Nini kilimuua Mehmed II aliyetaka kuufuta ukristo/dola ya kirumi ulaya ??

Nini kilimuua Mehmed II aliyetaka kuufuta ukristo/dola ya kirumi ulaya ??

Mkuu zitto junior ,
Hapa tunaweza kusikia mengi sana kuhusiana na Vatican au nguvu ya Papa.
Lakini jambo la msingi ni la kujiuliza hivi ni kweli Vatican ndiyo ilimuua mfalme wa Mehmed baada ya kuwatangazia vita ??
Hili jibu hata mimi sina japo tunaweza kutoa mawazo mbali mbali kama kweli jamaa angefutilia mbali dini ya Ukristo hapa duniani. Moja ya sheria ya kusoma historia ni kuweza kuyatafsiri matukio kulingana na mazingira ya wakati huo ili kuweza kutanua uelewa katika kuchambua mambo; hivyo kwenye historia huwa najiepusha sana na maneno kama "Ingekuwa hivi" au "Ingefanyika hivi" kwa Lugha ya Kiingereza tunasema The Study of History doesn't have "If/If's" or "the could have been". Tukianza kuchambua historia katika mtazamo huu bila vithibitisho basi tutakuwa tunasoma Revisionist History au Political Science na mwishowe tutakuwa na mijadala mizito sana ambao hauwezi kuisha. Japo binafsi napenda sana mijadala ya hivi kwasababu inatuongezea taarifa mpya na mwono wa kitofauti wa historia.

Japo kwa leo katika hii mada,
Siwezi kuongea sana lolote na ntataka sana niwe msomaji wa maoni ya wengine.
Lakini ninachokijua cha muhimu ni kwamba Sultan Mehmed II alikufa bila kumaliza Jihad yake ya huko Vatican.
Huu ndiyo ukweli na wala huawezi badilishwa na mtu yeyote yule. Hivyo basi tusema tukubali kama kweli Vatican walikuwa na mkono wao juu ya kifo cha huyu Sultani wa Ufalme wa Kiislamu wenye nguvu sana hapa duniani kuliko hata falme za Ulaya kwanini haya hawakuweza kuyazuia huko Ulaya ??:

1. Kwanini Vatican hawakuweza kumzuia Napoleon Bournaparte alivyovamia Italia mwaka 1796 na kuvamia Vatican, wakavishinda vikosi vyote vilivyokuwa vinalinda Papa na kumkata Papa Pius na kumfungia huko. Napoleon Bournaparte alikuwa Ufaransa lakini Wakatoliki walimshindwa kabisa, mpaka alivyoamua yeye mwenyewe kulirudisha nguvu ya kanisa kwa malengo yake ya kisiasa. Kwanini hawakulizuia hili tukio ambalo ndilo lilivunja kabisa mgongo wa nguvu ya Kanisa Katoliki kwasababu walinyang'anywa eneo kubwa la Ardhi na kupunguziwa ushawishi kwa miaka zaidi ya mia hadi pela waliposaini Mkataba wa Lateran mwaka 1929 na Benitho Mussolini wa Italy ???

2. Kwanini Vatican hawakuweza kumshinda Malkia Mwanamke Elizabeth I baada ya kutuma vikosi vya meli za Kijeshi kutoka Ufalme wa Uhispania mwaka 1588 ili kurudisha Ukatoliki visiwani Uingereza. Mfalme Philipo wa Uhispania alifanya maandalizi kwa miaka minne huku akipewa baraka zote za Papa akavamia Uingereza na meli 130 zenye wanajeshi 30,000 na Mapadri 180 ambao walikuwa wanawafanyia maombi na kuwahakikishia kwamba Ukatoliki utawaushinda Uanglikani (Uprotestanti) na watafanikiwa tena kuvitwaa visiwa vya Uingereza. Mbona wakina Papa hawakufanikiwa kumuua huyu mwanamke aliyeumiza maslahi makubwa ya kanisa ??? (Usisahau kwamba Uhispania ndiyo walikuwa dola lenye nguvu barani Ulaya kipindi hicho kama ambavyo tunawaona Wamarekani leo hii)

