Nini sababu ya Matajiri wengi kutokuwa wakweli juu ya utajiri wao?

Mafanikio ni siri. ukishindwa kutunza siri, sahau kuhusu utajiri na mafanikio.
 
Mtu anaweza kuongeza chumvi lakini mimi nimeshuhudia Fundi Baiskeli hatimae akafungua Duka la Spea za Baiskeli baadae akawa analeta Baiskeli na sasa kahamia kwenye Pikipiki na ni Multi Milionea.
Hii Ina make sense Haina ubishi
Sio zile za nilianza na kuuza karanga ss Nina kampuni ya mabasi 🀣
 
Utajiri ni siri ya mtu binafsi , washamba ni wale wanaoenda kwenye semina za kufundishwa utajir.
 
Utajiri ni siri ya mtu binafsi , washamba ni wale wanaoenda kwenye semina za kufundishwa utajir.
Hapa wanapigwa wengi sana, wanalipia semina na vitabu wana nunua eti wapate
maarifa na siri ya kupata utajiri.
 
Nakumbuka nilianza kufunga karanga za elfu moja. Sasa namiliki vi eite 5.
 
Nakumbuka nilianza kufunga karanga za elfu moja. Sasa namiliki vi eite 5.
Mara ooh mimi nilikuwa na zungusha mchicha na matembele kwenye nyumba za watu na beseni kichwani, biashara imekuwa sasa napeleka nje ya nchi kwa ndege nimeweza kujenga ghorofa mjini kati.
 
Mwisho mzuri ni upi na mwisho mbaya ni upi mkuu?
 
Sio wao tu hata wewe kesho ukiwa mmoja wao hutasema kila kitu kwa sababu utajiri ni matokeo ya tabia ya mtu katika kumudu mambo makuu matatu
Mosi, Imani katika utendaji
Pili, Siri katika utendaji
Tatu, Nidhamu katika utendaji
 
Matajiri hasa hawa wa kibongo wengi wana msongo wa mawazo coz utajiri wao mwingi ni wa kutumia juju.
 
Huyo super feo wako unamjua vizuri?πŸ€”. au unataka tukwambie,....?
 
hiyo ni kawaida na ndo siri zenyewe,....tuna mfano mzuri, mdogo wake ROSTAM AZIZ kukutwa na hazina ya meno ya tembo na silaha nzito,....watu wanaona gas na hisa kumbe nyuma ni jangiri mkubwa,....huku kwetu miaka ya nyuma matajiri wengi walidhamini makundi ya ujambazi,...watu wanabomoa maduka ya jumla yale makubwa au magodown , kisha wanapeleka mzigo kwa tajiri ananunua kwa bei ndogo mno,...huku yeye akiwalinda dhidi ya sheria na kuwapa silaha,...kwasasa ,...ni dili za dollar na dhahabu kwenye black market,....wasomali,,(wasafiri harmu) ,...utakatishaji wa fedha za kifisadi,....ndo vinashika kasi sana,...
 

Yes ,siri ya utajiri anajua mwenye tajiri ,wengi hizi biashara tunazoziona front ni zuga tu ,ni kama kina Shamim zeze na mumewe ,kina niffer wanatundanganya walianza na mitaji ya elfu 10 na elfu 40 ni nonsense...Waweke wazi tu kwamba niliwezeshwa fungu na mtu fulani siyo mbaya appreciation zinakubalika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…