Pitia hapa mkuu mwaka 1095 ndio wakristo walianza kuchinja watu wote waliokataa kubatizwa
Crusades - Wikipedia
Sio Wakristo Sema Waroman Cathorik ndio waliotisha waliokataa kubatizwa.
Watu wanashindwa kutofautisha kati ya Wakristo na Waroman Cathorik.
Roman Kathorik ni dhehebu kama walivyo Wa-Shia au Suni katika Uislam.
Sio Wakristo wote ni Roman.
Papa ni Kiongozi wa Waroman na sio Wakristo wote.
Imani ya Ukristo hairuhusu Kuadhibu watu katika kosa liwalo lolote lile. Wanaaambiwa anayeruhusiwa kuadhibu ni Mungu peke yake kwenye Makosa ya Kiroho.
Ukiona kundi la watu linaadhibu watu kwa kujidai lina mamlaka ya kiimani hao watakuwa watu wa dini fulani au dhehebu fulani na wanatimiza malengo ya dini hiyo na sio Ukristo.
Ukristo ni
"Kufanya mambo aliyo agiza Yesu Kristo kuyafanya kupitia mafundisho yake ya namna ya kuurithi ufalme wa Mbingu"
Hao waliochinja watu kwa kukataa kubatizwa sio Wakristo ingawa labda wenyewe walijiita hivyo kwakuwa hakuna agizo lolote toka kwa Kristo Yesu linalosema watu wasiotii maagizo yake wachinjwe.
Endelea kukumbuka kila wakati kuwa kuna Wakristo na wengine wanaoweza kujiita Wambagala, Waebrania, Waufufuo, Waroma, Wasabato, wainjiri nk.
Hayo ni majina tu ya dini na kujitambulisha lakini majina hayo hayawafanyi wawe Wakristo.
Sema Waroma waliwaua watu kipindi fulani kwa kuwalazimisha kubatizwa na sio Wakristo kwani haikuwa ajenda ya Kikristo na haitakuwa.