Nilikuwa kusini, ambako ndiyo nyumbani kwa Harmonize......nilichokutana nacho nilishangaa sana. yaani habari kubwa huko ni Diamond na alikiba, Harmonize yuko mbali kidogo kutoka kwa hao jamaa. kabla nilifikiri atakuwa na maelfu ya mashabiki kuwazidi wote kwakuwa anatoka huko.
Yote kwa yeto, anajitahidi sana maana kuendelea kuwepo tu mpaka muda huu ni ushindi tosha kwake....wafikiriwe tu waliochemka. Tatizo lake tu kuwa anapenda mno kujitutumua kwa huyo diamond kitu ambacho si chema sana kwani mwenzake yupo kitambo sana
Kwangu mimi, heshima pekee imuendee huyu alikiba.....jamaa ni wa tofauti sana aisee; yupo sana tu, utamsikiliza utamchukia baadae unarudi tena kumsikiliza mwenyewe. wengine wote watapita na watamuacha amesimama pale pale. tusubiri tu!