Nini kina sababisha siku za hedhi kupitiliza kama huna mimba?

Wakuu;
Heshima mbele.. Naomba kumuuliza anayefahamu.. Ni kawaida kwa binti kupitiliza siku zake (menstrual cycle) mpaka siku 10+.. Kwa mtu ambae ofcoz siku hubadilika kwa +5 au +4.. ??

Au yaweza kuwa dalili ya mimba?? Lakini a girl is normal healthwise.. Na zipi ni dalili za awali za ujauzito..?

NB: Naomba ujikite zaidi kwenye kujibu swali husika.. Kama huwezi basi ni busara zaidi ukasoma na kupita tu au kuweka like/dislike..

Karibuni wajuvi wa mambo!
 
sexologist kwa hii ID yako itakua wewe unamajibu mazuri ya swali lako
 
Last edited by a moderator:
Habari ndugu zangu, ninarafikiyangu anatatizo la kutokata kwa damu ya hedhi, sasa anamiezi mitatu hajawahi kujifungua wala kupata ujauzito.nisaidieni tatizo ni nini labda, na nini kifanyike? Asanteni.
 
Habari ndugu zangu, ninarafikiyangu anatatizo la kutokata kwa damu ya hedhi, sasa anamiezi mitatu hajawahi kujifungua wala kupata ujauzito.nisaidieni tatizo ni nini labda, na nini kifanyike? Asanteni.

Naomba nikufate PM kama hutajali uniambie kwanini unatumia ID hii...
 
Aende hospital, huko atakuwa muwazi kama alishawahi kutumia dawa za uzazi wa mpango ama lah. Pia kuna dawa huwa wanachomwa, inasababisha kufunga wa damu hiyo. Sijui sababu ya kutoka damu hiyo ni ipi wala madhara ya hizo sindano wanazochomwa.

Tena itakuwa vizuri akionana na Gyno.

Afu siku nyingine sitakupa ushauri ukianza mambo ya rafiki yangu wakati ni wewe.
 
hapana rafiki aseme hapa hapa nitakusemea kwa mama umeanza tabia ya kwenda vichakani

Hahahaha hapana rafiki, ID yake imeficha kitu may be atashindwa kusema hapa...naomba huyo mtu usimwambie nitalala chini leo
 
Yaani ana miezi mitatu tangu alipo anza ku bleed mfululizo.

Mpe pole rafiki yetu ila hiyo haitaitwa tena jina la hedhi, hedhi ni siku 7 kama sikosei, huo ni ugonjwa aende hospitali
 

Asante kwa ushauri. Ni rafiki yangu kweli na sio mimi.
 
Hii itakuwa ni njia za uzazi wa mpango ndo inamletea kubleed isivyo kawaida.mshauri amuone Daktari wa wanawake kwa matibabu/ushauri zaidi.
 
si aende hospitali? hapa watasaidia nini zaidi ya kumshauri akamwone gyno
 
pole sana uko wapi ni-pm nitakusaidia. inshaalha
Habari ndugu zangu, ninarafikiyangu anatatizo la kutokata kwa damu ya hedhi, sasa anamiezi mitatu hajawahi kujifungua wala kupata ujauzito.nisaidieni tatizo ni nini labda, na nini kifanyike? Asanteni.
 
docs,tafadhali naomba kufahamu tatizo ni nn? huyu m'mke alipata miscarrage tangu july 2013,lakini kila siku analalamika tumbo linauma,na bleeding haikatiki,halafu maziwa yavuja mpk sasa,hospl anaonekana tatizo hakuna,je shida ni nn?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…