Nini njia ya kukomesha wizi huu majumbani?

Nini njia ya kukomesha wizi huu majumbani?

Mimi Nina siku mbili nimefanyiwa unyama, Ila Kuna dawa nawaandalia hawatakaa wasahau, mwanaume siwezi jipinda kitafuta wewe unakuja kuchukua kirahisi tu. Wacha niishie hapo
 
Matukio yamezidi kuongezeka sasa hivi ukilinganisha na wakati huo. Jitahidi kuelewa.
Huku mtaani wizi ulikithiri kipindi cga jpm kila siku nyumba zilikuwa zinasafishwa mwaka 2020 watu wakapanga mikakati

Wezi wawili walikamatwa na kupewa kisago kikali

Siku nyingine mwizi mwingine msumbufu alidakwa alipewa adhabu na pona yake aliwahi kuishi mtaani zamani tokea hapo hadi leo mtaani kuna ogopeka lkn naweza kukuambia nyumba lukuki zilikuwa zinasafishwa

Kwahyk kipindi cha jpm unataka kusema police walikuwa wanafanya patrol mitaani?

Kata nyingi sumbufu zilikuwa na sungusungu kwahio watu wakeshe kulinda mitaa yao credits apewe jpm tuliza header
 
Kufungua makufuli wanatumia viberiti vya gesi kuyaunguza makufuli yanaua spring ndogo ndani ya kufuli na kufunguka kwa urahisi pia wanatumia mitungi midogo ya gesi wakija wanalichoma kufuli lako ni dk sifuli limeachia.
 
Kama unaweza weka alam za maget na madirisha, kufuli labda zile za alarm,
 
Halafu wakichomwa moto watetezi wanaibuka msijichukulie Sheria mkononi, hali yenyewe ngumu halafu mtu anakusafisha
Police na Waendesha Mashitaka ndiyo tatizo! hawako serious sana kumaliza hayo matatizo ya wezi au ya kudhulumiana!!!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Kuna funguo fulani wanachongaga
Mafundi funguo.....wakishapata/jua
Kitasa chako au kufuli lako
Wao wanachonga funguo malay
Wakija kwako wanakuja na maufunguo kama askari magereza
Hawakukosi
Na uwizi huu wanafanya huko pembezoni mwa miji

Ova
Kuliko tulia,kwa watasha,hata Ulinzi shirikishi hawawezi kuweka maana wote wako busy na life!!!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Kufuli wanafungua bila shida
Ukiwa ndani weka bomba na lock zake hata kama watafanikiwa kufungua milango lakini hawataweza usukuma sababu ya kizuizi cha bomba kwa nyuma ya mlango labda wang'oe na frame yake kabisa kitu ambacho ni shughuli pevu.
Dawa za usingizi ni zile za hospital za nusu kaputi wakati wa operation ndizo wanapuliza dirisani Ili muibiwe bila maumivu, mida yao ya Kazi saa nane hadi kumi kamili.
 
Pia Wana kawaida ya kutengeneza urafiki na dada wa Kazi akiwa mpenzi wake anapelelezwa bila kujua nae ufunguka, kumbuka dada wa Kazi ni watu wenye stress akipata mtu anamtolea stress umpa ushirikino wote, pia hata akiondoka au ukibadili dada wa Kazi ukiweza badili na makufuli kabisa.
 
Wezi+Majambazi yamejaa hadi wanawake wapo kazini Polisi wamekua mchele mchele nowdays.
Police sio tatizo bali Jamii aiwapi police ushirikiano, police sio day care ya kuhifadhia wezi ukipeleka mwizi usipofatilia kesi wao wafanye nini sasa.
Labda tu iwepo sheria ukipelekwa kituoni zaidi ya mara tatu kwa kesi za wizi, mahakama ni hukumu tu miaka 7 pasipohitajika ushahidi unahukumiwa kwa tuhuma za mazoea.
Kwani police ni day care ya kukutunzia mwizi wako unampeleka kituoni then una mdamp ufatilii
 
Ni sawa wanaiba ILA HILI la kuwapa napanga na kuwachoma moto sio zuri mkimkamata pelekeni mahala husika sio kujichukulia sheria mkonon
Tatizo la mkimpeleka huko mahali husika kesho tu huyo kitaaani na matusi juu huku Wahusika wakisema Yuko nje kwa dhamana na upelelezi unaendelea na ukikamilika basi atafikishwa Mahakamani! Maisha yana songaa tukio hadi tukio!!!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Kufungua makufuli wanatumia viberiti vya gesi kuyaunguza makufuli yanaua spring ndogo ndani ya kufuli na kufunguka kwa urahisi pia wanatumia mitungi midogo ya gesi wakija wanalichoma kufuli lako ni dk sifuli limeachia.
Na vitasa pia?
 
Back
Top Bottom