Nini kimemkuta Waziri wa zamani na Wakili Msomi, Lawrence Masha hadi kufika kwa “Kiboko ya Wachawi”?

Kwanini umeshangaa sasa? Inamaana kwakua ni msomi hapaswi kuabudu?

Anyway, but jana kuna pahala nilisema, haya maswala ya imani huwa hayaeleweki sana na watu ambao wako stable kimaisha yaani watu ambao hawajapungukiwa na chochote but once masahibu yanapokuchapa kisawa sawa basi usipoangukia kwa waganga lazima utaangukia kwenye hayo makanisa ya kiroho.

Kila anaemtafuta Mungu, jua ako na historia za tofauti na ngumu sana na mambo ya hapa duniani hasa ukiachana na wale ambao wamezaliwa kwenye misingi hiyo ya kiimani.
 
Ni upumbavu wa Watanzania! Halafu huwa kuna hohehahe mmoja humo kanisani huwa anaropoka kwa nguvu aminaaaa! Ananiudhi sana! Masha anajikabidhi kwa shetani!
 
kwa mtu aliyewahi fika peak ya mafanikio yake then ukafuata mdororo full msoto hawezi mshangaa Masha. Mpambanaji sasa haelewi ashike lipi, hapo kila mmoja na ushauri wake. Ila ipo siku atatoboa tu, japo inaweza isiwe namna alivyokuwa kabla, ila umri bado unamruhusu kufanya makubwa na kuishi vizuri.
 
Haya siyo maigizo kweli!!
 
Majibu....

1. Ni Mmoja wa Mfadhili wa huyo Tapeli wakiwemo na Wateule Wanne wa Mama yenu katika Serikali hii
2. Hapa anamtafutia Soko zaidi kwakuwa anajua Watu wengi watavutika kwenda kwa huyo Tapeli wakisikia nae kaenda
3. Ni mkakati Maalum wa Kutuhamisha Watanzania hasa Kimatukio kwakuwa wanajua tunapenda Matukio

Kila la Kheri.....!!
 
Malipo Ni hapa hapa.
Imagine mtu aliyekua mkurugenzi Tanga cement na kumiliki shirika la ndege Leo anakwenda kwa waganga buza.
Karma is real.
Tembo hata akonde vipi hawezi kuwa kama sungura
Jamaa anaweza kuwa ametumia hiyo stage kumkaanga mkewe si unaona alivyo panda kibabe hapo 😄 polo tshirt na jeans hana habari
 
Okay
 
Kwa video hiyo, nilikuwa nimeanza kuingia kwenye reli ya kumuamini bwana nabii, kiboko ya uchawi... Mpaka hapo mwishoni aliposema kuwa kumbe wamekwishazungumza ofisini.... Nilijua hawajuani na hawajaonana kabisa... Tunapigwa mazee, tunapigwa!!
Toka mwanzo tu unajua tu nabii alikua na info za kutosha kumhusu jamaa.

Na usomi wake anapigwa kijinga ivo, ila kwa muonekano wa sura tu anaonekana ana stress sana, uso umesawajika mno.
Watoto wake watakua wanajisikiaje kuona baba akimiminiwa futa na nabii uchwara.
 
Mapito ya kimaisha tu......
 

G7 ya Rose Garden baadae 777, imesambaratika na wengi wameenda nayo kama walivyotengeneza. Nafikiri ilikuwa kama mbeba chuma anayefanya mazoezi ya kujaza kifua na kuacha miguu ikikondeana kama fito za kujengea nyumba ya nyasi.
Teke lilipokuja, ni kuanguka. Si Masha peke yake, bali kundi zima ni kama limepotelea mbali. Wengi hawaeleweki kabisa.
Kweli maisha ni safari, ila tunavuna tunayopanda. hakuna mchawi ila tunajiroga wenyewe. Mtu mwenye akili zake anayeenda kupiga ramli chonganishi anajidharaulisha na kuwa kituko.
Sasa naamini IMMA ilijengwa kimkakati na kuna uwezekano ilikuwa zaidi ya kampuni ya kisheria. Muda unazidi kusema yote. Kuanzia zile enzi za kashfa ya Meremeta, kuna maswali mengi hayakuwa na majibu.
Pole sana Lau. Pambana urudi kwenye mstari. Usiende kumsumbua mkeo eti anakuroga kumbe mchawi mwenyewe
 
Ni mataokeo ya Magufuli kutaka kuuwa mashirikia mengine ya ndege ikwapo Fastjet na Precision Air. Alifanikiwa kuuwa Fastjet ambayo Masha alikuwa mdau mkubwa nadhani hiyo ndio imempiga shoti Masha kutamani kufa kabisa kuliko kuishi.

JPM ametangulia mbele ya haki miaka mitatu sasa. Ina maana hana namna ya kuweka mambo sawa mpaka leo? Basi sio mfanya biashara. Mbona alianzisha law firm nyingine nayo haieleweki?
 
Halafu mafuta yenyewe yamèchanganywa na mafuta ya maiti! Aibu sana Watanzania!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…