SAWA.
Na itafurahisha sana kama hayo uliyoyaeleza yatakuwepo.
Lakini swali gumu ni hili: Yote hayo yatarudi na kusimamiwa na hawa hawa waliojitoa akili na kuimba nyimbo za mfalme sasa hivi?
Mbona huo utakuwa kama muujiza? Viongozi hawa hawa watoke katika kutekeleza kila wanachoagizwa, hadi akili ziwarudi na kuanza kufanya kazi kwa kutumia akili?
Au wote wataondoka na mfalme wao; na hao wapya je, wamejificha mahali wakisubiri wakati wao?
Mkuu, mi nadhani umeipaka bendera yetu rangi nzuri kuliko uhalisia wenyewe. Twende taratibu kidogo kidogo, pengine tutafika huko tunakokupenda sote hatua kwa hatua.