilivyopeleka ujumbe UNO kuomba uhuru wa Tanganyika wakiwa kama kikundi cha kidini...na kule walifurushwa...ingawa Mzee aliniambia kuwa yeye hajawahi kusikia hilo.

Wao watakwambia Waingereza walihitaji Mkristo kwenda UNO, lakini hii haileti mantiki yoyote maana Waingereza wametawala nchi nyingi tu zenye Uislam kwa asilimia 70, 80, 95 na ulipofika muda walikabidhi uhuru nchi hizo zikiwa hivyo hivyo...sasa kwa hiyo nongwa ilikuwa Tanganyika tu?.

Waikela amewahi kusema namna walivyojaribu kumbana Mwalimu alipoenda Tabora kwenye harakati za uhuru wakimuuliza "ni nini hatma ya Uislamu baada ya Uhuru" na Mwalimu akamtahadharisha kuhusu udini akitolea mfano wa nchi zilizokuwa zina machafuko kwa sababu ya dini.

Hivyo ni kweli kunaweza kuwa na maswali kama kweli harakati za TAA zilikuwa ni kwa manufaa ya Watanganyika wote au kundi fulani tu.
 
WASIFU WA JULIUS NYERERE: HOTUBA KWA WAZEE WA DAR ES SALAAM KUWAAGA WATANZANIA UKUMBI WA DIAMOND JUBILEE NOVEMBA 5 MWAKA,1985

"Mimi nimeanza siasa na wazee wa Dar es Salaam; na wazee wa Tanzania.

Nimeanza nao mapema sana; mapema kweli.

Nilirudi kutoka masomoni, Uingereza Oktoba 1952 – miaka 33 nyuma.

Wakati huo nikiwa kijana mdogo wa miaka thelathini na kidogo hivi.

Niliporudi nikakubaliana na wamisionari hapo Pugu (sekondari), nifundishe shuleni kwao. Lakini nikiwa shuleni – Chuo Kikuu – nilijua.

Niliishaamua kwamba maisha yangu yatakuwa ya siasa.

Niliamua hivyo: Nitafundisha kwa muda wa miaka mitatu, nione hali inavyokwenda na kuzoeana na wenzangu kabla ya kuanza maisha ya siasa.

Niliporejea nchini hapo Oktoba, nikaenda Butiama.

Januari nikarudi Dar es Salaam.

Nikaanza kazi.

Nikataka kujua habari za African Association.

Mzee Mwangosi anakumbuka.

Yeye ndiye aliniambia habari za African Association.

Aliisha niambia habari hizo tangu nikiwa Makerere – Chuo Kikuu – nikiwa mwanafunzi.

Pale, mimi na wanafunzi wenzangu tulikuwa tumeanzisha chama kinachoitwa Tanganyika African Welfare Association (TAWA) cha wanafunzi wa Tanganyika; mimi nikiwa katibu wao. Hapa tukaona mambo yanakwenda vizuri kidogo.

Tukaona kwanini TAWA iwe ya wanafunzi peke yao na siyo Tanganyika nzima.

Kwa hiyo nikawaandikia baadhi ya watu Tanganyika. Nikasema, jamani ee, tumeanzisha chama, kwanini msianzishe huko matawi ya chama hicho?

Ndugu Mwangosi akapata barua hiyo.

Alikuwa miongoni mwa waliopata barua hiyo.

Akaniandikia – nikiwa Makerere – akasema: wewe kwanini unataka kuanzisha chama kipya?

Kipo chama.

Kipo chama cha TAA (Tanganyika African Association).

Kwa hiyo la maana siyo kuanzisha matawi, maana chama kipo na matawi yameenea; la maana ni kwamba hicho chama chenu mfute, na muanzishe tawi la Tanganyika African Association.

Hivyo ndivyo tulivyofanya.

Kwa hiyo mimi nikawa katibu wa katawi ka TAA hapo Makerere.

Niliporudi Tabora na kuanza kufundisha pale St. Marys (sasa inaitwa Sekondari ya Milambo) nikachaguliwa katibu wa TAA wa jimbo ambalo makao yake makuu yalikuwa Tabora.

Ulipofanyika mkutano wa TAA mjini Dar es Salaam, nilihudhuria nikiwa mjumbe kutoka Tabora.

Kwa hiyo nilikuwa naijua Tanganyika African Association.

