Nini madhara ya Kutoonekana mahakamani katika kesi ya Ndoa?

Nini madhara ya Kutoonekana mahakamani katika kesi ya Ndoa?

Yani ndo kilichomkimbiza mahakamani hiki😳,,nenda mahakamani naamini huwa haitoi maamuzi hapo hapo,kuna muda mtapewa wa kujitafakari huku mkiendelea kuishi pamoja,,,,,, nasema ivi coz nna ushuhuda wa wazazi wangu.
Na tena katika miaka yetu 15, nimempiga mara hiyo 1 tu, na sikumtoa hata ngeu wala damu wala kumvunja popote.
 
Wakuu heshima kwenu.

Habari za jioni, poleni na majukumu (kwa wale wenye majukukumu).

Naomba kufahamishwa KISHERIA kama kichwa cha uzi kimavyojieleza.

Mi hivi, baada ya mgogoro wa ghafla sana (only 2 months now) na vurugu zilizofuata hapo, hatimae mke wangu ame file kesi mahakama ya mwanzo jii ya dai la talaka.

Nimepogiwa simu siku kadhaa zimepita sasa kitaarifiwa pia kitakiwa kuchukua wito "samansi" wa mahakama juu ya kesi husika na kweli nikachukua.

Charges ambazo nimekuta zimeainishwa ni kama 4 hivi ikiwemo
  • talaka
  • mgawanyo wa mali
  • matunzo ya watoto
  • kuishi na watoto

Sasa katika maisha yetu tulifanikiwa kijenga nyumba , kuwa na kiwanja pia usafiri ndio angalau kwa uchache vitu vya kueleweka.

Wazo langu mimi ni kwamba, sitaki habar za kugombania kitu na huyu mama ambaye mpaka sasa alishachukua watoto na kwenda kupanga mtaani.

Na mi pia nikaamua kuhamisha harakati zangu mkoani kulingana na nature ya shughul zangu.
Hivyo sina mpango wa kugombania mali wala chochote katika vyote tulivyo navyo.

Moja ya vipengele nimesoma kwenye hii samansi ya mahakama inasema "endapo mdaiwa /mlalamikiwa (mimi yani ) hatafika mahakamani , shauri litasomwa na kusikilizwa upande mmoja bila mimi kuwepo.

Sasa naomba kufahamu, kisheria kama nitaamua KUTOONEKANA mahakamani siku hiyo, je ,nitakua nimetemda UHALIFU ambao unaweza kunigharimu??

Naomba kusaidowa ufafanuzi.

Ahsanten
Pole sana ndiyo maana mimi nimeshtuka mapema eti kanunua kiwanja chake kimya halafu kwenye kujenga eti tujenge wote sijachangia hata mia naogopa baadae kunyanyaswa
 
Pole sana ndiyo maana mimi nimeshtuka mapema eti kanunua kiwanja chake kimya halafu kwenye kujenga eti tujenge wote sijachangia hata mia naogopa baadae kunyanyaswa
Yaan hiyo tayar ni red flag mkuu. Hapo kuaminiana kabisaa unaona ni shida maana full mtego.
Yan ndoa za siku hiz ni tabu sanaa
 
Na tena katika miaka yetu 15, nimempiga mara hiyo 1 tu, na sikumtoa hata ngeu wala damu wala kumvunja popote.
Ni hasira tu uyo, sasa nawewe usitumie hasira kususia mahakama,nenda mpewe muda hasira zitaisha mengine yataendelea,na muda wenyewe ni zaidi ya mwezi sasa hadi apo mtakua shwariiiiii

Nb,,miaka 15 mingi jamani, naamini chembe za upendo bado mnazo mioyoni mwenu,,nachukia talaka hadi kesho huwa namuomba Mungu wazazi wangu warudi pamoja.
 
