Nini kimetokea mpaka kufa kwa uzalishaji wa Ngano hecta 350,000 kule Bassotu Manyara?

Hakuna 10% huko hahaha

Ova
 
Huku kudanganyana. Toka lini serikali ikawa mnunuzi wa ngano?

Viwanda vinaagiza ngano nje si vingepata unafuu sana. Labda huyo ngano yake haikukidhi vigezo vya wasagaji wa ngano, mfano Azam.
Uko sahihi Faizafoxy, Sio kweli hapa katudanganya, Serikali si mnunuzi wa ngano. Hii itakuwa ni changamsha baraza, Wanunuzi wakubwa wa ngano ni viwanda kama Bakhresa, Mo n.k unless ngano hiyo haikwa na vigezo kwahoyo mzalishaji alitegemea aiuzie Serikali, huu nao ni upigaji wa aina yake.
 
Umeongea point sana. Tatizo lilianzia kwenye Azimio la Arusha la kutaifisha mali za wawekezaji bila kutafakari kama serikali wataweza kuziendeleza. Mwisho wa siku walitaifisha wakashindwa kuendeleza changanya na ubunifu mdogo mabadiliko ya teknolojia halafu na kukumbatia sera za kijamaa bila kujiandaa na ujamaa wenyewe hali iliyofanya mabeberu kukasirika na kutupiga vikwazo vya kiuchumi hali iliyosababisha kushindwa kupata spear za mitambo au kushindwa kabisa kununua mitambo mipya na mwisho wa siku viwanda vikafa kabisa na viwanda vikifa na mashamba nayo yanakufa.

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
 
Wakulaumiwa wa kwanza ni aliyeleta sera ya utaifishaji na Ujamaa uchwara.

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
 
Hilo la "kumtongozea mtu" lina sound tam sana, lianzishie page yake[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]!
 
SUA wangetumia fursa hiyo
 

tuache kuilaumu CCM sasa...tutafute tatizo la msingi na wote kwa pamoja tupambane kuliondoa...umaisikini unanuka kila mahala Africa, shida utagundua ni common kwa waAfric wote na ndio hiyo umeionyesha hapo..

umeongea point kubwa sana, madhara ya ukoloni ndio mateso ya Mwafrica mpaka leo.. baada ya ukoloni Mwafrica alishindwa kujua anataka nini na matokeo yake mkoloni akaja tena na aina nyingine ya ukoloni..
 
Power nyingine Mkoloni aliyotumia na bado anaitumia ni elimu na technology. Wakati mkoloni anatutawala alitumia kilimo cha kisasa kulima mashamba, pamoja na kutumia Rasilimali watu kwa ujira mdogo pia alitumia mashine za kisasa kwa wakati ule.

Alifanya tafiti nyingi na kupata matokeo. Leo hii huko London na Berlin wanajua sehemu zote zenye madini Tanzania. Wanaweza kupanga mbinu yeyote ya kuyapata wakati sisi hatujui kinacho endelea.
 
Pale Muhimbili na mahospitali mengi tuu nchini ukiweza kuzunguka huko nyuma ya majengo yao utakuta lundo la vitanda vibovu, viti na vifaa chungu nzima ambavyo kiukweli wangekuwa na karakana ndogo tuu na mafundi wawili wangevirepea vyote na vikaendelea kutumika. Nenda kwenye mashule uone madawati yaliyotupwa na ambayo yangerepewa yangetumika. Nenda kwenye ofisi za serikali uone magari mabovu yanavyoachwa mpaka yanashika kutu.. [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 

elimu,teknolojia ongeza na utamaduni....hivi vyote kwa sasa ndio tools kubwa inayotumika kumfanya Mwafrica kuwa mtumwa bado...

Huu mtego mpaka sasa hakuna dalili za kuukwepa..
 
elimu,teknolojia ongeza na utamaduni....hivi vyote kwa sasa ndio tools kubwa inayotumika kumfanya Mwafrica kuwa mtumwa bado...

Huu mtego mpaka sasa hakuna dalili za kuukwepa..
Utamaduni wa Wazungu ni kufanya kazi, ubepari umelenga kuhakikisha kila mtu anafanya kazi. Baada ya WWII Mfalme wa Holland alifungua kiwanda cha kutengeneza vitenge ili vijana wapate kazi.

Soko la vitenge limelengwa Africa, usishangae kufa kwa viwanda vya Mwatex na Sungura Tex, fitina ya soko la vitenge ni kubwa na jamaa wanafanya uchunguzi na propaganda nyingi.

Tungekuwa imara sisi Tanzania tungengeneza vitenge kwa East na South Afrika kutokana na pamba tunayolima.
 
nilijaribu kuuliza kuhusu ile ngano ya kutengeneza bia, jibu lilikuwa ni baada ubinafsishaji wa viwanda vya bia wale wawekezaji walitoa sharti la kutumia ya kutoka s.Africa story ikaishia hapo.
Lakini kuna tatizo kubwa katika taifa hili sio ngano peke yake kuna kahawa, katani,korosho, pamba yote yamebaki historia tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…