Nilipokuwa ninaondoka kwenda Ulaya kusoma, nilikuwa nimeishaonja shughuli za TAA.

Sasa niliporudi, baada ya kukaa Pugu siku chache, nikaja mjini Dar es Salaam.

Nikauliza nani wanaongoza TAA?Nikaambiwa kuna jamaa mmoja anaitwa Abdul Sykes.

Sasa ni marehemu.
Abdul ndiye alikuwa katibu wakati huo.

Nilipelekwa na Kasela Bantu - ambaye naye aliteleza-teleza na hatunaye hapa (kwenye mkutano).

Kasela Bantu alikuwa mwalimu mwenzangu. Tulifundisha pamoja Milambo.

Nilipokuja Dar es Salaam, nikakuta anafanya kazi Redio (Tanganyika Broadcasting Corporation).

Ni Kasela Bantu aliyenipeleka kwa Sykes.

Wakati huo mambo yalikuwa yanasinzia kidogo. Kwa muda mfupi mwaka ule, tukafufua-fufua, hasa kutoka Januari.

Kufika Aprili, TAA ikafufuka.

Tukafanya mkutano hapo Arnautoglo.

Kwenye mkutano huu wakanichagua kuwa Rais wao – wa TAA.

Ninasema yote haya kwa shukrani kwa wazee.

Jamaa hawa walikuwa watu wazima wa Dar es Salaam, na mimi kijana mdogo Mzanaki, na Kiswahili changu si kizuri sana – cha matatizo.

Nimekuja, natoka Ulaya, tena masomoni.

Muda mfupi tu jamaa hawa wakaniamini haraka sana – katika muda wa miezi mitatu. Wakanichagua Rais wa TAA.

Hapo ndipo nilianza shughuli mpya ya kuandika katiba ya TAA na kuipa madhumuni hasa ya shabaha ya kuleta uhuru.

Baada ya miezi 13, hapo 1954, tukaanzisha TANU. Jina hili lilipendekezwa na akina Abdul Sykes.

Walikuwa wamelifikiria tangu zamani, walipokuwa askari vitani huko Burma (Vita vya Pili).

Miezi minne baada ya kuanza kazi Pugu nikawa ninakuja Dar es Salaam, kwa mguu; kila Jumamosi.

Baadaye wazee wakanipa baiskeli nikawa ninakuja mjini kukutana na wenzangu; kufanya mikutano.

Hivyo ndivyo tulivyofanya.
Wazee wakaniamini upesi sana.

Tukawa na uhusiano mkubwa sana.

Wadogo wenzangu wengine walikuwa Abdul Sykes, Abbas Sykes (mdogo wake), Dosa Aziz – waliokuwa wengi ni wazee.

Katika kuhutubia mikutano yangu, nilikuwa nikisema: Wazee na Ndugu zangu!

Wazee hasa ndio walikuwa na mikutano ya awali ya TAA na TANU.

Walikuwa na msimamo wa hali ya juu kabisa!

Hawakuyumba hata kidogo! Vijana walikuwa na mashaka.

Wengine walikuwa na vikazi vyao, waliogopa kuvipoteza.

Nalo jambo lenyewe ni la hatari – la kuzungumzia uhuru!

Unaweza ukakosa kazi; na wapo waliopoteza kazi; wengine wakaacha kazi.

Akina Rashid (Kawawa) waliona watoke kwenye shughuli hizo tuje tuungane katika chama.

Wazee wa Dar es Salaam, na baadaye wa nchi nzima, wakatuunga mkono, na kila nilipokwenda, watu wa kwanza walionielewa, walikuwa wazee.

Nilikwenda Songea mwaka 1955 mara baada ya kujiuzulu.

Huko wazee walinipokea na kunielewa.
Nilianza safari za kuitembelea Tanganyika nzima.

Nilikwenda Mbeya.

Mkutano wangu niliufanya na wazee; kikundi kidogo cha wazee, ndani ya nyumba ya mtu.

Kwa mkutano huu wa Mbeya, wazee wakauliza: Unatafuta nini?

Nikawaambia natafuta uhuru.

Wale wazee, kwa sababu ya vita vya Maji Maji, na wanakumbuka, kabisa, wakaona mimi ninatafuta jambo la hatari.

Tulifanya mkutano wa makini kweli.

Wakauliza: Wewe unawezaje kuleta uhuru?