NB: Mifano iko mingi sana ambayo imewaumiza Vatican lakini hawakufanya lolote zaidi ya kuwa wapole,
Hivyo basi kweli Sultan Mehmed II anaweza kweli kuwa alikuwa kwa kuumwa, kuuliwa au kufanyiwa fitna na watu wake kama ambavyo Mfalme Alexander wa Ugiriki alipewa sumu na Majemedari wake baada ya Vita vya Hindu Kushi...(Mengi yanawezekana lakini tusijikite sana kwenye hilo la kuuwawa na Vatican kwasababu tutakuwa tunafumbia macho sababu nyingine za kihistoria ambazo zinaweza kuwa ndiyo chanzo cha kifo chake haswa)
 
Aseee pope pius itakua huyo..... Sijui alipataje huo ujasiri

Lilikuwa ni vugu vugu la mapinduzi ya Kiraia ya Ufaransa ya mwaka 1789.
Kipindi cha Utawala wa familia ya Bourbon ya mfalme Lous na baba zake, familia chache zilitawala Ufaransa huku Ukatoliki ukiwa kame ni sehemu ya Utawala wa nchi. Walimiliki Ardhi kubwa na sehemu kubwa ya Utajiri huku watu wakiwa na maisha mabaya hivyo walivyopindua nchi Jacobins (Wanamapinduzi wa kijamaa) walianza kuwashughulikia wote waliokuwa wanaonekana ni wanyonyaji na wakandamizaji. Bahati mbaya Kanisa la Katoliki na Vatican wakonekana wanahusika moja kwa moja.
 
Aiseeee umenifungua mengi sikufaham kama papa alishindwa kuikwaa uingereza

Huwa unanikosha sana Role model wangu.... Embu nipe data kidogo kuna mdau hapo juu kaulia kati ya suleiman the magnificent na mehmet the conqueror nani alikuwa SHUJAA zaidi wa ottoman empire
 
Sio Wakristo Sema Waroman Cathorik ndio waliotisha waliokataa kubatizwa.
Watu wanashindwa kutofautisha kati ya Wakristo na Waroman Cathorik.
Roman Kathorik ni dhehebu kama walivyo Wa-Shia au Suni katika Uislam.
Sio Wakristo wote ni Roman.
Papa ni Kiongozi wa Waroman na sio Wakristo wote.

Imani ya Ukristo hairuhusu Kuadhibu watu katika kosa liwalo lolote lile. Wanaaambiwa anayeruhusiwa kuadhibu ni Mungu peke yake kwenye Makosa ya Kiroho.
Ukiona kundi la watu linaadhibu watu kwa kujidai lina mamlaka ya kiimani hao watakuwa watu wa dini fulani au dhehebu fulani na wanatimiza malengo ya dini hiyo na sio Ukristo.

Ukristo ni
"Kufanya mambo aliyo agiza Yesu Kristo kuyafanya kupitia mafundisho yake ya namna ya kuurithi ufalme wa Mbingu"

Hao waliochinja watu kwa kukataa kubatizwa sio Wakristo ingawa labda wenyewe walijiita hivyo kwakuwa hakuna agizo lolote toka kwa Kristo Yesu linalosema watu wasiotii maagizo yake wachinjwe.

Endelea kukumbuka kila wakati kuwa kuna Wakristo na wengine wanaoweza kujiita Wambagala, Waebrania, Waufufuo, Waroma, Wasabato, wainjiri nk.
Hayo ni majina tu ya dini na kujitambulisha lakini majina hayo hayawafanyi wawe Wakristo.

