Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hahahahaha najua mkuu ila wwe na mwenzio Kiranga ni atheists sasa hizi mada zinazogusa dini huwa tunawakwepa msije mkawafanya watu wakimbie nyumba za ibada 😀😀mkuu unajua mi ni guru wa haya mambo lakini hutaki kunipa tag
najua unaogopa ukweli mchungu
hebu nisije kuyumbisha imani yako pendwa ya kiristo😀😀
Duh uko deep sana sikuwa na hili wazo.... Ina maana chuki bado inaendelea au coincidence tu.... Very interesting!.. Je unajua pia kuwa mtu aliyetaka kumuua papa John Paul wa 2 kuwa (Mehmet Ali Agca) ana nasaba na huyo Mehmed?!. Wonders
Sio yeye ambaye alikua vampire ni yule mfalme wa romaniaHivi zile shutuma kwamba alikuwa vampire ni za kweli au wazungu tu walitaka kumchafua aonekane shetani
Huyu Mehmed II naona ndio alikuwa hatari zaidi maana aliweza kuwapiga biti hadi ulaya ikatetemekaHivi huyu au Suleman I the magnificent nani alikua anaitisha ulaya zaidi
Hiyo story ina ukweli kumbe.... So vampires do exist??Sio yeye ambaye alikua vampire ni yule mfalme wa romania
Ukiwa mzuri au akakupenda aahh jiandae kuwa kimada wake!!..
Mkuu Yule alikua anahubiri au anachinja watu waliokataa kuslimaiseee....hiyo laana kumbe ndio maaana alikufa kiboya "" hiyo dini alikuwa anaitangaza vipi sasa wakati alikuwa mshenzi "" yaani anahubiri watu wafnye mambo ambayo yeye mwenyew yanamshinda ...huu ulimwengu bwana
Mehmet hakujua kuwa wabunifu wa dini yake ya kiislam ni vaticani kwa lengo la kuua ukristo wa kweli,lakina sio kuua mamlaka ya upapa.dini ya kiislamu iliazinshwa kwa siri na kanisa la roman catholic kwa kuwatumia jesuits na Khadija mama mjane tajiri kwa wakati huo amabae alilirisha kanisa mali zake zote na akaolewa na mtume Muhamad.View attachment 722372 View attachment 722373 Habari za mchana wakuu kama kichwa cha thread kinavyosema kwenye historia ya ulaya na kiislam kulikuwa na mfalme wa Ottoman empire dola ya kiislam hii iliyovamia ulaya kutokea mashariki ya kati na asia kwa sababu za kupanua utawala wao na dini pia.
Katika miaka ya 1400 walifanikiwa kuikamata constantinople iliyokuwa makao makuu ya byanztium empire ambayo ilikuwa ndio tawi la Dola ya kirumi mashariki ya ulaya na ilikuwa chini ya wakristo ila Mehmed II alifanikiwa kukamata mji huu na kufuta ukristo na kuifanya dini ya kiislam kushamiri mpaka leo yaani uturuki ya sasa na nchi za jirani.
Sasa baada ya kumalizana na tawi hili la mashariki Mehmed II hapo kati aliteka miji mingi tu ya ulaya ila mwishoni kabisa alielekea kuvamia makao makuu ya dola ya kirumi yani Rome ili kuitawala na penginepo kufuta ukristo ulaya nzima maana kama makao makuu ya wakatoliki wakisilimu je nchi gani ya ulaya ingebaki na ukristo??
Alianzia mji wa Otranto hapo italia kwa kuwavamia na kutaka wasilimu walivyogoma alichinja mji mzima na alikuwa amepanga sasa kuelekea Roma na alikua ameagiza majeshi zaidi yatiririke ili kufanikisha adhma yake.... ila usiku mmoja kabla ya kuanza vita ya kuelekea Roma alifariki ghafla na hivyo mpango huo ukafia naye na tokea hapo hakuwahi patikana mtawala wa ottoman mwenye dhamira na uwezo wa kuvamia Roma tena.
Sasa wajuvi wa mambo naomba mtujuze je nini hasa kilimuua Mehmed II aka Mehmet the conqueror shujaa huyu wa kiislam je aliwekewa sumu?? Alisalitiwa?? Aliuawa na wakatoliki ?? Na kivipi jemedari huyu masaa machache kabla ya tukio la kihistoria afariki ghafla maana wajuzi wa mambo wanasema kma sio kifo chake leo hii ulaya nzima ingekuwa imesilimu
Naomba kuwasilisha
Cc Palantir Malcom Lumumba Eiyer MSEZA MKULU na wanajukwaa wote
NB: Mods naomba uzi huu msiufute maana huwa mnazimoderate then mnazifuta hii inavunja moyo sana watu kuanzisha thread za kufikirisha jukwaa hili maana wanatumia muda kutafiti alafu tafiti zao zinaishia kutupwa kapuni.....