Wewe una njia gani kudai uhuru na usitiwe kitanzi na Waingereza?

Tulielezana.

Nikawaambia ninyi wazee, Waingereza wanawadanganya, Waingereza wametumwa na ule Umoja wa Mataifa uliokufa (League of Nations), waje kuishika Tanganyika kwa muda tu; watusaidie, na wakati tutakapokuwa tayari, watuachie tukajitawale.

Waingereza wanafanya ujanja; hawasemi.

Vita vimekwisha (vya Pili) na Umoja wa Mataifa mwingine – mpya (United Nations Organisation – UNO) umewakabidhi Tanganyika kwa shabaha ileile.

Sisi siyo koloni lao.
Wamepewa dhamana tu.

Kwa hiyo nikawaambia wazee, hakuna haja ya kumwaga damu.

Tuwaseme tu!

Tuwashitaki kwa waliowaleta hapa kwamba hawafanyi kazi yao; wamesahau kabisa!

Wazee wakauliza: Eh, inawezekana?

Nikasema inawezekana.

Kazi yetu ya kwanza ilikuwa kuwaambia watu kwamba uwezekano wa kujitawala upo.

Hilo lilikuwa la kwanza.

Wazee walijua maana ya kujitawala. Walitamani kujitawala, lakini hawakujua waanzie wapi.

Vijana hawakuwa na habari kwamba kujitawala kunawezekana.

Kwa hiyo kwa wazee sikuwa na matatizo.

Wao hawakuwa na kazi; hawakumwogopa Mwingereza.

Hawakuogopa kufukuzwa kazi.
Baadhi walikuwa wafanyabiashara.

Mzee John Rupia (marehemu) alikwua mfanyabiashara na kaidi kidogo.

Aliwahi kutishwa na kunyang’anywa leseni yake ya biashara.

Akaambiwa akiendelea kushirikiana na kijana mwenda wazimu (Julius Nyerere), atanyang’anywa leseni moja kwa moja.

Rupia aliwajibu: Potelea mbali!

Nasema yote haya ikiwa njia ya kutoa shukrani kwa wazee na imani yao kwa vijana wakati huo.

Imani hujenga imani.

Na mambo haya makubwa ya nchi, kama hayana baraka za wazee hayaendi.

Magumu sana.

Wanasema ngoma ya watoto haikeshi!

Mimi nilipata baraka za wazee tangu zamani.
Tangu awali kabisa.

Siku moja, Dosa akanifuata Magomeni (Dar es Salaam).

Akasema: Leo wazee wanakutaka.
Wapi?

Kwa Mzee Jumbe Tambaza.
Wanakutaka usiku.

Nikasema haya, nitakuja.
Nikaenda.

Nikakuta wazee wameshakaa; wameniita kijana wao kuniombea dua.

Mimi Mkristo, wao Waislamu watupu.
Wakaniombea dua za ubani.

Tukamaliza.
Tulipomaliza wakasema kuna dua pia za wazee wao.

Basi wakanitoa nje.
Tukatoka.

Zilipomalizika zilikuwa za Korani; sasa zikaja dua za wazee – za jadi.

Walikuwa na beberu la mbuzi.
Wamechimba shimo.

Wakaniambia simama.
Nikasimama.

Beberu akachinjwa, huku anaambiwa, “Twining (Twainingi) umekwisha!” (Edward Twining alikuwa Gavana wakati huo).

Ndipo nikaambiwa: Tambuka!
Nikavuka lile shimo.

Hapo nikaambiwa na wazee: Basi nenda zako; tangu leo Twainingi amekwisha!

Sasa mimi Mkristo; hao Waislamu.

Na mimi mkorofi-korofi katika mambo haya (ya kutambika).

Lakini tulikuwa tunaelewana na wazee wangu hao.

Kwa hiyo nilitambuka pale na kuambiwa: Nenda nyumbani salama.

Twaining hawezi tena!

Wazee wangu wengine wanakumbuka tulikuwa tunakwenda Bagamoyo.

Kwenye makaburi kule!

Tunapiga dua huko kwenye makaburi na wazee wangu.

Baadhi yetu mtakumbuka safari moja jamaa wa Kenya, hawa akina Tom Mboya (marehemu) walishitakiwa.

Tukasema tuwasaidie.
Tuwasaidie vipi?

Tukasema tufunge.
Tukaomba nchi nzima kufunga siku hiyo.

