Nini sababu ya Matajiri wengi kutokuwa wakweli juu ya utajiri wao?

Wasalam wakuu,

Imekuwa ni jambo la kawaida matajiri wakihojiwa kuhusu utajiri wao utasikia anasema nilianza na baiskeli sasa
namiliki kampuni kubwa ya mabasi. Mwingine atasema nilianza mama ntilie leo namiliki hoteli kadhaa mjini, mwingine anasema nilianza kushona viatu ila sasa na miliki kiwanda cha viatu, mara nilianza na mtaji wa 20,0000 sasa nina billion 5.

Wanaeleza mambo kana kwamba ni mepesi sana na baadhi ya vijana wasio fikirisha akili yao vizuri wana chukua kama ilivyo wana hamasika wana enda kupambana bila mafanikio, matokeo yake wanakata tamaa zaidi. Jamani kama alivyo wahi sema Mh raisi mstaafu Jakaya Kikwete kwamba akili za kuambiwa changanya na za kwako hii ni muhimu sana.

Nyie mna mtizamo gani ndugu wanabodi.
Yule aliyekamatwa na Semi-trailer lenye Mabomba kumbe limejaa Wahamiaji haramu unadhani wanaweza kusema ukweli zaidi ya Kukwambia tu Biashara ya Bomba inalipa.
 
Mtu akisema alianza kwa kuuza karanga leo anamiliki kisiwa sio uongo kwamba halikuwa hauzi Karanga huenda alikuwa anauza na Bangi na Mirungi (sasa unataka akwambie kwamba na Mirungi aliuza) na kodi alikuwa halipi ?
Uko sahihi sana.

Nina Jamaa yangu( shemeji) alikuwa anauza Machungwa na matunda kwenye Troli.

Baadae akapata Pesa za Kafara akatajirika sana. Hii haikufuta ukweli kwamba aliuza machunga kwenye tenga.

Baadae masharti yalimshinda akafilisika. Ndio akasema ukweli kuwa Pesa zile zilikuwa za kichawi.
 
Mkuu uko sahihi kabisa ktk mada yako, bahati mbaya sana Jambo hili huo halitupiwi jicho la mashaka coz wahusika ni matajiri, so vijana wanabugia hayo matangopori bila hata kuzingatia kauli ya mstaafu mzee jakaya.
Hiki ndio kimepelekea vijana wengi wamedata kwa kukimbilia mali au kishabikia habari za uongo.

Mtu anakwambia kauza mayai akawa tajiri kwani Hayo mayai alikiwa anauza peke yake? nchi nzima Tajiri wa Mayai awe mmoja tu?
 
Ni kwa mkuu vijana wana babaishwa kifikra kwa sababu ya maneno yao. Mfano kama hawa akina Mwijaku na Babalevo kwamba wana miliki majumba ya billion kwa kufanya tu uchawa na baadhi ya watu wana amini.
 
Watu wanashindwa kutofautisha kati ya utajiri na kuyapatia maisha!

Kila mtu huyapatia maisha kipindi fulani Cha maisha yake!kubaki kwenye kilele hicho na kuendelea zaidi Hadi utajiri ndio kazi ilipo hapo!!

Kwanza ku maintain bila kushuka halafu kupanda kilele kufikia utajiri hapo ndipo majaaliwa ya Mungu au kulazimisha kwa kafara ya maisha Yako has uchawi na uganga!

Wengi TU tunajipata lakini baada ya kujipata unapigwa scard na shetani Hadi unaweza anguka anguko kuu!

Wengi tumewaona!
 
Mkuu uko sahihi kabisa ktk mada yako, bahati mbaya sana Jambo hili huo halitupiwi jicho la mashaka coz wahusika ni matajiri, so vijana wanabugia hayo matangopori bila hata kuzingatia kauli ya mstaafu mzee jakaya.
Kabisa mkuu
 
Hiki ndio kimepelekea vijana wengi wamedata kwa kukimbilia mali au kishabikia habari za uongo.

Mtu anakwambia kauza mayai akawa tajiri kwani Hayo mayai alikiwa anauza peke yake? nchi nzima Tajiri wa Mayai awe mmoja tu?
Kitu ambacho tumekosa ni fikra tunduizi ( Critical thinking) ndio maana watu wana danganywa kirahisi.

Chukulia mfano wa hawa manabii pia. Mtu anaambiwa pokea makontena toka China nae anaamini kuwa atapokea.
 
Wasalam wakuu,

Imekuwa ni jambo la kawaida matajiri wakihojiwa kuhusu utajiri wao utasikia anasema nilianza na baiskeli sasa
namiliki kampuni kubwa ya mabasi. Mwingine atasema nilianza mama ntilie leo namiliki hoteli kadhaa mjini, mwingine anasema nilianza kushona viatu ila sasa na miliki kiwanda cha viatu, mara nilianza na mtaji wa 20,0000 sasa nina billion 5.

Wanaeleza mambo kana kwamba ni mepesi sana na baadhi ya vijana wasio fikirisha akili yao vizuri wana chukua kama ilivyo wana hamasika wana enda kupambana bila mafanikio, matokeo yake wanakata tamaa zaidi. Jamani kama alivyo wahi sema Mh raisi mstaafu Jakaya Kikwete kwamba akili za kuambiwa changanya na za kwako hii ni muhimu sana.

Nyie mna mtizamo gani ndugu wanabodi.
Kwanini nchi hii watu mnachuki na watu waliofanikiwa ni lini nchi ilikuwa tajiri kwanini hamtaki kuamini walianza kuuza karanga mpaka kutajirika ni kama vile darasa ni Moja lakini wapo wachache wanapata div 1 na wengine wanapata div 0 hilo linawezekana kabisa
 
Back
Top Bottom