Nina rafiki majambazi wezi sijui, walipofika nyumbani kwake, waka wanahangaika na mlango wa jikoni, hapo mlinzi walishampiga mapanga, R.I.P alifariki, rafiki akawa bize kupigia simu majirani, katika purukushani, mmoja wao wale wezi, akawaambia wenzake, siyo mlango huu ni ule mlango wa Mbele, wakaenda mlango wa Mbele, wanajua walichofanya, Ila mlango ulifunguka fasta Tu, wakaingia, wakakomba walivyoweza, DK 10 nyingi, majirani wakawa wameshaamshana, mmoja alikuwa na silaha akaipiga juu, wezi wakakimbia!
Nahisi wakati wa ujenzi. Kuna Kikundi cha mafundi au someone kwenye shughuli nzima anayewapa ramani!
Mpaka kesho hatukujua nini, Ila walibadili milango, na locks na makomeo yakaongezeka!