Tufunge! Tukafunga.
Hakuna kula.

Na siku ya kufunga tulikuwa na mkutano Bagamoyo. Tukaenda huko.

Tukafanya mkutano hadi saa 12 jioni.

Baada ya mkutano tukaenda nyumbani kwa Mzee Mohamed Ramia (marehemu).

Hapa ndipo tulikuwa tumefikia.
Mimi nikamuuliza mzee: Sheikh, una Aspro?

Akajibu: Kwa nini unataka Aspro?

Nikajibu kuwa kichwa kinaniuma kwelikweli.
Akasema subiri.

Tulisubiri hadi saa ya kufuturu.
Tukafuturu vizuri.

Mzee Ramia akaniuliza: bado unataka Aspro?

Nikajibu kichwa sasa hakiumi.
Kumbe ilikuwa njaa.

Nawaelezeni haya kwa sababu huko tulikotoka, tulishikamana sana.

Tulishirikiana sana na wazee.
 
Hili halina haja ya mada sababu nimeshalimaliza, na huna hoja ya kupinga hili, na jambo kwa ujumla wake huna elimu nalo.

Hili kadhalika haliko nje ya mada, sababu wewe umeleta ujinga, lazima tukukosoe hapa hapa.

Nimecheka sana, yaani kitu unakiandika mwenyewe lakini unashindwa kutofautisha, sasa sisi tunaandika elimu, tunakukanya uache ubishi wa kijinga kwa jambo ambalo huna elimu nalo.

Wewe unadhani huo utumbo wako mimi nilikuwa na muda wa kuusoma?!!---- wala sikuusoma kabisa, kwanza nipo kazini pili mimi ninakufahamu kwani sijaanza leo kujadiliana nawe, Elimu yako ni ya aina ya "majini-paka na majini-mbwa" na ububusa (dogmatic) . Pia ni ya copy-pasting kibubusa.

Sio, juzi tu kulingana Qur'an nilikuambia kuwa Mitume walifika katika kila umma, kwa maana kwamba hata huku kwetu Africa nk, mitume walifika, ukabisha na huku ukitaka ushahidi kana kwamba hukuiona hiyo aya ya Qur'an!!.

Sasa kama unaweza kupingana na Qur'an mimi ni nani nikuweze???
 
Mzee Mohamed Said mengi unayoandika hasa haya ya kiduka cha Mama Maria Nyerere...yanavutia

nenda Mikocheni omba appointiment naye kamhoji...ya kiduka,fenicha,kupewa malazi na pia utapata ya ziada kusapoti historia ya Sykes na harakati zako
 
Like,
Mimi huwashauri wanaokuja kunihoji kuwa ni bora wakafanya mazungumzo na Mama Maria lakini wanasema kuwa Mama Maria ameshauriwa kupumzika asifanye mahojiano.

Nakuwekea hapa nyongeza katika historia ya TANU:

YALIYOJIRI MWAKA MMOJA NYUMA KABLA YA KUUNDWA KWA TANU: VIPI ILIUNDWA TANU NA NANI WALIUNDA TANU 1954?

Nimeulizwa swali hilo hapo juu katika group moja.

Swali nimelifanyia uhariri kidogo ili mada ikae vyema.

Jibu la swali hili ni hili hapa chini:

Nitakupa jibu kwa muhktasari.

Kuna waraka wa Kleist Sykes Secretary African Association wa mwaka wa 1933 akimwandikia Mzee bin Sudi aliyekuwa President wake.

Katika waraka ule Kleist alianza kuandika kwa maneno haya: "Bismillah Rahman Rahim."

Katika maneno mengi aliyosema mwisho aliandika kuwa juhudi hizi wanazofanya lazima wazifikishe mwisho na kama wao hawatafanikiwa basi hao watakaokuja baadae wafanikishe kuitoa Tanganyika kwenye mikono ya wakoloni.

Waraka huu upo katika mswada wa kitabu alichoandika Kleist Sykes kabla hajafariki mwaka wa 1949 na alimwachia mwanae Abdul na kwake ukawa kama usia.

Unaweza kuusoma waraka huu Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, East Africana, Daisy Sykes Buruku (1968) na Iliffe (1973).

Abdul Sykes alipokuwa Burma WWII (1939 - 1945) aliwakusanya askari wenzake katika 6th Battalion kutoka Tanganyika na kuwaambia wao ndiyo watakuwa msingi wa kuunda TANU wadai uhuru wa nchi yao.

