Nini madhara ya Kutoonekana mahakamani katika kesi ya Ndoa?

Inaonekana mkeo amerubuniwa huko nje na watu kama vile marafiki,ndugu au jamaa,kaza mkuu utavuka tu hili,na huyo mkeo atakuja kujuta huko mbeleni ila usimpe nafasi tena,

Muhimu jali wanao kwa hukumu yeyote ile itakayo tokea,weka makaratasi yote yakimahakama pamoja ili huko mbeleni uje uwaonyeshe wanao waujue ukweli,

All the best Mkuu.
 
Ahsante kwa ushauri mkuu, karatas zoote kuanzia samansi ya polisi aliponilaza ndani na hii ya mahaka vyoote hivi vile well stored for future uses
 
Siku ile nilivyokwambia wewe ni mwanaume legelege ukaona natania.

Hutaki kwenda mahakamani kusomewa mashtaka. Hukumu ikitoka utasikilizwa upande mmoja, nyumba atapewa mwanamke alafu uachiwe mzigo wa kutunza watoto wakati umetoka kapa. Si bora muuze nyumba mgawane, au umuachie ila matunzo ya watoto usitoe.

Na gharama za matunzo ya watoto mwanamke atadai labda milioni kwa mwezi na ambavyo haupo itapitishwa. Ukiwepo unatoa hoja za kwanini kiasi kiwe chini.
 
Pole sana aisee, ngoja wajuvi waje, ila hawa wanawake hawa ndio maana wengine wanaamua kuwakia kiberiti
Kwakwel ukiwa na moyo dhaifu unaweza fanya kitu kibaya sana.
Nilipopokea samansi ,siku nzima ikawa mbaya mnooo, hisia za chuki, hasira na uchungu nikiona nimesalitiwa pakubwa mnooo na mtu ambaye sikutegemea, nilietoka nae mbaalii toka 0 hatuna kitu tukiwa tumekutana kama form 6 leavers 2010 Feb..

Hizi hisia unaweza ua au ukajiua kama utakosa watu wa kukusaidia.
Kuna jamaa yangu mmoja kila napozidiwa na mawazo huwa nampigia simu najieleezaaaa, atanisiklizaaaaa bila kuchoka na kunishauri tena na tena na tena ,haijalishi ni mara ngapi kwa siku, he has been so welcomming na hii ndio imekua ikinisaidoa kuondoa uchungu na hisia mbaya
 
Ni hasara mwanangu, ndoa?? Ndoa sio kabisaa mazee
 
π™³πšŠπš‘ πšœπš’πš”πšž πš’πš£πš’ πš—πšπš˜πšŠ πš£πš’πš–πšŽπš”πšžπš πšŠ πšŒπš‘πšŠπš—πšπšŠπš–πš˜πšπš˜, πš πšŠπš—πšŠπš πšŠπš”πšŽ 𝚠𝚊 πšœπš’πš”πšž πš’πš£πš’ πš’πš”πš’πšπš˜πš”πšŽπšŠ πšŸπšžπš›πšžπšπšž 𝚝𝚞 ,πš–πšŠπš‘πšŠπš”πšŠπš–πš—πš’ πš”πšžπš˜πš–πš‹πšŠ πšπšŠπš•πšŠπš”πšŠ πš—πšŠ πš”πšžπšπšŠπš πšŠπš—πšŠ πš–πšŠπš•πš’
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…