Nini kinachangia makampuni ya mabasi kufa, pindi waasisi wanapokufa au kuwaachia watoto?

Kuna hajees, na Hajis, Hajis ni ya yule mzee wa arusha mtata mtata, wanamuita haji haji, aliyekuwa na ma mbuzi yanayozunguka mji mzima bila mchungaji, mbuzi zake zilikuwa zinachungwa na mbwa tu, sasa mkoromee mbuzi uone balaa la mbwa, hata akitafuna muhogo wako jikoni inabidi uwe mpole tu, ukimgusa mbwa wananunua kesi.
Nimekuelewa vp Tashriff na bembea bado zipo Capt Tamar
 
Watu wamejieleza sana ila point kubwa ni ;
1) succession plan .. hii wabongo hatuna !
2)kingine biasha zina siri ... nikisema siri unaelewa... mzee akiondoka mali zinaenda kimiujiza tu hadi mnafilisika ! Tena kama magari yanaoza kabisa na ukitengeneza Leo kesho inakuja shida hii...mwisho wa siku unapaki juu ya mawe
 
Waarabu na Wahindi wana succession plan nzuri sana

Mmiliki wa mabasi ya AN Classic alikufa kwenye ajali ya basi la AN na siku hiyo yeye ndiye alikuwa dereva Mbeya-Tabora chuma ikala buyu Chunya

Ulizia sasa hivi kampuni inaendaje? Mwaka jana mwishoni wameagiza mikwaju mipya ya Yutong D14 kutoka China

Angalia wamiliki wa kibongo sasa, Sauli mmiliki wa mabasi ya Sauli alipokufa na kampuni ikafa

Mmiliki wa mabasi ya Chakaby amekufa hivi karibuni hii kampuni ikitoboa miaka 5 ni kwa neema mark this comment
 
Kwa hood Inaelezwa madogo walimpiga chini aliyekuwa msimamizi na ndie aliyekuwa jiran na mzee kisa hakuwa mwanafamilia ila alilelewa na mzee wao nandio aliweza kuiendesha the rest madogo wakachemka kuiendesha baada wakata kumrudisha mwamba ikawa too late alikataaaa kurud maden yalikuwa mengi madogo bata nyingi
 
Mmiliki wa mabasi ya God First Luxury amekufa hivi karibuni hii kampuni ikitoboa miaka 5 ni kwa neema mark this comment
Wa God first yupo mkuu aliyefariki karibuni ni wa chakaby, bus za mwanza mbeya
 
Shida ndio hio hapo hakuna nyingine, kumfundisha mtoto kuna namna 2 moja ni kumpa mbinu na namna ya kuvua samaki au mbili kumpa samaki kila anapoomba kupewa samaki hapo ndipo kunapoanzia tatizo lenyewe la vifo vya makampuni, mtoto kashazoea kupewa samaki yeye samaki kuvua hajui unafikiri siku akipewa ndoana akavue na hakuwahi kufundishwa kuvua atafanya nini? Km sio kuitupa ndoana
Umenikumbusha baba angu huu msemo wake.

"Sikupi samaki, ila nakupa chambo na ndoano ukavue mwenyewe samaki, ili hata siku nikiwa sipo ukitaka samaki uweze kumpata".

Leo watoto wake wanaona faida ya huu msemo wake.
 
Nianze na mfano wa Hood class limited, Haya mabasi enzi zake kipindi kampuni anaiendesha mzee mwenyewe hood, yalikuwa ni balaa.

Ndio mabasi yakwanza kuwa na TV kwa ndani kwa Tz,
Ndio mabasi yakwanza kuwa na choo kwa ndani.

Marcopolo yakwanza bongo ni Hood ndio ilileta, hata madereva waliofanya kazi katika mabasi ya hood wote walitajirika sana.

Kwanini mabasi mengi hufa baada ya waasisi kuwaachia watoto shida huwa nini?
Mfano Ngorika, Mtei, Osaka, Mberesero, dar express, Royal coach, bembea, kimotco, fresh ya shamba n.k
Fresh ya Shamba alikiuka masharti ya mganga. Hajafa yuko Mbeya ni mtu wa kawaida tu
 
sio mabasi tu, biashara nyingi na miradi mingi mikubwa ya sisi Wabongo hufa kwa sababu mwanzilishi hakushirikisha watoto wake mapema, hakumwandaa mtu wa kuja kusimamia mapema, wengi hung'ang'ania kuongoza mpk anakuwa mzee au hana nguvu tena ndio anaweka mtu wa kusimamia, ambaye hajui chochote (biashara zina siri nyingi) wakati ilitakiwa kumwandaa mtoto mapema, hii ni tofauti sana kwa ndugu zetu Wahindi, mtoto mdogo akitoka shule anaenda dukani, anauza na kurudisha change mzazi akiwa pembeni...mfano mzuri ni MO Dewji kuna kijana wake ambaye anamwandaa vzr sana kuja kushika nafasi na mara nyingi kila mahali anakuwa naye...
Kwa wabongo, naona Wachaga wana hii desturi.
Kuna mzee alikua ni tajiri pale mtaani kwetu, alikua anawajengea watoto wakw msingi wa urithi ktk uchumi wake.
Though aliwapa Elimu, ila bado akawashirikisha ktk miradi yake, leo hii yeye kafariki miaka 7 nyuma, ila watoto wake wanaendeleza zile mali na miradi hadi kesho.
 
Waarabu na Wahindi wana succession plan nzuri sana

Mmiliki wa mabasi ya AN Classic alikufa kwenye ajali ya basi la AN na siku hiyo yeye ndiye alikuwa dereva Mbeya-Tabora chuma ikala buyu Chunya

Ulizia sasa hivi kampuni inaendaje? Mwaka jana mwishoni wameagiza mikwaju mipya ya Yutong D14 kutoka China

Angalia wamiliki wa kibongo sasa, Sauli mmiliki wa mabasi ya Sauli alipokufa na kampuni ikafa

Mmiliki wa mabasi ya Chakaby amekufa hivi karibuni hii kampuni ikitoboa miaka 5 ni kwa neema mark this comment
Yule wa AN alikuwa ni mtoto
 
Kwa hood Inaelezwa madogo walimpiga chini aliyekuwa msimamizi na ndie aliyekuwa jiran na mzee kisa hakuwa mwanafamilia ila alilelewa na mzee wao nandio aliweza kuiendesha the rest madogo wakachemka kuiendesha baada wakata kumrudisha mwamba ikawa too late alikataaaa kurud maden yalikuwa mengi madogo bata nyingi
Hivi yule jamaa aliendaga kufungua kampuni yake ya mabasi au vipi?
 
Nianze na mfano wa Hood class limited, Haya mabasi enzi zake kipindi kampuni anaiendesha mzee mwenyewe hood, yalikuwa ni balaa.

Ndio mabasi yakwanza kuwa na TV kwa ndani kwa Tz,
Ndio mabasi yakwanza kuwa na choo kwa ndani.

Marcopolo yakwanza bongo ni Hood ndio ilileta, hata madereva waliofanya kazi katika mabasi ya hood wote walitajirika sana.

Kwanini mabasi mengi hufa baada ya waasisi kuwaachia watoto shida huwa nini?
Mfano Ngorika, Mtei, Osaka, Mberesero, dar express, Royal coach, bembea, kimotco, fresh ya shamba n.k
Mzee Mtei yupo hai chief. Waliokufa ni wanawe wawili watatu hiviii! Ila mzee bado yupo!
 
Back
Top Bottom