Waliporudi Tanganyika mwaka wa 1945 wakaikuta African Association iko mikononi mwa wazee na hapakuwa na dalili ya mabadiliko.

Mwaka wa 1950 Abdul Sykes na Hamza Mwapachu wakaupindua uongozi wa Thomas Plantan akiwa TAA President na Clement Mtamila Secretary.

Waingereza hawakukubali hili wakatoa amri uitishwe uchaguzi.

Uchaguzi ukafanyika mwaka wa 1950 Dr. Vedasto Kyaruzi akawa President na Abdul Sykes Secretary nafasi ile ile iliyokuwa ikishikwa na baba yake kwa miaka mingi.

Mwaka huo wa 1950 Abdul akaunda Political Subcommittee ndani ya TAA kazi kubwa ikiwa kutayarisha mipango ya kuigeuza TAA kuwa chama kamili cha siasa kudai uhuru.

Pamoja na haya wakafanikisha safari ya Japhet Kirilo na Earle Seaton kwenda UNO mwaka wa 1952 katika madai ya mgogoro wa ardhi ya Wameru.

Wajumbe wa kamati hii walikuwa Vedasto Kyaruzi, Abdul, Hamza Mwapachu, Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Abdallah Chaurembo, Steven Mhando na John Rupia.

Waingereza waliona mwelekeo huu mpya wa TAA wakatishika wakatoa onyo kupitia Government Circular kadhaa kuhusu TAA kujiingiza katika siasa na wakawahamisha Dar es Salaam Mwapachu, Dr. Kyaruzi na wazalendo wengine wengi.

Baada ya kuondoka Dr. Kyaruzi Abdul akawa Act. President na Secretary na akaanza mazungumzo na Chief David Kidaha Makwaia amlete TAA wamchague kuwa President waunde TANU na Chief Kidaha aongoze harakati za kudai uhuru wa Tanganyika.

Mazungumzo haya hayakufanikiwa.

Chief Kidaha alikuwa msomi wa Oxford, Mwapachu University of Wales na alikuwapo Dr. Wilbard Mwanjisi aliyehitimu udaktari Makerere.

Kwa miaka kama mitatu Abdul akawa amekwama katika azma ya kuunda TANU lakini alikuwa na mshauri hodari na rafiki yake Earle Seaton mtu mweusi kutoka Bermuda na mwanasheria aliyemsaidia sana katika kusukuma mambo serikalini kwa Gavana Edward Twining na UNO.

Hiki ndicho kipindi Abdul alipojaribu kuunganisha harakati za TAA na KAU kwa kukutana na Jomo Kenyatta na wenzake akina Bildad Kaggia, Achieng Oneko, James Mbiu Koinange na Kung'u Karumba, Nairobi katika mkutano wa siri.

Lakini Hamza Mwapachu yeye akijuana na Julius Nyerere toka Makerere na walikuwa pamoja katika uongozi wa TAA Tabora mwaka wa 1948.

Nyerere alipokutana na Abdul Dar es Salaam mwaka wa 1952 ikawa Abdul kapata mwenzake waliokubaliana katika fikra zao.

Hamza Mwapachu na alimweleza Abdul kuwa Nyerere angefaa sana kutiwa katika uongozi wa juu wa TAA.

Uchaguzi wa TAA ulikuwa unakaribia mwezi April 1953.

Abdul na Ali Mwinyi Tambwe Secretary wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) wakaenda Nansio Ukerewe ambako Mwapachu alikuwa amehamishiwa, kupata kauli yake ya mwisho kuhusu kumuingiza Julius Nyerere katika uongozi wa TAA kama President katika uchaguzi uliokuwa mbele yao.

Hamza alielekeza kuwa Nyerere aingizwe katika uongozi na Abdul amsaidie kupata nafasi ile.

Mbali na sifa na uwezo ambao Hamza akiujua aliokuwanao Nyerere, Hamza alisisitiza kuwa Nyerere kama Mkristo katika kudai uhuru ataondoa hofu ya kuwa hizi ni harakati za Waislam peke yao.

Tarehe 17 April 1953 Nyerere alipambana na Abdul Sykes katika uchaguzi wa TAA Ukumbi wa Arnautoglo Hall.

Julius Nyerere akachaguliwa kuwa President na Abdulwahid Sykes Vice President.