Sema Waroma waliwaua watu kipindi fulani kwa kuwalazimisha kubatizwa na sio Wakristo kwani haikuwa ajenda ya Kikristo na haitakuwa.
So dini ya ukristo nayo ni nini
 
Ni lini waislam wameanza kuabudu majini au umekaririshwa tu mkuu..... Yaani waache kumuabudu Allah waabudu viumbe??? Duh
Anyway ngoja nikawaite wenye dini zao

Cc kahtaan hydroxo inamankusweke
Amemezeshwa huyo wala usitumie akili nyungi juu yake
 
Lilikuwa ni vugu vugu la mapinduzi ya Kiraia ya Ufaransa ya mwaka 1789.
Kipindi cha Utawala wa familia ya Bourbon ya mfalme Lous na baba zake, familia chache zilitawala Ufaransa huku Ukatoliki ukiwa kame ni sehemu ya Utawala wa nchi. Walimiliki Ardhi kubwa na sehemu kubwa ya Utajiri huku watu wakiwa na maisha mabaya hivyo walivyopindua nchi Jacobins (Wanamapinduzi wa kijamaa) walianza kuwashughulikia wote waliokuwa wanaonekana ni wanyonyaji na wakandamizaji. Bahati mbaya Kanisa la Katoliki na Vatican wakonekana wanahusika moja kwa moja.
Umegusia mapinduzi ya ufaransa..... kwa miaka mingi wamesifia sana kikosi cha swiss guards kumlinda papa kwa ufanisi sana je kivipi kilishindwa kumlinda Mfalme Louis hadi akauawa??

Hivi napoleon hakuwa pandikizi la watu fulani sababu inakuaje wakati wa mapinduzi hakuwepo wakatawala kina Robespierre na danton ila anayekuja kubeba madaraka na ushawishi wote alikuwa napoleon..... Au kuna siri nzito hapa imejificha

Embu tuhabarishe hapa kwa faida ya wote mkuu
 
View attachment 722372 View attachment 722373 Habari za mchana wakuu kama kichwa cha thread kinavyosema kwenye historia ya ulaya na kiislam kulikuwa na mfalme wa Ottoman empire dola ya kiislam hii iliyovamia ulaya kutokea mashariki ya kati na asia kwa sababu za kupanua utawala wao na dini pia.

Katika miaka ya 1400 walifanikiwa kuikamata constantinople iliyokuwa makao makuu ya byanztium empire ambayo ilikuwa ndio tawi la Dola ya kirumi mashariki ya ulaya na ilikuwa chini ya wakristo ila Mehmed II alifanikiwa kukamata mji huu na kufuta ukristo na kuifanya dini ya kiislam kushamiri mpaka leo yaani uturuki ya sasa na nchi za jirani.

Sasa baada ya kumalizana na tawi hili la mashariki Mehmed II hapo kati aliteka miji mingi tu ya ulaya ila mwishoni kabisa alielekea kuvamia makao makuu ya dola ya kirumi yani Rome ili kuitawala na penginepo kufuta ukristo ulaya nzima maana kama makao makuu ya wakatoliki wakisilimu je nchi gani ya ulaya ingebaki na ukristo??

Alianzia mji wa Otranto hapo italia kwa kuwavamia na kutaka wasilimu walivyogoma alichinja mji mzima na alikuwa amepanga sasa kuelekea Roma na alikua ameagiza majeshi zaidi yatiririke ili kufanikisha adhma yake.... ila usiku mmoja kabla ya kuanza vita ya kuelekea Roma alifariki ghafla na hivyo mpango huo ukafia naye na tokea hapo hakuwahi patikana mtawala wa ottoman mwenye dhamira na uwezo wa kuvamia Roma tena.

