Nini madhara ya Kutoonekana mahakamani katika kesi ya Ndoa?

Nini madhara ya Kutoonekana mahakamani katika kesi ya Ndoa?

Siku ile nilivyokwambia wewe ni mwanaume legelege ukaona natania.

Hutaki kwenda mahakamani kusomewa mashtaka. Hukumu ikitoka utasikilizwa upande mmoja, nyumba atapewa mwanamke alafu uachiwe mzigo wa kutunza watoto wakati umetoka kapa. Si bora muuze nyumba mgawane, au umuachie ila matunzo ya watoto usitoe.

Na gharama za matunzo ya watoto mwanamke atadai labda milioni kwa mwezi na ambavyo haupo itapitishwa. Ukiwepo unatoa hoja za kwanini kiasi kiwe chini.
Jamaa anazingua,,,hapo ubaya ubwela
Nenda mahakami kama mali zote zilipatikana ndani ya ndoa,,,ziuzwe mgawane kila mtu akafie mbele,,,,watoto mtajua jinsi ya kuhudumia
 
Kwanini Unafanya Uamuzi wa kuacha Kila kitu?.

Kwanini wanaume wajinga huwa mnaamini Maisha ni kufumba na Kufumbua umetoboa?.

Kwanini wanaume wajinga ,Huwa mnafanya maamuzi ya ajabu sana?.

Unahisi huko ulikoenda kuanza Upya, Utafanikiwa?.

Kwamba Unahisi ukimuachia Kila kitu, Nawewe ukaenda kuanza Upya, siku ukifulia atakupokea?

Kama ambavyo Hana kitu lkn kaamua kutaka nusu ya Mali, vivovivo utakapofulia utakua Hauna Thaman yoyote kwako.

Wewe huwajui Wanawake, Wanawake hawajawah kupenda na hawatokaa wapende, WANAWAKE SIKU ZOTE HUMHESHIMU MWANAUME YOYOTE atakayepita machoni mwao na kuwafanyia wajihisi comfotaboooo.

Hapo upo ??

Jambo ambalo ulitakiwa kulipigania ni kuhakikisha JASHO LAKO HALIPOTEI BURE

Ona mtego ulipo, Anachukia Kila kitu, wewe ndo umeenda kujitafuta Upya, alafu bado UTAWAJIBIKA KWEMYE MATUNZO BILA KUJALI UNAJITAFUTA AU LAH!!.

NADHAN UMEROGWA, WALA USIDHAN NDIO UANAUME.

Mimi Sina Undugu na mwanamke, Undugu wangu ni watoto tu .
Eheheh..mkuu umenifokea sana bwana
 
Wakuu heshima kwenu.

Habari za jioni, poleni na majukumu (kwa wale wenye majukukumu).

Naomba kufahamishwa KISHERIA kama kichwa cha uzi kimavyojieleza.

Mi hivi, baada ya mgogoro wa ghafla sana (only 2 months now) na vurugu zilizofuata hapo, hatimae mke wangu ame file kesi mahakama ya mwanzo jii ya dai la talaka.

Nimepogiwa simu siku kadhaa zimepita sasa kitaarifiwa pia kitakiwa kuchukua wito "samansi" wa mahakama juu ya kesi husika na kweli nikachukua.

Charges ambazo nimekuta zimeainishwa ni kama 4 hivi ikiwemo
  • talaka
  • mgawanyo wa mali
  • matunzo ya watoto
  • kuishi na watoto

Sasa katika maisha yetu tulifanikiwa kijenga nyumba , kuwa na kiwanja pia usafiri ndio angalau kwa uchache vitu vya kueleweka.

Wazo langu mimi ni kwamba, sitaki habar za kugombania kitu na huyu mama ambaye mpaka sasa alishachukua watoto na kwenda kupanga mtaani.

Na mi pia nikaamua kuhamisha harakati zangu mkoani kulingana na nature ya shughul zangu.
Hivyo sina mpango wa kugombania mali wala chochote katika vyote tulivyo navyo.

Moja ya vipengele nimesoma kwenye hii samansi ya mahakama inasema "endapo mdaiwa
 
Eheheh..mkuu umenifokea sana bwana
Acha Ufala aiseee.

Wenzio Akina Bill gates wanakomaa kuliko kupoteza chote, wanaamua kugawana.

Unadhan kwann?? Unafikiria Maisha na mwanzo wake ni mwepesi kama unavyowaza?

Sasa huyo ni Bill Gates, ni vipi kuhusu Mtanzania wewe unayejitafuta?.

Kutokuonekana kwako maana yake ,Maamuzi ya Hukumu yataegemea Upande mmoja tu.

Mke atapewa Kila kitu, na kwakua Watoto ni Wa Baba, wewe Tena ndo UTAWAJIBIKA malezi.

Maisha yako yatakua yakupelekwa Polisi Kila siku, utayachukia, Akili itakua kifungoni, matokeo yake msongonwa mawazo,mwanaumke anazidi kupigwa Mashine Nje n.k mpaka unakufa mwenyewe.
 
Wakuu heshima kwenu.

Habari za jioni, poleni na majukumu (kwa wale wenye majukukumu).

Naomba kufahamishwa KISHERIA kama kichwa cha uzi kimavyojieleza.

Mi hivi, baada ya mgogoro wa ghafla sana (only 2 months now) na vurugu zilizofuata hapo, hatimae mke wangu ame file kesi mahakama ya mwanzo jii ya dai la talaka.