Mwaka wa 1954 TANU ikaundwa.

Ni bahati mbaya sana kuwa katika uhai wake wote Nyerere hakupata kueleza historia yake vipi alipokelewa na Abdul Sykes na nduguye Ally na vipi kupitia kwa Abdul akajuana na wote waliokuwa katika harakati za kudai uhuru mfano wa Dossa Aziz, Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Suleiman Takadir, Mshume Kiyate, John Rupia na wengine wengi na vipi ikapangwa mipango ya safari ya UNO mwaka wa 1955 mwaka wa pili tu baada ya kundwa kwa TANU nk. nk.
 
Maneno nimengi swali lamsingi linabaki palepale bila majibu

KWA NINI BENJAMIN MKAPA ALISHINDWA KUCHAPA TAAZIA YA ABDUL SYKES(muasisi wa TANU) KATIKA MAGAZETI YA CHAMA??

Tangu kupitia nyuzi za mzee mohd said nilijigundua sinanijuacho chochote kuhusu mambo ya siasa zahapa nyumban
 
Wakubeti,
Wachangiaji inaelekea hawana jibu la swali hili kwa nini magazeti ya TANU yalishindwa kuchapa historia ya muasisi na mfadhili mkubwa wa TANU?
 
Mzee ni bingwa wa kukwepa hoja ya msingi pale unapombana.

Mzee humtaja Mzee Waikela, lakini ukileta hoja uliyoitoa kwa huyo huyo Mzee Waikela Mzee Said anaipotezea.

Ukimfuatilia Mzee Waikela kwa makini utagundua ya kuwa pamoja na kwamba TAA iliasisiwa na Wafanyakazi wa serikali wa wakati huo ila Viongozi wake walikuwa na ajenda zao tofauti....huenda ni tangu mwanzo walipoanzisha chama au baadae chama kikiendelea na shughuli zake.

Nimewahi kumuhoji Mzee Said namna ambavyo TAA ilivyopeleka ujumbe UNO kuomba uhuru wa Tanganyika wakiwa kama kikundi cha kidini...na kule walifurushwa...ingawa Mzee aliniambia kuwa yeye hajawahi kusikia hilo.

Wao watakwambia Waingereza walihitaji Mkristo kwenda UNO, lakini hii haileti mantiki yoyote maana Waingereza wametawala nchi nyingi tu zenye Uislam kwa asilimia 70, 80, 95 na ulipofika muda walikabidhi uhuru nchi hizo zikiwa hivyo hivyo...sasa kwa hiyo nongwa ilikuwa Tanganyika tu?.

Waikela amewahi kusema namna walivyojaribu kumbana Mwalimu alipoenda Tabora kwenye harakati za uhuru wakimuuliza "ni nini hatma ya Uislamu baada ya Uhuru" na Mwalimu akamtahadharisha kuhusu udini akitolea mfano wa nchi zilizokuwa zina machafuko kwa sababu ya dini.

Hivyo ni kweli kunaweza kuwa na maswali kama kweli harakati za TAA zilikuwa ni kwa manufaa ya Watanganyika wote au kundi fulani tu.
May Day,
Mjadala unapeneza lugha za kiungwana zikotumika.

Ukitumia lugha za " kufurushwa," unawakaribisha watu pengine hodari wa lugha mfano wa hizo kukushinda.

Kabla ya Nyerere kwenda UNO 1955 alitanguliwa na Japhet Kirilo 1952 mkalimani wake akiwa Earle Seaton.

Hapakuwa na kikundi kilichokwenda UNO kabla ya Kirilo na Nyerere.
 
Mohamed ana sifa moja kubwa miongoni mwa nyingi.
Ni mtu anayejua kuipeleka hadhra aliyoikusudia kule anakotaka.
Katika kufanisha mipango yake iwe kwa uzuri au ubaya kutegemea hoja, Mohamed hurudi jambo hata mara 1000. Mzee Said anafahamu, kurudia rudia uongo mara nyingi hugeuka kuwa ukweli.
Soma hapa chini
Kwa mtu anayesoma vitu juu juu, au asiye na ufahamu wa kina na mada au mwenye upungufu tu wa kibinadamu wa kuelewa, hoja ya Mohamed inasomeka tofauti lakini kwa mtazamo wa kusudio lake.

