Nini kipo nyuma ya ukuaji na ongezeko la watu wasiokuwa na dini?

Nini kipo nyuma ya ukuaji na ongezeko la watu wasiokuwa na dini?

Habari 👋🏾

Nimefanya tafiti katika vipindi, nyakati na maeneo tofauti na inaonekana wazi ushawishi wa dini unapungua kwa kasi kubwa sana.

Inaonekana wengi kutokuwa na hakika katika dini mbalimbali na wengi wao bado wanajaribu kujionesha katika ngwe hiyo kwa sababu kadhaa ikiwemo kutokataliwa na jamii hizo.

Je, ni ipi sababu ya ukuaji wa kiwango hiki cha watu kutokuwa na dini kama ilivyozoeleka?
=>Utandawazi na elimu: hivi vitu vimerahisisha upatikanaji wa maarifa, na binadamu waliopata neema ya kuyapata hayo maarifa wamepevuka kiupeo.

Wanasemaga "njia ya muongo ni fupi"
 
Kwa maana hiyo unataka kuniambia kuwa waislam wana MUNGU wao na wakristo nao wana MUNGU wao...Yes kwa hiyo hapo tayari wamepatikana miungu wawili provided kwamba hatuwezi kubainisha ukweli na uongo!
Mingi wa wakristo yesu,alizaliwa na mariamu,mungu wa waislam Allah(sw),muumba wa kila kitu akiwemo mariamu na yesu mungu wa wakristo,mungu wa wahindu ng'ombe
 
Sisi binaadamu ni viumbe wa mwisho kuumbwa ninamaana hapo mwanzo kulikuwapo na viumbe walio ishi kabla yetu na huyo ambaye kwa sasa ni shetani ni mmoja wa viumbe hao
Hilo linafahamika Sasa huyo shetani alipata wapi roho ya uasi akiwa Hiko mbinguni tunapoaminishwa hakuna ubaya?
 
Utaitafuta Dini au utamfuta Mungu?Dini zimefail ndio maana uovu umeongezeka Mara dufu.Siku watu wakiamua kutafuta Mungu na kuwa na hofu nae Dunia hii tutaifaurahi.NB Mungu hayupo kwenye hizo Dini Yesu kristo alileta Wokovu sio ukristo.Ukristo ni matokeo ya watu wachache kutaka kuhodhi wenzao.Mungu awe nawe Daima.
Kuamini mungu Bila kuwa na utaratibu wa maisha toka kwa mungu huyo ni unyama
 
Kuna Bible/ Quran ndugu.....ambavyo ndo muongozo na msingi wa IMANI...hivi vitabu sio DINI bali ni IMANI....so nitaenenda Kwa misingi ya hivyo vitabu na si DINI.
Dini ni mfumo wa maisha,usipozini,usipoua,usipokula ribs,usipodhilumu,usipoabudu mungu mwingine zaidi ya Allah,ukiamini siku ya malipo,hapo unakua umeishi kiislam
 
Kama Mungu anadhihakiwa na kudharauriwa hivi hadharani

Ni dalili za wazi mwisho wa dunia haupo mbali sana
 
Kuna tofauti kubwa Sana Kati ya DINI na IMANI....hata kwangu Mimi siamini Sana katika dini Ila kwangu IMANI ya uwepo wa MUNGU MUUMBA NA MWENYEZI ninayo na hiki ndo nadhani ni kitu muhimu Sana kuliko DINI.
Safi sana mkuu... kuna uwezekano hizi dini zinauhusiano na Mungu (yaani zinajibabatiza kwa) ila Mungu mwenyewe hana uhusiano na hizi dini(kwa maana kwamba hakuamrisha iundwe dini ila watu tu wenyewe waliamua kufanya hivyo).
 
Nimeona jibu lako nilicho gundua mimi na wewe ni imani za dini mbili tofauti ili tuwekane sawa ni lazima tuamini kitabu kimoja bila ya hivyo kuelewana ni ngumu
Sasa siku nyingine usipinge kitu mbacho hujaelewa. Jifunze kuuliza
 
Inaonekana kuna maswali mengi miongoni wa waumini, lakini kwa nini awahoji masuala haya katika mikusanyiko yao?
Kukuuliza unaambiwa kuna mabo hutakiwi kuhoji kwa sabbu ni kumtilia Mungu mshaka.

Ndio maana kwenye mikusanyiko ya dini baada ya mahubiri hawaruhusu maswali, vinginevyo watakimbia madhabhu maana kuna vitu viko kwenye mwandiko amvayo tafsiri zake hawazijui.
 
Unamaanisha dini ni sehemu ya watu wasiokuwa na uwezo wa reasoning? Ni yapi ambayo yamefichwa kwa watu wasiokuwa na uwezo huo?
Nadhani haujaelewa nilichokimaanisha ila yanayotendeka na yanayotendwa na viongozi wetu wa kiroho huwa yanaturudisha nyuma sana kiimani aise.
 
Niongezee kidogo hapa; ilikuwa je akaasi wakati tunaambiwa Mungu anatujua hat jabl hatujazaliwa; kanuni aliruhusu shetani awepo?
nakazia Tena hapa ilikuaje alivyoasi akamtupa duniani kwenye sayari wanayoishi viumbe binadamu Ili hali akijua atakuja kuwavuruga,na yeye hukiri kwamba binadamu ni kiumbe dhaifu yaani akili za huyo Mungu ni sawa na za baba Mwendawazimu anayefungia watoto chumbani na kuwatupia nyoka mwenye sumu Kali black mamba na anawambia wamshinde Kwa kuepuka sumu yake Ili hali yeye kamshindwa!
 
Back
Top Bottom