Mimi kijana wenu mpendwa ninawasalimu sana. Ni muda mrefu toka tuonane kipindi kile nikiwa napita hapo Ruangwa nikielekea Nachingwea shuleni.
Utulivu huu ulipo wikendi hii unaletwa kwa hisani yenu wazee. Hatujasikia matusi wala makelele ktk Runinga zetu wala redio wikendi hii tuna Amani kweli kweli.
Wakati tumedhulumiwa nyongeza za mishahara kwa miaka minne, kutopandishwa vyeo kwa wakati, kutolipwa pesa za likizo, na dhuruma kede kede Mtu anatuongezea mimatusi na kebehi za ulevi wa madaraka.
Wazee endeleeni na Moyo huo huo wa kulipenda taifa letu. Ninyi ndio tumaini pekee lililo bakia kuleta Amani na utulivu mioyoni mwetu wana wa nchi.
CC wapenda Amani