Msomaji ataamini kuwa Nyerere alitoka Butiama na kufikia kwa Abdul Sykes.
Na kwamba ujio wa Nyerere ilikuwa zao la juhudi za Abdul Sykes.
Hapo Mohamed atakuwa tayari amempa 'mbwa jina baya ili amuue''

Hapa ieleweke suala si uhusiano wa Nyerere na Abdul unaopingwa.
Nyerere alifika Dar es Salaam kwa mara ya kwanza katika mkutano mwaka 1948 akitokea Tabora.

Baadaye Nyerere alikuja Dar kufundisha kama Mwalimu kule Pugu.

Alipoacha kazi ya Ualimu ndipo alipokwenda kuishi na Abdul

Mohamed hawezi kukueleza mahusiano ya kufahamiana japo kwa juu juu kati ya Nyerere na Abdul

Atakachokueleza ni Nyerere kuishi kwa Abdul na atarudia mara 1000 na inageuka kuwa ''ukweli ''

Tumemueleza Mohamed, haiwezekani Chama kikawa na makao makuu Dar es Salaam chini ya Abdul Kleist Syke Mbuwane, na mwenyekiti huyo asitambue uwepo wa tawi kubwa sana la Tabora likiongozwa na katibu Nyerere.

Haiwezekani kwamba Nyerere alizuka mwaka 1948 kuja katika mkutano ambao watu hawamjui na wala hawakutaka kumjua baada ya hapo.

Ikiwa ni hivyo huyu Abdul atakuwa kiongozi Mpumbavu sana.
Abdul hakuwa mpumbavu! wa kutambua wasomi wachache sana enzi hizo Nyerere akiwa miongoni!

Na ikiwa ilitokea haitakuwa ajabu, Abdul alikuwa Askari na aliwahi kuwafurumusha kwa makonde baba zake katika mapinduzi ya chama, seuse kumtambua Nyerere!

Sina tatizo na mtazamo wa Mohamed wala historia yake.

Nina tatizo na jinsi anavyotumia kalamu yake kuudurusu uongo mara 100 hata kuufanya uwe ukweli kwa sababu rahisi tu '' ukitaka kumuu mbwa mpe jina baya'' na hapa Nyerere hakwepi jina.

Masalaam, narudi viungani kuokota kumbaa !

JokaKuu Pascal Mayalla Mag3
Nashukuru mkuu kwa kuelewa na kuweka wazi hila za huyu mzee! Mimi namchukulia kama mhalifu tu...anaepotosha kwa hila historia ya Mwl Nyerere kwa malengo ya "kishetani".
 
Mzee ni bingwa wa kukwepa hoja ya msingi pale unapombana.

Mzee humtaja Mzee Waikela, lakini ukileta hoja uliyoitoa kwa huyo huyo Mzee Waikela Mzee Said anaipotezea.

Ukimfuatilia Mzee Waikela kwa makini utagundua ya kuwa pamoja na kwamba TAA iliasisiwa na Wafanyakazi wa serikali wa wakati huo ila Viongozi wake walikuwa na ajenda zao tofauti....huenda ni tangu mwanzo walipoanzisha chama au baadae chama kikiendelea na shughuli zake.

Nimewahi kumuhoji Mzee Said namna ambavyo TAA ilivyopeleka ujumbe UNO kuomba uhuru wa Tanganyika wakiwa kama kikundi cha kidini...na kule walifurushwa...ingawa Mzee aliniambia kuwa yeye hajawahi kusikia hilo.

Wao watakwambia Waingereza walihitaji Mkristo kwenda UNO, lakini hii haileti mantiki yoyote maana Waingereza wametawala nchi nyingi tu zenye Uislam kwa asilimia 70, 80, 95 na ulipofika muda walikabidhi uhuru nchi hizo zikiwa hivyo hivyo...sasa kwa hiyo nongwa ilikuwa Tanganyika tu?.

Waikela amewahi kusema namna walivyojaribu kumbana Mwalimu alipoenda Tabora kwenye harakati za uhuru wakimuuliza "ni nini hatma ya Uislamu baada ya Uhuru" na Mwalimu akamtahadharisha kuhusu udini akitolea mfano wa nchi zilizokuwa zina machafuko kwa sababu ya dini.

Hivyo ni kweli kunaweza kuwa na maswali kama kweli harakati za TAA zilikuwa ni kwa manufaa ya Watanganyika wote au kundi fulani tu.
May Day,
Juma Volter Mwapachu ni mtoto wa Hamza Kibwana Mwapachu.

