Nini kiliua safari za moja kwa moja za mashirika ya ndege ya Ulaya kama Scandinavian Airlines na Lufthansa?

Mambo vp jamiiforums.

Nini kiliua safari za moja kwa moja (Direct Flight) za kuja Tanzania kwa mashirika ya ndege ya Ulaya kama Scandinavian Airlines System (SAS) pamoja na Lufthansa ya Ujerumani? Mbona mkongwe mwenzao KLM bado anakujaga?
==========
View attachment 1727879
==========
Jana nikiwa nimepaki gari yangu (Taxi Bubu) hapa kijiweni nilipigiwa simu kwenda kuchukua abiria mmoja pale uwanja wa ndege wa mwalimu Nyerere (JNIA) alikuwa anatokea hukoooo majuu.

Sasa wakati ninasoma vijarida kadhaa pamoja na kupiga stories na abiria pamoja na ndugu waliokuja kupokea wenzako pale sehemu ya kusubiria, nikajifunza mambo yafuatayo.

Kuna njia mbili tu za moja kwa moja kutoka Ulaya hadi Tanzania kwa njia ya ndege. Kwanza kuna KLM (Royal Dutch Airlines) ambayo huruka kila siku kuja Dar es Salaam kutoka Amsterdam nchini Uholanzi.

View attachment 1727881

Njia ya pili ni kupitia shirika la ndege la Uturuki kutoka Istanbul uwanja wa ndege wa Ataturk. Vinginevyo wasafiri kutoka Ulaya wanaweza kupanda ndege kwenda Nairobi. Halafu Kenya Airways inakujaga karibia kila siku huku Dar/Tanzania.

Mashirika yanayokwenda Nairobi ni pamoja na British Airways kutoka London Heathrow; Air France kutoka Paris; Swiss Air kutoka Zurich; Brussels Airlines kutoka Brussels nchini Ubelgiji; Lufthansa kutoka Frankfurt; na Kenya Airways kutoka London Heathrow au Amsterdam.

Kwa ujumla, Shirika la Ndege la Kenya huchukua chini ya masaa tisa usiku mzima kutoka London hadi Nairobi, ambayo inaunganisha kufika Dar es Salaam.

Ikiwa unataka kuja Dar es Salaam, basi vinginevyo unaweza kuunganisha kupitia Cairo na Egypt Air; kupitia Dubai na Emirates; kupitia Abu Dhabi na Etihad Airways; kupitia Addis Ababa na Shirika la ndege la Ethiopia.

View attachment 1727882

Pia abiria anaweza kupitia Muscat na Oman Air; au kupitia Doha na Qatar Airways. Baadhi ya mashirika haya ya ndege pia yana njia zinazoingia Kilimanjaro na Zanzibar.

SWALI LANGU: Nini kiliua safari za moja kwa moja (Direct Flights) za mashirika ya ndege ya Ulaya kama kama Scandinavian Airlines (SAS) pamoja na Lufthansa ya Ujerumani? Mbona mkongwe KLM bado anakuja Tanzania?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Watanzania wasiokua na uzalendo kwa kushirikiana na kenya walifanya hiyo kitu ili kuufanya uwanja wa ndege wa jomo kenyata uwe busy na hapo kenya itumie nafasi hiyo kukuza shirika lao la ndege
 
Landing fee ni kubwa sana.. Fikiria Turkish airlines inatua KIA inakaa masaa mawili wanalipishwa hela nyingi sana..
Wanachofanya kupitia agents wao wa Arusha na Kilimanjaro ni kuconnect abiria wapandie Jomo Kenyatta JKIA..
Mpaka serikali ije kustuka labda mwaka 2090
 
Unajua ni kwanini Rais Samia anamshinda Tundu Lissu? Ni kwa sababu yule kiwete wa Ubelgiji hana jipya na watanzania wamechoka kelele zake
 
Mara nyingi ndege uvunja route kama inaonekana hakuna abiria wa kutosha kwenye hiyo route. Baada ya vulu-vulu zilizotokea hapa katikati hatuna uwekezaji mkubwa kutoka Ulaya na sisi kiwango cha biashara tunachofanya nao ni kdogo sana hivyo kuto-attract movement kubwa ya vitu na watu.

Hapa Tanzania ni watu wachache wanaweza ku-afford products za Ulaya, wengi tunajisalimisha kweye mediocre stuff from Asia. Wazungu wa Ulaya wanaokuja huku sanasana ni utalii ambao pia kwenye destination hiyo bado tunajikongoja, ingawaje Zanzibar wanafanya vizuri ku-attract Wazungu wa Ulaya.
Sawa mkuu
 
Mambo vp jamiiforums.

Nini kiliua safari za moja kwa moja (Direct Flight) za kuja Tanzania kwa mashirika ya ndege ya Ulaya kama Scandinavian Airlines System (SAS) pamoja na Lufthansa ya Ujerumani? Mbona mkongwe mwenzao KLM bado anakujaga?
==========
View attachment 1727879
==========
Jana nikiwa nimepaki gari yangu (Taxi Bubu) hapa kijiweni nilipigiwa simu kwenda kuchukua abiria mmoja pale uwanja wa ndege wa mwalimu Nyerere (JNIA) alikuwa anatokea hukoooo majuu.

Sasa wakati ninasoma vijarida kadhaa pamoja na kupiga stories na abiria pamoja na ndugu waliokuja kupokea wenzako pale sehemu ya kusubiria, nikajifunza mambo yafuatayo.

Kuna njia mbili tu za moja kwa moja kutoka Ulaya hadi Tanzania kwa njia ya ndege. Kwanza kuna KLM (Royal Dutch Airlines) ambayo huruka kila siku kuja Dar es Salaam kutoka Amsterdam nchini Uholanzi.

View attachment 1727881

Njia ya pili ni kupitia shirika la ndege la Uturuki kutoka Istanbul uwanja wa ndege wa Ataturk. Vinginevyo wasafiri kutoka Ulaya wanaweza kupanda ndege kwenda Nairobi. Halafu Kenya Airways inakujaga karibia kila siku huku Dar/Tanzania.

Mashirika yanayokwenda Nairobi ni pamoja na British Airways kutoka London Heathrow; Air France kutoka Paris; Swiss Air kutoka Zurich; Brussels Airlines kutoka Brussels nchini Ubelgiji; Lufthansa kutoka Frankfurt; na Kenya Airways kutoka London Heathrow au Amsterdam.

Kwa ujumla, Shirika la Ndege la Kenya huchukua chini ya masaa tisa usiku mzima kutoka London hadi Nairobi, ambayo inaunganisha kufika Dar es Salaam.

Ikiwa unataka kuja Dar es Salaam, basi vinginevyo unaweza kuunganisha kupitia Cairo na Egypt Air; kupitia Dubai na Emirates; kupitia Abu Dhabi na Etihad Airways; kupitia Addis Ababa na Shirika la ndege la Ethiopia.

View attachment 1727882

Pia abiria anaweza kupitia Muscat na Oman Air; au kupitia Doha na Qatar Airways. Baadhi ya mashirika haya ya ndege pia yana njia zinazoingia Kilimanjaro na Zanzibar.

SWALI LANGU: Nini kiliua safari za moja kwa moja (Direct Flights) za mashirika ya ndege ya Ulaya kama kama Scandinavian Airlines (SAS) pamoja na Lufthansa ya Ujerumani? Mbona mkongwe KLM bado anakuja Tanzania?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Swiss (sio Ulaya)?
 
Back
Top Bottom