Nini madhara ya Kutoonekana mahakamani katika kesi ya Ndoa?

Nini madhara ya Kutoonekana mahakamani katika kesi ya Ndoa?

Fanton Mahal

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2024
Posts
1,597
Reaction score
4,661
Wakuu heshima kwenu.

Habari za jioni, poleni na majukumu (kwa wale wenye majukukumu).

Naomba kufahamishwa KISHERIA kama kichwa cha uzi kimavyojieleza.

Mi hivi, baada ya mgogoro wa ghafla sana (only 2 months now) na vurugu zilizofuata hapo, hatimae mke wangu ame file kesi mahakama ya mwanzo jii ya dai la talaka.

Nimepogiwa simu siku kadhaa zimepita sasa kitaarifiwa pia kitakiwa kuchukua wito "samansi" wa mahakama juu ya kesi husika na kweli nikachukua.

Charges ambazo nimekuta zimeainishwa ni kama 4 hivi ikiwemo
  • talaka
  • mgawanyo wa mali
  • matunzo ya watoto
  • kuishi na watoto

Sasa katika maisha yetu tulifanikiwa kijenga nyumba , kuwa na kiwanja pia usafiri ndio angalau kwa uchache vitu vya kueleweka.

Wazo langu mimi ni kwamba, sitaki habar za kugombania kitu na huyu mama ambaye mpaka sasa alishachukua watoto na kwenda kupanga mtaani.

Na mi pia nikaamua kuhamisha harakati zangu mkoani kulingana na nature ya shughul zangu.
Hivyo sina mpango wa kugombania mali wala chochote katika vyote tulivyo navyo.

Moja ya vipengele nimesoma kwenye hii samansi ya mahakama inasema "endapo mdaiwa /mlalamikiwa (mimi yani ) hatafika mahakamani , shauri litasomwa na kusikilizwa upande mmoja bila mimi kuwepo.

Sasa naomba kufahamu, kisheria kama nitaamua KUTOONEKANA mahakamani siku hiyo, je ,nitakua nimetemda UHALIFU ambao unaweza kunigharimu??

Naomba kusaidowa ufafanuzi.

Ahsanten
 
Ndoa ni hasara sana.

Hebu tazama mwanaume mwenzetu anavyopata shida, hana uhuru tena na maisha yake kwa ujumla, hata kama hili litaisha, atabaki na kovu moyoni mwake milele.

Na kwa jinsi sheria zilivyo kandamizi hapo ni lazima mwanamke ashinde kesi.

Kataa ndoa, ndoa ni utapeli ndio maana inawezekana kuzaa hata bila ndoa.
 
Wakuu heshima kwenu.

Habari za jioni, poleni na majukumu (kwa wale wenye majukukumu).

Naomba kufahamishwa KISHERIA kama kichwa cha uzi kimavyojieleza.

Mi hivi, baada ya mgogoro wa ghafla sana (only 2 months now) na vurugu zilizofuata hapo, hatimae mke wangu ame file kesi mahakama ya mwanzo jii ya dai la talaka.

Nimepogiwa simu siku kadhaa zimepita sasa kitaarifiwa pia kitakiwa kuchukua wito "samansi" wa mahakama juu ya kesi husika na kweli nikachukua.

Charges ambazo nimekuta zimeainishwa ni kama 4 hivi ikiwemo
  • talaka
  • mgawanyo wa mali
  • matunzo ya watoto
  • kuishi na watoto

Sasa katika maisha yetu tulifanikiwa kijenga nyumba , kuwa na kiwanja pia usafiri ndio angalau kwa uchache vitu vya kueleweka.

Wazo langu mimi ni kwamba, sitaki habar za kugombania kitu na huyu mama ambaye mpaka sasa alishachukua watoto na kwenda kupanga mtaani.

Na mi pia nikaamua kuhamisha harakati zangu mkoani kulingana na nature ya shughul zangu.
Hivyo sina mpango wa kugombania mali wala chochote katika vyote tulivyo navyo.

Moja ya vipengele nimesoma kwenye hii samansi ya mahakama inasema "endapo mdaiwa /mlalamikiwa (mimi yani ) hatafika mahakamani , shauri litasomwa na kusikilizwa upande mmoja bila mimi kuwepo.

Sasa naomba kufahamu, kisheria kama nitaamua KUTOONEKANA mahakamani siku hiyo, je ,nitakua nimetemda UHALIFU ambao unaweza kunigharimu??

Naomba kusaidowa ufafanuzi.

Ahsanten
Hukumu itampendelea yeye.
 
Kwanini Unafanya Uamuzi wa kuacha Kila kitu?.

Kwanini wanaume wajinga huwa mnaamini Maisha ni kufumba na Kufumbua umetoboa?.

Kwanini wanaume wajinga ,Huwa mnafanya maamuzi ya ajabu sana?.

Unahisi huko ulikoenda kuanza Upya, Utafanikiwa?.

Kwamba Unahisi ukimuachia Kila kitu, Nawewe ukaenda kuanza Upya, siku ukifulia atakupokea?

Kama ambavyo Hana kitu lkn kaamua kutaka nusu ya Mali, vivovivo utakapofulia utakua Hauna Thaman yoyote kwako.

Wewe huwajui Wanawake, Wanawake hawajawah kupenda na hawatokaa wapende, WANAWAKE SIKU ZOTE HUMHESHIMU MWANAUME YOYOTE atakayepita machoni mwao na kuwafanyia wajihisi comfotaboooo.

Hapo upo ??

Jambo ambalo ulitakiwa kulipigania ni kuhakikisha JASHO LAKO HALIPOTEI BURE

Ona mtego ulipo, Anachukia Kila kitu, wewe ndo umeenda kujitafuta Upya, alafu bado UTAWAJIBIKA KWEMYE MATUNZO BILA KUJALI UNAJITAFUTA AU LAH!!.

NADHAN UMEROGWA, WALA USIDHAN NDIO UANAUME.

Mimi Sina Undugu na mwanamke, Undugu wangu ni watoto tu .
 
Nenda Mahakamani. Kataa Talaka kama Ni mkristo kisha omba mtengwe mjitafakari.

Au
Kubali Talaka
Kubali Mgawanyo wa Mali nusu kwa nusu
Sijui Umri wa watoto kama ni 7+ wachukue wewe wote itakusaidia kwenye matunzo

Au usiende mahakamani
Mahakama ivunje ndoa
Igawanye mali
Impe mwanamke watoto
Upewe garama za matunzo.

Je Mwanamke akiolewa tena papo kwa hapo sheria inasemaje?
 
Usipoenda mahakama itatoa maamuzi inaweza kuamua nyumba abaki nayo mke wako na upeleke pesa ya matumizi kila mwezi.

Sasa usipotekeleza baada ya hapo polisi watapewa Arrest warrant waje kukukamata kwa kudharau amri ya mahakama alaf utaenda kupumzishwa mahabusu gerezani siku kadhaa
 
Back
Top Bottom