Duh hii mbona kali mkuu..... Dunia ina siri nyingi sana hiiMehmet hakujua kuwa wabunifu wa dini yake ya kiislam ni vaticani kwa lengo la kuua ukristo wa kweli,lakina sio kuua mamlaka ya upapa.dini ya kiislamu iliazinshwa kwa siri na kanisa la roman catholic kwa kuwatumia jesuits na Khadija mama mjane tajiri kwa wakati huo amabae alilirisha kanisa mali zake zote na akaolewa na mtume Muhamad.
lengo la jesuits ililikuwa kuua ukristo uliokuwa umeshamiri ulaya mashariki mpaka mashariki ya kati na Afrika kaskazin.
siri wanayo viongozi wa juu wa dini hizo,ndio maana ukatoriki na uislam una vitu vinafanana,na uislam unaukosoa mno ukatoriki zaidi kuliko ukristo kwa ujumla.mengi yanayokosolewa msingi wake ni mapokeo ya kipagani ya kanisa la katoliki
mtafte jesuit Alberto RiveraDuh hii mbona kali mkuu..... Dunia ina siri nyingi sana hii
Hiyo sio hearsay ilikuwa ni utaratibu wa kipindi hicho hebu search catamite ujionee ni nini!.hta idd amini tuliambiwa anakula nyama za watu na kwenye movie tukaonyeshwa....wazee wa propaganda wakianua lao huwa hawashindwi
mimi sio atheist kama kirangaHahahahaha najua mkuu ila wwe na mwenzio Kiranga ni atheists sasa hizi mada zinazogusa dini huwa tunawakwepa msije mkawafanya watu wakimbie nyumba za ibada 😀😀
story ya "Vampire" haina ukweli wowote!. Zamani baba yake Vlad the Impaler (dracula) alikuwa anaitwa Vlad ambapo baada ya kutoka pigana crusade akarudi Transvania kutawala akaadapt neno 'The Dracul' ambalo kwa english lilimaanisha " The Dragon" so akawaita na watoto wake "Dracula" ambalo lilimaanisha "Son of the DDragon", baada ya kufa na mtoto wake mmoja kurithi ufalme ingawa hakuurithi kiamani ilibidi jamaa amuue binamu yake alliyekuwa amewekwa kama mfalme. Huyu Vlad II akaja kuitwa "dracula" yeye alikuwa katili kweli!!.. Alikuwa akikamata adui hakuwa na haja ya kuwaua lakini alikuwa anawakata kifundo (kile kisehemu kwenye mguu- sijui nimepatia kiswahili chake) ina maana wenzenu wakija wanawakuta mpo chini mnaumia na wengine lazima naturally Mfe!...Hiyo story ina ukweli kumbe.... So vampires do exist??
Mkuu nakubaliana na wewe kabisa huyu Mehned The Conqueor alifariki 3 May 1481 kwa ugonjwa ambao haukutajwa japo alipigana vita vingi sana.Hongera kwa kuanzisha uzi murua kabisa.
Hemed II kimsingi aliugua na kufariki dunia mwaka 1481 akiwa katika kampeni ya kivita huko Italy, japo mpango ulikuwa pia kuikamata Misri.
Ugonjwa uliomuua mpaka leo haujafahamika.
Lakini kabla ya mauti yake alikuwa mtu anayesumbuliwa sana na magonjwa ya viungo kwa muda mrefu hali iliyopelekea mpaka mguu wake mmoja kuharibika kabisa(kuwa deformed), pia alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa gout.
Siku mbili kabla ya kifo chake aliugua ugonjwa wa tumbo na hakuweza kabisa kutokea kwenye ukaguzi wa vikosi vyake kama ilivyo ada ya wababe wa kivita kwa wakati huo.
Lakini taarifa za siri kutoka Ottoman Empire zinasema aliwekewa sumu na mtoto wake wa kwanza ambaye alikuwa pia mrithi wake mtarajiwa aliyejulikana kwa jina la Bayezid kwa sababu ya uchu wa madaraka.
Ikumbukwe kuwa Hemed II alikuwa na miaka 49 tu wakati mauti inampata, kwa picha hio ina maana kuwa alikuwa bado na safari ndefu sana ya kutawala, almost miaka 40 mbele, kitu ambacho dogo aliona kama "kinamchelewesha", ikabidi amuwahishe baba mapema.
Ni propaganda tu hii....UISLAMU unafanana zaid na uyahud kuliko ukristo....kwa sabab katka series ya mitume wote na the same bloodline na Muhamamad alitumwa kuja kukamilisha kile kilichoanzishwa na nabii Adam....hakuja na jipya sana isipokuwa Quran tukufu ambayo n mjumuisho wa Torati la kweli, zaburi iliosahih, injili ya kweli na Quran yenyewe iliokamilisha mfumo sahihi wa maisha uliokusudiwa na Mwenyezi.......ndio maana hutoona tofauti kubwa baina ya Uyahudi na Uislam. Mtume Muhammad n wa mwisho katka ile bloodline ya kitume toka kwa Nabii Ibrahim(Baba wa Mitume)Mehmet hakujua kuwa wabunifu wa dini yake ya kiislam ni vaticani kwa lengo la kuua ukristo wa kweli,lakina sio kuua mamlaka ya upapa.dini ya kiislamu iliazinshwa kwa siri na kanisa la roman catholic kwa kuwatumia jesuits na Khadija mama mjane tajiri kwa wakati huo amabae alilirisha kanisa mali zake zote na akaolewa na mtume Muhamad.
lengo la jesuits ililikuwa kuua ukristo uliokuwa umeshamiri ulaya mashariki mpaka mashariki ya kati na Afrika kaskazin.
siri wanayo viongozi wa juu wa dini hizo,ndio maana ukatoriki na uislam una vitu vinafanana,na uislam unaukosoa mno ukatoriki zaidi kuliko ukristo kwa ujumla.mengi yanayokosolewa msingi wake ni mapokeo ya kipagani ya kanisa la katoliki
ndugu fuatilia vizuri history ..hakuna dini ambayo haijawahi kuchinja watu ....Mkuu Yule alikua anahubiri au anachinja watu waliokataa kuslim