Nini kiliua safari za moja kwa moja za mashirika ya ndege ya Ulaya kama Scandinavian Airlines na Lufthansa?

Nini kiliua safari za moja kwa moja za mashirika ya ndege ya Ulaya kama Scandinavian Airlines na Lufthansa?

Pia walikuwa wanatuletea madege ya zamani.

Waarabu walipokuja wakawa wanaleta ndege mpya kwa kuwa yalikuwa ni mashirika mapya. Mashirika ya ulaya yakashindwa kushindana, huku wakilalamika ndege za waarabu zinashindana unfairly kwa kuwa wanapata mafuta bure kutoka serikali zao.
Madege ya zamani [emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ni orodha ya mashirika yaliyokuwa yanatua Dar na sasa yameacha:
1. PIA (Pakistani International Airlines)
2. SAS (Scandivian Airline Systems)
3. Luthfansa
4. British Airways
5. Aeroflot (Mrusi)
6. Air France (ilikuwa inakuja ile Boeng 747 yenye kigorofa)
7. Gulf Air (Bahrain)
9.
10.
SABENA ni aje
 
Mambo vp jamiiforums.

Nini kiliua safari za moja kwa moja (Direct Flight) za kuja Tanzania kwa mashirika ya ndege ya Ulaya kama Scandinavian Airlines System (SAS) pamoja na Lufthansa ya Ujerumani? Mbona mkongwe mwenzao KLM bado anakujaga?
==========
View attachment 1727879
==========
Jana nikiwa nimepaki gari yangu (Taxi Bubu) hapa kijiweni nilipigiwa simu kwenda kuchukua abiria mmoja pale uwanja wa ndege wa mwalimu Nyerere (JNIA) alikuwa anatokea hukoooo majuu.

Sasa wakati ninasoma vijarida kadhaa pamoja na kupiga stories na abiria pamoja na ndugu waliokuja kupokea wenzako pale sehemu ya kusubiria, nikajifunza mambo yafuatayo.

Kuna njia mbili tu za moja kwa moja kutoka Ulaya hadi Tanzania kwa njia ya ndege. Kwanza kuna KLM (Royal Dutch Airlines) ambayo huruka kila siku kuja Dar es Salaam kutoka Amsterdam nchini Uholanzi.

View attachment 1727881

Njia ya pili ni kupitia shirika la ndege la Uturuki kutoka Istanbul uwanja wa ndege wa Ataturk. Vinginevyo wasafiri kutoka Ulaya wanaweza kupanda ndege kwenda Nairobi. Halafu Kenya Airways inakujaga karibia kila siku huku Dar/Tanzania.

Mashirika yanayokwenda Nairobi ni pamoja na British Airways kutoka London Heathrow; Air France kutoka Paris; Swiss Air kutoka Zurich; Brussels Airlines kutoka Brussels nchini Ubelgiji; Lufthansa kutoka Frankfurt; na Kenya Airways kutoka London Heathrow au Amsterdam.

Kwa ujumla, Shirika la Ndege la Kenya huchukua chini ya masaa tisa usiku mzima kutoka London hadi Nairobi, ambayo inaunganisha kufika Dar es Salaam.

Ikiwa unataka kuja Dar es Salaam, basi vinginevyo unaweza kuunganisha kupitia Cairo na Egypt Air; kupitia Dubai na Emirates; kupitia Abu Dhabi na Etihad Airways; kupitia Addis Ababa na Shirika la ndege la Ethiopia.

View attachment 1727882

Pia abiria anaweza kupitia Muscat na Oman Air; au kupitia Doha na Qatar Airways. Baadhi ya mashirika haya ya ndege pia yana njia zinazoingia Kilimanjaro na Zanzibar.

SWALI LANGU: Nini kiliua safari za moja kwa moja (Direct Flights) za mashirika ya ndege ya Ulaya kama kama Scandinavian Airlines (SAS) pamoja na Lufthansa ya Ujerumani? Mbona mkongwe KLM bado anakuja Tanzania?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Huu uzi wako uliuanzisha siku muhimu sana!
 
Unfortunately kuvunja uhusiano huwa ni rahisi sana lakini kuujenga upya ni kugumu sana.

Uzuri wa uwanja kwa macho ya mashirika ya ndege siyo ule uzuri wa majengo ya terminal, wao wanaangalia mambo kama usalama wa ndege zao na huduma ambazo ndege zao zinapata zinapokuwa pale airport. Mambo hayo hayaletwi na ufunguzi wa jengo la terminal 3. Sababu kubwa ya Lufthansa kusitisha safari zake ilikuwa ni kuwa kuna wakati walikuwa wan-land usiku (alfajiri sana) huku hakuna taa za kutosha uwanjani. Uwanja utakamilika tu utakapokuwa na taa za kutosha na vile vile kuwa na automatic landing system (ALS) infrastructure!!
Kwa umeme upi?
 
Hii ni orodha ya mashirika yaliyokuwa yanatua Dar na sasa yameacha:
1. PIA (Pakistani International Airlines)
2. SAS (Scandivian Airline Systems)
3. Luthfansa
4. British Airways
5. Aeroflot (Mrusi)
6. Air France (ilikuwa inakuja ile Boeng 747 yenye kigorofa)
7. Gulf Air (Bahrain)
9.
10.
9. Air Zanzibar
10. Air Pemba
 
France Air anategemea kuridisha Route ya kutoka Paris Direct to Dar, Kwasasa France Air ameungana na KLM wanafanya kazi kwa pamoja.

Hata ivyo ndege nyingi zinategemewa kuleta safari zake hapa Dar Es Salaam mwishoni mwa mwaka huu mpaka mwakani..

Hapa juzi mwezi wa 4 Saudi Arabia kaanzisha Route yake kuja Dar na anaendele kufanya vizuri katika Soko.
 
Back
Top Bottom