Sio wewe tu imekutokea, hayo huwa yanatokea, stahamili, muombe Mungu akupe subira na uvumilivu yatapita salama.
Kuna jamaa mwezi ulopita alipelekwa polisi kisha mahakani yeye na mwanae ambae wamezaa na mkewe huyo sababu wameenda home toka Safari bila kumtaarifu wakati kulikuwa na kutoelewana , akasema wanemwibia n.k
Ebwanaa ilikuwa almanusra wafungwe wakati mtoto ni mwanafunzi wa sekondari.
Jamani ambao bado hamjaoa Ombeni na kufunga na wazazi wenu Mungu awaongoze kuchaguaa sahihi wanawake wa sasa wengi wamekuwa na mioyo mikatili mno.
Hizi empowerments zimeharibu na mioyo migumu na ushirikina.
Familia nyingine sio za kuoa.
 
Hivi kwa nia ya kujifunza.
Kama umeoa mfano mwanamke akakuta una nyumba,gari na assets zingine.

Mbele ya safari likija swala la talaka hizi mali alizokuta zinamhusu kwenye kugawana?
Wqtakuja wenyewe wataalam, ila uwezekano upo kama suala la kuendelezwa kwa mali hizo kutamhusisha.
Mfano, kakukuta na nyumba ila bada ya kuoana mkajenga fensi na yeye akichangia, hiyo bana ishakula kwako. Nafikiri hata akinunua balbu tubakaweka 😂😂😂😂.
Akikupikia uwe na nguvu ili uendeahe hilo gar barabarani, tayar na yeye anahusika..

NB
Nimesoma mahala
 
Hivi kwa nia ya kujifunza.
Kama umeoa mfano mwanamke akakuta una nyumba,gari na assets zingine.

Mbele ya safari likija swala la talaka hizi mali alizokuta zinamhusu kwenye kugawana?
Mali zilizo patikana kabla ya ndoa huwa hazi orodheshwi kwenye mgao wa mali baada ya talaka.
 
Sio wewe tu imekutokea, hayo huwa yanatokea, stahamili, muombe Mungu akupe subira na uvumilivu yatapita salama.
Kuna jamaa mwezi ulopita alipelekwa polisi kisha mahakani yeye na mwanae ambae wamezaa na mkewe huyo sababu wameenda home toka Safari bila kumtaarifu wakati kulikuwa na kutoelewana , akasema wanemwibia n.k
Ebwanaa ilikuwa almanusra wafungwe wakati mtoto ni mwanafunzi wa sekondari.
Jamani ambao bado hamjaoa Ombeni na kufunga na wazazi wenu Mungu awaongoze kuchaguaa sahihi wanawake wa sasa wengi wamekuwa na mioyo mikatili mno.
Hizi empowerments zimę Haribo na mioyo migumu na ushirikina.
Familia nyingine sio za kuoa.
Sasa akataka amfunge mpaka mwanae ?? Hiz familia kiukwel za kuangalia sana kabla ya hujachukua uamuzi wa kuoa
 
Hivi kwa nia ya kujifunza.
Kama umeoa mfano mwanamke akakuta una nyumba,gari na assets zingine.

Mbele ya safari likija swala la talaka hizi mali alizokuta zinamhusu kwenye kugawana?
Kuna condition mnaweza kugawana Kama tu utamshirikisha uwepo wa hiyo Mali...pia mnaweza msigawane Kama hutamshirikisha uwepo wa hivyo vitu.
 
Wqtakuja wenyewe wataalam, ila uwezekano upo kama suala la kuendelezwa kwa mali hizo kutamhusisha.
Mfano, kakukuta na nyumba ila bada ya kuoana mkajenga fensi na yeye akichangia, hiyo bana ishakula kwako. Nafikiri hata akinunua balbu tubakaweka 😂😂😂😂.
Akikupikia uwe na nguvu ili uendeahe hilo gar barabarani, tayar na yeye anahusika..

NB
Nimesoma mahala
Hivyo ndivyo ilivyo nimemjibu pia
 
Yaan hiyo tayar ni red flag mkuu. Hapo kuaminiana kabisaa unaona ni shida maana full mtego.
Yan ndoa za siku hiz ni tabu sanaa
Acha tu kuna kipindi tulinunua kiwanja mm nilikuwa naishi mkoa mwingine na yeye mkoa mwingine sasa kutokana na kumuamini sikuwahi kumuuliza kuhusu document za hicho kiwanja. Hivi karibuni nikauliza nimepigwa kalenda miez kadhaa sasa juz juz ananionyesha hizo document nakuta kajiandika yeye tu
 
Back
Top Bottom