Nini maana ya ndoto hii?

Nini maana ya ndoto hii?

Nimeota nipo sehemu nisioijua ni kama mji hivi, umechangamka kiasi nikajikuta na mtu nisiemjua, tukaenda kwenye mwembe uliokua umemwaga maembe mengi lakini hayana muokotaji.

Basi tukaanza kuyaokota lakini mengi yalikua mabichi nikasema niokote mabichi ndio makubwa na la kuiva lilikua dogo nililiokota hivohivo, kwa pembeni kulikua na nyasi nikahisi uwepo wa nyoka mweusi mdogo, nikarusha jiwe sikujua kama lilimpata au la, nikajikuta kwenye mfuko nina embe moja tu lililoiva dogo.

Nikawa najiuliza inawezekanaje wakati nimeokota mengi sana na yule mtu alinipotea tu sikumuona, nikajikuta nipo mjini kwenye huo mji, kilichonifanya nijue hapa ni mjini ni wingi wa magari ajabu kila gari ninayotaka kuipanda imejaa na haisimami, mwisho ikaja gar haikua na watu wengi nikaingia lakini lile gari likakwama kuondoka.

Nikashtuka, inaweza kuwa kuna kitu gani kinaendelea? naomba kutafsiriwa kwa anejua.
Omba Mungu kwa imani yako ili akuonyeshe kama ni ndoto ya mafanikio au ya watu waovu.
 
Kuna mwanaume alikuhadaa au ata kuhadaa kufanya jambo ambalo Kwa picha ya nje litaonekana Lina manufaa lakini baadae halitokuwa na manufaa. Kwa kifupi mtu huyo atakupotezea sana muda.😭😭😭😭

Atasababisha hata wengine uwanyime nafasi na wao pia kipindi ambacho huyo mtu atakuwa ameondoka awatokupa nafasi...!​
au sio? vipi kama nimeolewa? kwa hio baba mwana ananihadaa sio? 😂😂😂 pls come again
 
Naona watu wanapinga ndoto..

Usipuuze ndoto iwe nzuri au mbaya...

Ndoto ni njia ya Mungu kuongea na wanadamu..
 
Hapo ulikuwa Gaza,na maembe uloyaona ni mabomu. So? Mi natania bwana
 
Acha kusikiliza maneno ya watu (mji wenye watu wengi usio wajua)na usipokee kila ushauri unaopewa( maembe mabichi), Una melengo uliojiwekea japo hujui namna ya kuyageuza kuwa mafankio(embe dogo mfukoni) ,Jipange uongeze elim ujitofautishe na watu wengi (watu kwenye gari lilojaa) ,Wenye mafanikio (gari ulilopanda) siku zote huwa ni wachache acha kufuata mkumbu.
Duuh...! Unatafsiri siku zote mkuu au niaje?. Ni kama uko mle mle. Uko vizuri mkuu
 
Back
Top Bottom