Nini sababu ya mikoa ya Kusini kuwa salama sana kibinadamu?

Ni kweli na katika hilo napongeza japo nawapinga vikali waliosema sababu ni dini

Mimi ni mmoja kati ya watu niliyeleta mpaka nyuzi humu kuonesha huku wana tabia za tofauti (mbaya) sana ukilinganisha na sehemu nyingine.

Kuhusu dini ni kweli unakuta kijiji 99% ni waislamu lakini ni waislamu jina. Kuhusu hayo uliyoyasema yapo lakini kwa kiwango kidogo sana na (binafsi) huwa najiulizaga sana kwanini?

Yaani kwa amani na uhuru wa kuishi huku ni namba moja... mfano msimu ukiingia watu wanaenda kuchomoa pesa benki wanabeba kwenye mabegi kienyeji lakini mpaka msimu unaisha unasikia kalizwa pengine mmoja tu yaani hadi huwa nashangaa



Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Niliwahi kwenda huko nikiwa sina ndugu wala rafiki ila wale watu ni waungwana mno wana madhaifu mengine ila huko ni sehemu salama kuishi na kuolewa/kuoa huwezi chinjwa kikatili
Karibu mtwara bi Nuzulati ..Kama hautojali
 
Hapo lindi full ushirikina
 
Huku Bado tunaishi maisha ya ujamaa tena pure socialism na dini kiasi ..huku hakuna kujiua au kuuana kisa mapenzi...wapenzi/wanandoa wakichokana Ni kuachana tu maisha yaendelee..
Huku watu sio wabinafsi km Arusha au Kilimanjaro watu hawana hulka na Mali..
Huku Ni kawaida Sana mzazi kukuozesha mwanae bure kabsa au mahari kidogo tu
 
Hakuna mambo ya hivi mkuu.Watu wakusini(Pwani ya kusini)ni wastarabu sana na wakarimu.
 
Unaanzaje kumuonea wivu mwanamke wa kimakonde?
Vifupi, sura imekoma na hawana shepu. Nishafika Mtwara na Lindi
Nyumba za kizamani bora hata Masasi kuna nyumba mpya
Cha kushangaza kutoka Dar mpk Mtwara 23,000
Dar to Lindi 23,000
Dar to Masasi 23,000
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…