Nini kimeiua CHADEMA? Walikosea wapi? Vyama vingine vya upinzani vijifunze kuepuka kibri cha kupendwa


Chama sio mali ya umma acha uongo, chama ni mali ya wanachama. Wanachama ndio huamua chama kiendeje.

Unafiki ni kutetea CCM kukaa madarakani kwa muda wote huo kupitia wizi wa tume ya mahera lakini kukasirika wanachama wa Chadema kuchaguwa mwenyekiti wao kwa muda.

Hiyo ni mbinu pia ya kupambana na mitego ya ccm . Ona kundi la Zitto lililotaka kuiongoza CHADEMA kipindi hicho lipo wapi? Wote wanerudi CCM. Hivi unadhani Zitto angechaguliwa mwenyekiti wa chadema kipindi kile mambo yangekuwaje?
 
Mi pale ndio nikavua gwanda na zote nikazigawa. Nikaona kwa sasa nitakuwa naangalia mtu mwenye uwezo na maono nitamsapoti. Awe wa ccm, CUF, ACT, CHAUMA au Chadema.

Na nikapata nafasi nzuri ya kumsapoti Magu na sio CCM.

Kwa sasa nipo nipo tu. Sisapoti yoyote na sijajua kama 2025 nitapiga kura.
 
Nani kataka kumaliza upinzani? Usije kuwa wewe unajiita upinzani ndiye hutaki kusikia upinzani, maana hutaki kusikia kuwa
vyama vya upinzani ni vya kihuni na kidikteta.

Vyama vya upinzani vilimfanyia nani udikteta?. Kwenye kugombea uenyekiti wagombea ni zaidi ya mmoja na kwenye kugombea urais mgombea ni zaidi ya mmoja, shida ipo wapi?

Kwa CCM mgombea uenyekiti ni mmoja tu na hakuna mwingine na kwenye awamu ya pili mgombea urais ni mmoja tu. Membe alitaka kugombea urais akanyofolewa uanachama.

Anza kwanza na CCM ndio uje upinzani. Ndoa yako kila siku magomvi, ila kutwa kusema ndoa za wengine.
 
Yaani wewe ni [emoji706][emoji706][emoji706]sana. Mtu anapiga risasi wapinzani na kuwafunga jela, anapiga marufuku mikutano ya kisiasa halaf unasema chadema imekufa! Idiot!
Ukitaka maendeleo ya kweli hakikisha umenyamazisha wapinzani wako.

Wapinzani wapo kwa ajili ya kupewa asali tena kila wanapotaka. Siku ukiwanyima wanakuchafua na watasema ulikuwaga unawapa asali kuwafunga mdomo.
 
Chadema bado kipo sana na kitaendelea kuwepo.
The funny shit ni kwamba aliyetumia nguvu nyingi na kila ya recourses kukiua amekufa yeye na Chadema kiko hai.

Mkuu ili jambo watu wengi wanajifanya kulipotezea, ila kuna fundisho nyuma yake. Mimi nilimchukia magufuli moja kwa moja baada ya ule uchaguzi wa 2020.

Nchi zingine ubunge wanawaachia wananchi waamue kwenye urais ndio wanaiba. Yeye kaiba kila kitu kuanzia uwenyeviti, udiwani ,ubunge na urais. Lakini akafa ndani ya miezi minne baada ya wizi
 
Kwanini mnakuwa na hasira hebu weka point tano tu kwanini niwachague Chadema? wana nini wanataka kutu offer mimi kama mwananchi wa kawaida tu, vitu vitano tu

Vitu vitano?. Hivyo vitu vitano kawaambie CCM waliopo madarakani.
 
Mwana uchumi kweli unaamini kabisa Chadema wanaweza kutawala? Chadema kama mchezaji mpira kwenda Kagera au Mtibwa kutengeneza jina akipata ndoto kwenda Simba au Yanga. Akikosa huko ndio utamkuta Lindi au Singida united.

Kwanini chadema wasiweze?. Mwaka 2015 walipata asilimia 40 ya kura za urais, ina maana walibakia asilimia 10 tu wafikishe 50. Hivi chama chenye margin ya asilimia 10, hakiwezi kupewa madaraka?. Yani pamoja na tume ya uchaguzi kuwa ya rais na upendeleo kuwa wa wazi, bado chadema ilifanikiwa kuzoa asilimia 40.

Hivi fikiria kwanini mwaka 2020 mizengwe ilikuwa mingi dhidi ya chadema? Issue ni kwamba ukiachia chadema nafasi ikafanya siasa kwa uhuru , tume huru hakuna kubambikiana kesi, utakuja kuniambia. Mazingira ya sasa yana ifavour CCM sana.
 
Wamejiua wenyewe kwa tamaa zao
  1. Mbowe
  2. Lissu
  3. Lema
  4. Msigwa
  5. Mnyika
Walisimama majukwaani kusema Lowasa fisadi papa, ndimi hizohizo zikaja kusema Lowasa safiiiii👍🤣

View attachment 2480444
Utamwamini mtu wa hivi?
Utamuelewa?