Nimepogiwa simu siku kadhaa zimepita sasa kitaarifiwa pia kitakiwa kuchukua wito "samansi" wa mahakama juu ya kesi husika na kweli nikachukua.

Charges ambazo nimekuta zimeainishwa ni kama 4 hivi ikiwemo
  • talaka
  • mgawanyo wa mali
  • matunzo ya watoto
  • kuishi na watoto

Sasa katika maisha yetu tulifanikiwa kijenga nyumba , kuwa na kiwanja pia usafiri ndio angalau kwa uchache vitu vya kueleweka.

Wazo langu mimi ni kwamba, sitaki habar za kugombania kitu na huyu mama ambaye mpaka sasa alishachukua watoto na kwenda kupanga mtaani.

Na mi pia nikaamua kuhamisha harakati zangu mkoani kulingana na nature ya shughul zangu.
Hivyo sina mpango wa kugombania mali wala chochote katika vyote tulivyo navyo.

Moja ya vipengele nimesoma kwenye hii samansi ya mahakama inasema "endapo mdaiwa /mlalamikiwa (mimi yani ) hatafika mahakamani , shauri litasomwa na kusikilizwa upande mmoja bila mimi kuwepo.

Sasa naomba kufahamu, kisheria kama nitaamua KUTOONEKANA mahakamani siku hiyo, je ,nitakua nimetemda UHALIFU ambao unaweza kunigharimu??

Naomba kusaidowa ufafanuzi.

Ahsanten
Utaitwa kwa "summons" Mara tatu.. Kama utakuwa huzipokei zitatumwa kwa njia ya WhatsApp
Kama hujatokea sheria inamruhusu kwenda kwenye gazeti la serikali na kuweka tangazo hilo la wito juu ya kesi ya mahari
Tangazo husika lina vipimo maalum na linalipiwa
Mdai sheria itamtaka apeleke mahakamani risiti ya tangazo na gazeti ama kipande cha gazeti la serikali lenye tangazo husika
Baada ya hapo kesi itaitwa tena kama bado hujatokea ataapa na kutoa ushahidi wake bila uwepo wako.. Kisha hakimu atatoa hukumu ya upande mmoja na kumpa ushindi yeye
Hukumu ikishatoka hataipewa mpaka upite mwezi nadhani kwa ajili ya kutoa nafasi ya kukata rufaa.. Kama mpaka hapo bado tuu .. Jalada la shauri litafungwa na yeye kutakiwa kukazia hukumu.

Ushauri Wangu kwa afya ya watoto unaweza kuwaandia power of attorney umiliki wa nyumba na mashamba
Mama usimuache kabisa. Ila mwache aende mwenyewe mahakamani..KESI ZA TALAKA ZINADHALILISHA SANA
 
Hao watoto mali wamezitafuta lini ilhali bado wadogo,mnashauri vitu ambavyo hamvijui mkuu, mali lazima mgawane na jukumu la mume ni kulea watoto,

Wanawake nuksi sana
 
Nenda Mahakamani. Kataa Talaka kama Ni mkristo kisha omba mtengwe mjitafakari.

Au
Kubali Talaka
Kubali Mgawanyo wa Mali nusu kwa nusu
Sijui Umri wa watoto kama ni 7+ wachukue wewe wote itakusaidia kwenye matunzo

Au usiende mahakamani
Mahakama ivunje ndoa
Igawanye mali
Impe mwanamke watoto
Upewe garama za matunzo.

Je Mwanamke akiolewa tena papo kwa hapo sheria inasemaje?
Unawezaje kugomea talaka mkuu, nisaidie hapo ufafanuzi
 
Usipoenda mahakama itatoa maamuzi inaweza kuamua nyumba abaki nayo mke wako na upeleke pesa ya matumizi kila mwezi.

Sasa usipotekeleza baada ya hapo polisi watapewa Arrest warrant waje kukukamata kwa kudharau amri ya mahakama alaf utaenda kupumzishwa mahabusu gerezani siku kadhaa
Ahahahah.
Kwahiyo kumbe usipopeleka matumiz ni kssi??
Kudadekii.. hapo sasa mwanamke sinanaweza kukunyanyasa sana kama utatoa matumiz bila kuweka proper records ,akisema hujatoa!!?
 
Kwahiyo jukumu hil la kulea watoto, kisheria mama yao halimuhusu mkuu??
Sheria zetu ni za ovyo sana,zina wapendelea wanawake, halafu mitoto yenyewe ikikuwa inaegemea kwa mama yao ilhali umetumia ghalama kubwa kuilea na kushtakiwa umeshtakiwa, mkuu jitaidi ufike mahakamani kutetea haki yako,usipoenda huyo shetani atapewa mali zote yeye.
 
Hao watoto mali wamezitafuta lini ilhali bado wadogo,mnashauri vitu ambavyo hamvijui mkuu, mali lazima mgawane na jukumu la mume ni kulea watoto,

Wanawake nuksi sana
Mkuu what if kama mlishawah kuchukua mkopo na moja kati ya mali zilizo kwenye mgawanyo ( nyumba au kiwanja) mlichukulia mkopo kama dhamana, je mahakama itaamuru kuuza hivyo au mliyemkopa anaweza akazuia kwa kuweka stop order kisa dhamana????

Nisaidieni hapa pia
 
Back
Top Bottom