Nini njia ya kukomesha wizi huu majumbani?

Nini njia ya kukomesha wizi huu majumbani?

Kuna funguo fulani wanachongaga
Mafundi funguo.....wakishapata/jua
Kitasa chako au kufuli lako
Wao wanachonga funguo malay
Wakija kwako wanakuja na maufunguo kama askari magereza
Hawakukosi
Na uwizi huu wanafanya huko pembezoni mwa miji

Ova
Wakishajua aina ya kufuli ndo wmeshua na aina ya fuunguo, kinachofuata ni kuja na lundo la funguo malaya za aina hiyo.

Njia nyingine wanayotumia ni unga wa baruti ya kununua au hata ya kiberiti tu, njia hii utakuta ule utumbo wa ndani ya kufuli uko nje! Ni wahuni sana'
 
Kwa taarifa yako funguo nyingi za milango ya grill zinaingiliana
Si zile komeo za grill na funguo wanauza 15000/25000 kama sikosei

Ova
Umenikumbusha mkuu, kipindi zile nyumba 300 za kisasa dodoma zilipokuwa zinajengwa funguo nyingi zilikuwa zinaingiliana tu! Yaani hata huwazi nichukue funguo gani! Mradi tu uwenazo 2&3 unauhakika zitafungua. Kipindi watu sio wengi mitaa ile nyumba zimesafishwa sana na waizi.
 
Misigiri ndani ndani huku😂😂😂😂

Ndanindani kitusha au ulemo?

Wezi hawana adabu. Walisafisha gari vifaa muhimu na iligharimu sana kujiweka sawa. Kama hautoshi baada ya wiki tatu wakaijia TV.

Nikipewa taarifa ya wizi jambo la kwanza nauliza nyie wote mko salama? Wakishajibu ndio, navuta shuka naendelea kuota.
 
Kwa taarifa yako funguo nyingi za milango ya grill zinaingiliana
Si zile komeo za grill na funguo wanauza 15000/25000 kama sikosei

Ova
funguo za grill zinaingiliana kweli,mi mlango wa ndani si wa grill ila ufunguo wake unafungua grill ya nje
 
Fungeni. CCTV cameras
Zinasaidiaje kudhibiti ujambaz/wizi wa ghafla? Mfano hao wanaotumia gesi kufungua makufuli, na wanaopuliza dawa za usingizi.. utaangalia kesho yake jinsi ulivyoibiwa na waliofunga nyuso kwa mask!
 
Wale jamaa ni wachawi ila pia wana tembea na kifaa Fulani kipo kama nondo au spoku wakigusa kwenye kofuli au kitasa kinaachia
 
Nina rafiki majambazi wezi sijui, walipofika nyumbani kwake, waka wanahangaika na mlango wa jikoni, hapo mlinzi walishampiga mapanga, R.I.P alifariki, rafiki akawa bize kupigia simu majirani, katika purukushani, mmoja wao wale wezi, akawaambia wenzake, siyo mlango huu ni ule mlango wa Mbele, wakaenda mlango wa Mbele, wanajua walichofanya, Ila mlango ulifunguka fasta Tu, wakaingia, wakakomba walivyoweza, DK 10 nyingi, majirani wakawa wameshaamshana, mmoja alikuwa na silaha akaipiga juu, wezi wakakimbia!

Nahisi wakati wa ujenzi. Kuna Kikundi cha mafundi au someone kwenye shughuli nzima anayewapa ramani!

Mpaka kesho hatukujua nini, Ila walibadili milango, na locks na makomeo yakaongezeka!
Mafundi karibia wote ni wezi wakiamua kukuchoma au wakiwekewa dau kubwa
Au wale wapuliza dawa sijui nini wote watoa ramani wale.
 
Kufuli halizuii mwizi kuiba, kufuli linachomwa na kiberiti cha gas, kisha linaachia
 
Tatizo la hizi adhabu za papo kwa papo ni namna ya kuthibitisha kama mnayemuua ndiye haswa ni Mwizi.

Mnaweza kukurupusha Wezi wakasepa alafu mkakutana na Jamaa katoka kwenye shughuli zake wala ahusiki na Wananchi tayari mihemuko ipo juu unafikiri atapona?.