Kwa hivyo Lissu na mbowe ni mahakama? Lazima uelewe wale ni wanasiasa, na siasa ni dynamic. Alikuwa fisadi au hakuwa fisadi, hilo sio issue, ila cha muhimu Lowassa na Chadema walimpa headache magufuli mpaka kufuta mikutano ya hadhara.
 
Umma maana yeke watu wengi. Ndiyo maana kuna umma wa waislamu nk. Kitu kama hicho hakiwezi kuendeshwa kwa kidikteta kampuni ya mtu binafsi. Ikitokea kimeendeshwa kwa udikteta basi ni makosa. Zitto angepata uenyekiti chama kingeweza kuwa vizuri kuliko kilivyo sasa. Ni unafiki mkubwa kuona ubaya wa udikteta wanapofanya wengine na kushangilia unapofanya wewe.
 
Hao unaosema wamekuwa na mgombea mmoja wamebadilisha wenyeviti mara nne ndani ya miaka 20. Vyama vya upinzani vipo na watu walewale, Mbatia, Lipumba, Mbowe, Mrema nk nk. Wenyeviti wa vyama vya siasa vya upinzani ni madikteta wakubwa. Bahati mbaya wafuasi wao wamejaa mahaba kiasi kwamba hawaoni udikteta huo. Lazima kuwe na ukomo wa mtu kuongoza, tofauti na hapo ni kuanzisha mazalia ya madikteta.
 
Kelele nyingi, huyo Lowassa si yupo CCM mbona hamjamshtaki? Na mmempa mwanae ubunge?.

Chadema walipata kura milioni sita na wabunge wa kutosha. Hilo kwenye siasa ndilo la maana. Mbona magufuli alikuwa na kashfa ya ufisadi ya kuuza nyumba za serikali kwa hawala yake?. Lakini akateuliwa kuwa rais?. Lowassa alikuwa anaenda kutoa shukrani mpanda baada ya uchaguzi akakamatwa na polisi na mikutano ikazuiliwa.
 
Una chuki na Mbowe na si vinginevyo,ukweli uko pale pale CHADEMA haijafa na haiwezi kufa kwa mawazo yako.
 
Magufuli alitaka kuua CHADEMA lakini alikufa yeye tarehe 17/03/21. Yule kichaa alipopewa madaraka ya kuwa Rais October 2015 akapagawa akajiona yeye ni mungu.

Akataka kumuua Lissu na kumzika Ikungi chapchap tarehe 17/09/2017 baada ya kumshambuliankwa risasi, lakini Mungu wetu aliyejuu akasema wewe ni nani mpaka uamue nani Aishi na nani afe. Mwishowe akafa mwenyewe.

Usijidanganye kuwa CHADEMA imekufa hata kwa 1%, instead nakuhakikishia CHADEMA imekuzwa na vitendo viovu vya magufuli pengine kwa 300%
 
Ukitaka maendeleo ya kweli hakikisha umenyamazisha wapinzani wako.

Wapinzani wapo kwa ajili ya kupewa asali tena kila wanapotaka. Siku ukiwanyima wanakuchafua na watasema ulikuwaga unawapa asali kuwafunga mdomo.

Upinzani ni hoja pana sana. Tatizo tunadhani upinzani ni CHADEMA tu. Kipindi cha Nyerere alinusurika mara mbili kupinduliwa na ulikuwa mfumo wa chama kimoja. Nyie bakieni kudhani Upinzani ni mbowe na Lissu.

Magufuli alidhani wapinzani wake ni chadema, lakini kipindi anakufa chadema ndio walipaza sauti kuhusu kifo chake mpaka ilipotangazwa rasmi.
 
Dr Slaa huyu huyu zuzu asiyejielewa? Angekuwa na msima walau 10% ya Mbowe angalau angekuwa 'mtu', mtu kadindisha kuunga mkono 'juhudi' licha ya kuharibiwa na kufilisiwa investments kibao unadhani ni wangapi wanaliweza hilo.
Lowassa businesses zake zimeguswa kidogo tu kaufyata na kurudi tena akapokelewa kwa bashasha ikulu Jiwe akiuhesabu kuwa ni ushindi wa ndugu.
 
Mali
Nimekuambia umma ni jumla ya jamii yote, lakini wanachama ni specific. Ndio maana mambo ya CCM yanawahusu wanachama wa CCM pekee. Sasa kulazimisha maamuzi ya CHADEMA kuwa ya watanzania wote unakosea sana. Wanaotakiwa kulalamika ni wanachama wa chadema sio wengine.

Zitto yupi? Huyu aliye ambulia kura za urais elfu tisini nch nzima mwaka 2015? Kipindi hicho ACT ipo hot kabisa. Mwaka 2020 wakashindwa hata kumcontrol mgombea wao wa urais?. Kama Zitto kashindwa kukiamsha chama kipya kama ACT angeweza kwa CHADEMA?. Yupo wapi msando, Dr Kitila, Pamba, et al?. Wote walirudi CCM. Sasa jiulize walitaka kuiongoza chadema kwanini kama ACT iliwashinda.
 
Haya mikutano mmeruhusiwa tuone kama mtashindaa
 
Zitto au Slaa wangefanikiwa kuongoza CDM leo hii kingeshageuka na kuwa tawi la CCM na kisingekuwa kinapigiwa kelele na supporters wa CCM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…