Polepole ana hoja nzuri tu kwa anavyozijenga. Yeye kwa mujibu wake anataka chama chao kiende kwa mujibu ya katiba, na uta utamaduni wao.
Tundu Lissu nae ana hoja na agenda nzuri tu yenye maslahi mapana kwa taifa, tuwe democratic kweli kama tumeridhia, turekebishe hayo mambo kuwe na uchaguzi huru na haki. Kwa uzoefu wangu mdogo bila mapenzi kwa kweli kura huwa zinaibiwa.
Serikali nao wana SABABU zao nzuri tu kuendelea na mfumo uliopo japo una mapungufu yake mengi.
Humu JF tunatoana akili bure lakini wakati mwingine anaekuambia ujitoe katika mapambano, hana hata experience ya matumizi ya mabavu katika kudai haki yake binafsi. Huenda hata shule au chuo hakuwahi kukaa frontline katika migomo akaona namna watu wanavyoweza kukuacha mwenyewe.
Watanzania kiukweli wengi wanajitambua, achana na suala la elimu zao, wanajua vizuri tu kuwa kuna tatizo lakini "masihi" wetu hajaja.
Hata yule aliyefanana fanana,na akaenda zake hakuwa mkweli kivile, rejea issue ya trillion 1.4, watu kupotea, bwawa la Nyerere kusemekana linajengwa kwa gharama zaidi ya gharama halisi n.k n.k
Ukituliza kichwa unaweza kuona atleast huyu Lissu ana ukweli katika anayoyaamini kwa mujibu wa haki za katiba yetu, na taratibu za uendeshaji wa serikali... kinachomponza ni approach yake ya mwaka 3000 kwa Tanzania, yeye anataka aitumie 2025.
Polepole kwa haraka ni issue ya genge lao kuonekana linafutwa kabla halijafikia height tarajiwa ndani ya chama. Kama jamaa ni mkweli na alitaka watanzania tuishi kwa kunufaika kwa mujibu wa katiba na rasilimali zetu basi angeanza mapema pindi alipokuwa katika nafasi, pia hakuna hukumu ya moja kwa moja huenda kabadilika anataka chama kiende inavyotakiwa.
Mbona CCM hawamvui uanachama? Inawazisha hii.
Hint nyingine ni kuwa hali ya udini katika masuala ya serikali na uendeshaji inafumbiiwa macho lakini ipo, huenda kwa kasi ya ukuaji wa udini ni kubwa kuliko ukanda na ukabila. Lakini huwa inaonewa aibu hasa na dini hizi mbili Waislamu na Wakristo wa kikatoliki kuliongelea.
Pia kuna influence za majirani katika kutupachikia wageni katika maeneo nyeti, reference;
Askari wa JWTZ mwenye asili ya Rwanda adaiwa kutoroka Tanzania! Jeshi limesema litatoa taarifa zaidi kuhusu mwanajeshi huyo anayedaiwa kutoroka na nyaraka muhimu za jeshi!! Source: Mtanzania Jumapili ====== OFISA wa cheo cha juu katika Jeshi la Wananchi (JWTZ), anayeaminika kuwa na asili...
www.jamiiforums.com
Kuna mama aliwahi kushika nafasi nyeti tu BOT sio raia wa Tanzania, mpaka alipogundulika na kusimamishwa hata hatujui yaliishia wapi.