Nini kilisababisha urafiki na Besti/ Mshkaji wako kufa?

πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Alikuwa haeleweki. Mtu hana malengo ya kimaisha yeye ni bata tu umri umeenda bado ana akili kama yupo foolish age.

Anaweza pata laki 5 hapa akapigia simu washkaji ikachakazwa ikaisha yote akaamka asubuhi ana 30,000 tu.

Ukiwa na shida ukimwambia anataka ujielezee kama unaomba mkopo wakati yeye akiwa na shida hata simuulizi nampa kile anachoomba.

Alikuwa anatabia anakuja na gari yake anaipaki anaomba yangu aendee mtaa wa nyuma sababu anasema yake ipo chini sana halafu inatoa mlio hauelewi ila nikajua anafanya kusudi tu ila nikawa nampa tu ufunguo afanye anachotaka sijui alikuwa anaenda gongea mademu zake kwenye gari. Maana anaweza ondoka saa kumi na moja jioni anarudi saa tano au saa nne za usiku. Nikamwambia nataka nisepe gari ipo wapi ananiambia niende na yake atakuja home kuichukua me huwa namkatalia namwambia niambie ulipo unikuletee gari yako me naenda home basi hapo ataogopa utashangaa huyo hapo baada ya nusu saa.

Nilipopitia kipindi kigumu kidogo ndipo nikajua tabia zake halisi. Kwanza alikata mguu, simu zangu akawa hapokei, nishamuomba sana hizi hela ndogo ndogo hajawahi nitoa hata 10. Kuna siku mshikaji wetu mwingine akasema mbona jana nilikuwa na fulani nikamwambia nikupigie simu uje akasema nisikuite, mnashida gani? Nikatabasamu tu na kutikisa kichwa nikamwambia acha tu ubinadamu kazi ndugu yangu. Nikamuelezea jamaa akasikitika sana na yeye akaanza muepuka. Akawa akienda kiwanja ananipigia ananitumia boda boda tunaenda kula bata kimya kimya.

Kuna siku akatukuta kwa bahati mbaya kiwanja kinaitwa small planet pale tabata. Akawa ananionyesha sura ya dharau kabisa yaani utasema kuna kitu nimemfanyia, aisee nilipatwa na hasira nusu nimfyatukie sema nikajikaza. Akaondoka na demu alikutana nae pale pale akaenda zake.

Fast-forward leo mimi niliendelea jikongoja nikakaa sawa hali si mbaya, aliniona wapi sijui naendesha gari ya mshikaji wangu mwingine akajua sijui yangu nashangaa simu ananipigia ananichangamkia sana. Nikajisemea "ona jinga hili".

Akawa anataka sana tuonane namkwepa hadi leo. Nasubiria kwa hamu sana nipate usafiri wangu tena nitahakikisha anajua halafu ajaribu kuniletea mazoea aisee ntamlipua dry na nitampa makavu yote hadi ajue kuwa kazingua.
 
Yakutunga wapi huo ndio ukweli wako rafiki mnafkiπŸ˜‚
 
Nilikosana na rafiki yangu kipenzi,kwa sababu ya kutembea na mpenzi wangu
 
Niliona text kala shoga
 
Duuu nsamehe mwanangu kwaiyo umeamua uje unichome huku?
 
Huyu kama sio nshomile basi anatokea ujitani wengi wapo hivi hivi
 
Mwanangu umejuaje? [emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]

Jamaa ni muhaya kwa baba na mama wote ni wahaya.

Dah aiseee basi nimeamini kuna tabia ni common na jamii fulani tu ya watu.
Nawajua nje ndani wana mazuri yao ila roho mbaya km hiyo ni dosari yao kubwa sana hawapendi uwe juu kumzidi hata akiwa ndg yake wapo hivyo,

wengi wao wapo hivyo
 
bora umekua mkweliπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
My best friend ni mmoja tu since class 3 primary mpaka leo hatujawahi gombana kwa lolote
 
1πŸ˜€eni,nilimkopesha fedha ndefu ili alipe mahakamani alikokua na kesi ya madai sikuwahi kulipwa pesa yangu mpaka leo
2:Usaliti,kuna fala mmoja nilikua karibu nae sana ila ndo hivyo tena alikua na tabia ya kutongoza mademu ziangu(akiwa anajua kabisa)then baada ya mimi kuoa akaanza mazoea yaliyopitiliza kwa mrs,baada ya hapo ushikaji ukafa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…