Nimejuana na Juma Mwapachu 1967 nikiwa na umri wa miaka 15 na amekuwa kaka na rafiki yangu hadi leo.

Miaka michache nyuma aliniandikia hayo hapo chini tafadhali soma:

''Mohamed kuna sehemu katika maelezo yako ambayo kwa kweli ni murua sana ambako katika kuwataja Bwana Abdul na Bwana Mwinyi na suala la Nyerere kupata nafasi ya Urais wa TAA mwaka 1953 ulikuwa utaarifu safari yao kwenda Ukerewe na kufikizia kwa Hamza.

Msingi wa safari ile haukuwa pleasure.

Ulikuwa kujadili uongozi wa TAA. Usisahau kwamba uongozi wa TAA wakati Abdul akiwa Rais ulizidiwa nguvu na Waislamu.

Hata Mzee Rupia alivutiwa sana na Waislamu.

Mzee Rupia alimpenda Hamza tangu 1945 na kumsaidia ujenzi wa nyumba yake ya kwanza mtaa wa Tabora, Mwanza. Rupia alikuwa tayari ni contractor wa ujenzi.

Safari ya Ukerewe ilikua kupata mawazo ya Hamza kuhusu mustakabali wa vita ya uhuru na nani aongoze.

Waislamu Dar walimtaka Abdul.

Hamza aliwashauri kumkubali Nyerere na aliwapa sababu nyingi mojawapo ni Ukristo mbali na maarifa yake.

Hamza hakuwa mgombea kwa sababu za kifamilia.

Nakumbuka safari hiyo nikiwa darasa la nne hapo Bukongo Primary school.

Nilisikia mazungumzo yao.

Na kuja kwao ilibidi kaka Bakari na mimi tuhamishwe chumba cha kulala.

Jamani, historia ya TANU bado mbichi.
 
Nashukuru mkuu kwa kuelewa na kuweka wazi hila za huyu mzee! Mimi namchukulia kama mhalifu tu...anaepotosha kwa hila historia ya Mwl Nyerere kwa malengo ya "kishetani".
Mzizi...
Nimeweka jibu na rejea kutoka kwa Juma Mwapachu.
Soma inaweza kuongeza afya katika mjadala huu wetu.

Nakuomba punguza hamaki huu ni mjadala tu wewe unayo ambayo mimi utanifunza na mimi ninayo ambayo wewe hyajui na ukiyasikia utakuwa umeongeza elimu yako.

Na hii ndiyo ibra ya kushangaza ya historia hii hapa kwetu.

Wengi wakiisikia wanapandwa na hasira lakini nje ya mipaka yetu nimefanya mihadhara mingi na husikii mtu kughadhibika.
 
Ila Mohamed sasa naona unaleta story za kwenye vijiwe vya kahawa magomeni.... 😂😂

Mwalimu Nyerere alipohamia Magomeni mwaka wa 1955 Ali Msham alimfungulia Mama Maria kijiduka kidogo hapo kwake cha kuuza mafuta ya taa.

Mama Maria alikuwa pia akiwa dukani kwake akifuma sweta.

Siku moja Ali Msham alikwenda ofisini kwa Mwalimu Nyerere pale New Street akakuta samani alizokuwa akitumia Mwalimu ni duni sana.

Jile,
Angalia hizo picha hapo chini siku Ali Msham alipomkabidhi Nyerere samani mpya na saa ya ukutani kwa ajili ya ofisi yake pale.

Angalia hao waliosimama nyuma ya Nyerere utaona kuna mwanamke amshika saa.

Kulia wa kwanza ni Ali Msham na Nyerere amekaa kwenye meza.

Huu ni Mtaa wa Jaribu Magomeni Mapipa ambako ndiyo nyumbani kwa Ali Msham na ndipo alipofungua tawi la TANU.
ALI MSHAM.jpg

Zuhra Yunus ana kipindi kinaitwa, ''Zoom na Zu.''

Juma lililopita nilishiriki katika kipindi hiki ambacho nia ilikuwa kuwakumbuka wazalendo ambao historia imewasahau.

Mimi nilimzungumza Ali Msham na Iddi Faiz Mafungo.
Namzungumza Ali Msham dakika ya 35:

Back
Top Bottom