Sasa wajuvi wa mambo naomba mtujuze je nini hasa kilimuua Mehmed II aka Mehmet the conqueror shujaa huyu wa kiislam je aliwekewa sumu?? Alisalitiwa?? Aliuawa na wakatoliki ?? Na kivipi jemedari huyu masaa machache kabla ya tukio la kihistoria afariki ghafla maana wajuzi wa mambo wanasema kma sio kifo chake leo hii ulaya nzima ingekuwa imesilimu

Naomba kuwasilisha

Cc Palantir Malcom Lumumba Eiyer MSEZA MKULU na wanajukwaa wote

NB: Mods naomba uzi huu msiufute maana huwa mnazimoderate then mnazifuta hii inavunja moyo sana watu kuanzisha thread za kufikirisha jukwaa hili maana wanatumia muda kutafiti alafu tafiti zao zinaishia kutupwa kapuni.....
Hayakuwa mapenzi ya Mungu.
 
Ukatoliki ni Dini Pekee Mungu anayoiamini, hauwezi kushindana na Ukatoliki!, Ee Mungu Baba Mwenyezi Libariki Kanisa Lako Kuu takatifu Katoliki la Mitume!
 
Hispania ilikuwa nchi ya Kiislam, ilikombokewa baadae katika vita ya Msalaba. Sina uhakika na historia ya Ureno ingawa ninafahamu mji wa Fatima uliopo Ureno ulipata jina lake kutokana na mfalme kumpa mji ule binti yake kama zawadi.
Kipindi cha Mfalme Ferdinand ndio uislam uliisha ndani ya Hispani baada ya kuoa Binti Mfalme wa Uingeleza ambaye alikuwa mkatoliki na alichukizwa na kuona nchi ya uhispania ikiwa ya kiislam

Hivyo akamshawishi Mfalme kutangaza crusade na kutoa tangazo kwamba waislam wote wawe wakatoliki lasivyo waondoke katika nchi hiyo mpaka kufikia siku ya pili la sivyo watauawa

Hata kanisa kathedo kubwa ya hispania ilikuwa ni mmoja ya misikiti mikubwa barani ulaya

Stori hii siikumbuki vizuri lakini ndio ipo hivyo
 
Asante mkuu, hata msikiti mkubwa Uturuki ulikuwa Cathedral
 
Duh naweza kukubaliana na jibu lako hili lakini je kwanini iwe wakati wa kwenda kuifuta Roma?? Kwanini kijana asingesubiri baba yake amalize ulaya nzima ili hata akija kutawala asipate upinzani kipindi akipata madaraka ?
Haya maswali ni magumu kigogo, unakumbuka ile midege iliyoteketea pale Misri masaa machache kabla ya kuruka kwenda kuharibu nchi jirani?
 
Mehmet hakujua kuwa wabunifu wa dini yake ya kiislam ni vaticani kwa lengo la kuua ukristo wa kweli,lakina sio kuua mamlaka ya upapa.dini ya kiislamu iliazinshwa kwa siri na kanisa la roman catholic kwa kuwatumia jesuits na Khadija mama mjane tajiri kwa wakati huo amabae alilirisha kanisa mali zake zote na akaolewa na mtume Muhamad.
lengo la jesuits ililikuwa kuua ukristo uliokuwa umeshamiri ulaya mashariki mpaka mashariki ya kati na Afrika kaskazin.
siri wanayo viongozi wa juu wa dini hizo,ndio maana ukatoriki na uislam una vitu vinafanana,na uislam unaukosoa mno ukatoriki zaidi kuliko ukristo kwa ujumla.mengi yanayokosolewa msingi wake ni mapokeo ya kipagani ya kanisa la katoliki
Mkuu uislamu umeanza lini na Jesuit imeanzishwa lini???
 
2. Nimeipenda hiyo namba 2 asee so uko deep kwenye mambo ya ancient egypt..... Next tym shusha thread basi ya dynasty za kipindi hicho kuanzia kina Pharaoh thutmose na kina Akhenaten maana nayo egypt ina golden history sana
Egypt ni moja ya sehemu zenye historia muhimu sana kuzijua
 
Back
Top Bottom