Nini njia ya kukomesha wizi huu majumbani?

Nini njia ya kukomesha wizi huu majumbani?

Dawa ni ukiwakamata unawafanyia kama jamaa wa kule uingereza maana aliwafungia ndani na kuwashugulikia ipasavyo

Ova
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ila wee jaman, khaaah
 
Kuna style nyingine,wanakuja kwako kama una bomba nje wanafungulia maji ,we ukitoka tu unao

Ila kikubwa ni kuimarisha ulinzi tu
Nyie wenyewe

Ova
Duuuh hali ni mbaya sana, mweeeeh
 
Kinachoniumizaga anakuibia kitu kikubwa chenye thamani anaenda kuuza bei ya nyanya,si heri angekuomba umpe hiyo hela.

Simu ya laki mbili anaenda kubadilishana na konyagi ndogo aisee.
Wanatia hasira sana hao viumbe.

Halaf bora wengine wakuibie kistaarabu basi... unakuta kipigo wanakupa na bado vitu vyako wanakuibia.
 
Niende moja kwa moja kwenye mada kama maeneo nayoishi kumekuwa na vitendo vya wizi mchana na usiku ila style wanayotumia wizi ni kama aina mpya flani kwani kama miezi miwili kuna wezi walivamia usiku kwenye duka la vifaa vya ujenzi na kuiba bila kuvunja grill yaani walifungua kufuli kama kwao vile.

Juzi tena kuna jirani mchana ametoka amefunga mlango pamoja na grill jamaa wakaenda wakafungua kama kwao na kubeba kila kitu walichotamani kubeba.

Usiku wa leo jamaa wameenda tena mtaa wa jirani wakafungua mlango bila kuvunja wakabeba Tv ,simu pamoja na pesa japo kwa maelezo yake anahisi walimpulizia dawa za kulala .

Hatua ya kwanza tumechukua ni kuaza kulala na majaba au mabeseni ya maji chumbani kwani inasemekana hata wakikupulizia dawa ya kulala haifanyi kazi (hatuna uhakika).
Ila kinachotupa shida wanawezaje kufungua milango na magrill bila kufunja wanatumia njia gani na njia gani ya kuweza kudhibiti wizi huu wa majumbani?
Fungeni. CCTV cameras
 
Ni sawa wanaiba ILA HILI la kuwapa napanga na kuwachoma moto sio zuri mkimkamata pelekeni mahala husika sio kujichukulia sheria mkonon
Ila wao wakitupiga mapanga ya kichwa ni sawa na mali wanakomba na pesa mpaka ya kujitibia wanakomba.
 
Angalia pia isije ikauwa familia yako au Jamaa zako!!? Mistake zipo! Mtego wa panya hata mendi aweza nasa!!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
True kuna mtu aliua mtoto wake,alitega umeme kwenye gari akasahau kuzima mchana, watoto wanacheza mpira umeingia uvunguni Mwa gari mtoto wake kaufuata uvunguni Mwa gari akapigwa short.
Umeme tega juu ya fence au juu ya paa uwapige shoti wachawi.
 
Back
Top Bottom