Pana mtu wa jogging asubui tena ni daktari alfajiri aliwahi chomwa moto bila hatia kuhisiwa mwizi,wezi walikurupushwa wakakimbia uelekeo wa jamaa wa jogging bahati mbaya wakamuungia wizi, ikawa mwisho wake
 
Elewa mwizi ni shetani aliyevaa mwili wa binadamu. Kwa akili ya kawaida huwezi kuwa mwizi ni lazima uvae roho, thus wezi wote ni lazima wawe washirikina.
Mwizi hawezi Acha wizi kwa kipigo au kifungo ile ni roho.
Mwizi ni mtumwa yaani nafsi yake imeuzwa kwa shetani, nafsi yake ikirejeshwa huwa wanajutia Sana maisha ya wizi na huwa watu wema kwenye Jamii. Roho ya mwizi inaambukizwa inazaliwa na uzao wa wezi. Pana familia babu ni mwizi mstaafu, watoto wezi wajukuu wezi.
 
Elewa mwizi ni shetani aliyevaa mwili wa binadamu. Kwa akili ya kawaida huwezi kuwa mwizi ni lazima uvae roho, thus wezi wote ni lazima wawe washirikina.
Mwizi hawezi Acha wizi kwa kipigo au kifungo ile ni roho.
Mwizi ni mtumwa yaani nafsi yake imeuzwa kwa shetani, nafsi yake ikirejeshwa huwa wanajutia Sana maisha ya wizi na huwa watu wema kwenye Jamii. Roho ya mwizi inaambukizwa inazaliwa na uzao wa wezi. Pana familia babu ni mwizi mstaafu, watoto wezi wajukuu wezi.
Kuna Ka ukweli hapa, hii ni kaa laana inaenda vizazi na vizazi!
 
Mmeshauriwa camera mnaanza kuuliza humuhumu tena ooh bei gani kama Kuna duka hapa
Yapo madukani jamani
Kama mnaona ni gharama pia kununua Solex ya myahudi Basi weka gogo na kamba wakifungua tu linaondoka na mtu

Yaani ni kurudi enzi za The Flinstones sawa
 
Mimi wamebeba TV na laptop majuzi tena mchana. Dawa ziendeshwe operations za kura za siri kila mtaa alafu Polisi wachunguze wakisaidiana na viongozi wa mtaa. Wezi wanafahamika mitaani.
 
Mimi nilichotendwa na wezi aisee hata nikisikia mtaa flani huko Singida wamekamata mwizi niko radhi nipande Bus ili nikashiriki kumpiga japo naishi moro
 
Ukipata mwizi home kwako dawa yake ni hii chukua msumari wa nchi 4 gonja kichwani kwake mwachie aende zake tu
 
Niende moja kwa moja kwenye mada kama maeneo nayoishi kumekuwa na vitendo vya wizi mchana na usiku ila style wanayotumia wizi ni kama aina mpya flani kwani kama miezi miwili kuna wezi walivamia usiku kwenye duka la vifaa vya ujenzi na kuiba bila kuvunja grill yaani walifungua kufuli kama kwao vile.

Juzi tena kuna jirani mchana ametoka amefunga mlango pamoja na grill jamaa wakaenda wakafungua kama kwao na kubeba kila kitu walichotamani kubeba.

Usiku wa leo jamaa wameenda tena mtaa wa jirani wakafungua mlango bila kuvunja wakabeba Tv ,simu pamoja na pesa japo kwa maelezo yake anahisi walimpulizia dawa za kulala .

Hatua ya kwanza tumechukua ni kuaza kulala na majaba au mabeseni ya maji chumbani kwani inasemekana hata wakikupulizia dawa ya kulala haifanyi kazi (hatuna uhakika).
Ila kinachotupa shida wanawezaje kufungua milango na magrill bila kufunja wanatumia njia gani na njia gani ya kuweza kudhibiti wizi huu wa majumbani?
Kaka kwema,. ISECURE TECHNOLOGY tunaweza kukufungia GPS kwenye Tv yako. Hii GPS itakusaidia wakati umeibiwa unaweza kujua wezi wako wameelekea wapi na tv yako. hii ni ulinzi tosha kabisa
 
Back
Top Bottom