Nini tafsiri ya Megawatts 2,115 za umeme wa bwawa la Mwalimu Nyerere (Stiegler's Gorge)?

Nini tafsiri ya Megawatts 2,115 za umeme wa bwawa la Mwalimu Nyerere (Stiegler's Gorge)?

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
NINI TAFSIRI YA MEGAWATTS 2,115 ZA UMEME WA BWAWA LA MWALIMU NYERERE (Stiglers Gorge)?

Wengi tunaona na kusikia kuhusu habari ya utekelezaji wa mradi mkubwa wa uzalishaji umeme wa maji wa Megawatts 2115 kutoka kwenye Mto Rufiji, mradi uliobuniwa na Mwalimu Nyerere toka mwaka 1975 na sasa unatekelezwa na Rais wa awamu ya 5 Dkt John Pombe Magufuli.

Tumesikia habari ya ukubwa wake huo mradi, gharama ya utekelezaji wa mradi wenyewe, umeme unaoenda kuzalishwa na mambo mengine mengi sana kuuhusu mradi huo wa Stieglers Gorge (Bwawa la Mwalimu Nyerere). Sasa leo ngoja tuumulike kidogo mradi huu wa umeme, tujue idadi ya namba zilizoko za gharama na Megawatts zinazoenda kuzalishwa hapo na tafsili yake kwa Watanzania na uchumi wetu.

Kwanza kuingia kwa Serikali ya awamu ya 5 kulifungua ukurasa mpya wa utekelezaji wa maono ya Baba wa Taifa ya toka mwaka 1975 ya kutaka kuzalisha umeme kwenye bonde la Mto Rufiji kupitia mradi huo mkubwa kabisa namba 4 wa uzalishaji wa umeme barani Afrika unaoenda kuzalisha Megawatts 2115 kwa gharama ya Trillion 6.5 tena kwa fedha zetu za ndani.

Adhima ya utekelezaji wa mradi huo inakuja wakati nchi ikiwa kwenye ujenzi wa uchumi wa viwanda ambao kwa kiwango kikubwa unategemea sana nishati umeme ya kuwezesha viwanda kupata nishati ya kutosha ili iweze kuzalisha vya kutosha na muhimu kwa gharama nafuu. Viwanda ni umeme na umeme ni viwanda.

Lakini licha ya yote ni wangapi tunaelewa tafsiri halisi ya Megawatts 2,115 za umeme zinazoenda kuzalishwa pale Mto Rufiji? kwa sisi watu wa kawaida ambao si wataalamu wala wahandisi tunaelewa nini kuhusu Megawatts 2115? twende sawa hapo chini.

Kuzielewa Megawatts 2115 na ukubwa wake ni rahisi ukipitia na kujua matumizi ya umeme na mahitaji ya umeme kwa taifa letu. Mfano mwepesi tu ni kwamba mahitaji halisi ya umeme kwa mikoa kama ya Mtwara na Lindi ili umeme usikatike hata sekunde ni Megawatts 22 hadi 30 tu, ina maana katika zile Megawatts 2,115 tunakuwa na chenji kama ya Megawatts 2,085.

Tanzania ina Mikoa 31, hivyo ukifanya kila mkoa upate Megawatts 50 tu kama makadirio ya juu kabisa hata kwa mikoa isiyozidi matumizi hayo maana yake ni sawa na kupeleka bahari ya umeme kila mkoa na bado matumizi tutaishia Megawatts 1,550 na bado zitabaki Megawatts 565 kama akiba ya umeme tuliyoiweka kibindoni. Bado hiyo Megawatts 50 kiwastani hata ukijumlisha mikoa yenye viwanda vingi na vikubwa kama Pwani, Dar es Salaam, Arusha, Tanga na Mwanza bado ni kubwa sana. Nimeweka kwa kiwango cha Juu saana usisahau matumizi ya Mtwara na Lindi ni Megawatts 22- 30 tu.

Ina maana hapo tunaenda kuua kabisa stori za mgao wa umeme na mambo ya umeme kukatikakatika. Hapo wenye viwanda vikubwa, vya kati na vidogo kabisa watazalisha bidhaa zao bila tatizo na zaidi kwa gharama nafuu kutegemea na urahisi wa gharama kwa umeme wa maji.

Umeme wa Kinyerezi ambao ndiyo tunaojivunia kwa sasa kuwa ni mradi mkubwa wa umeme kiwango chake cha mwisho cha kuzalisha umeme ni Megawatts 1,560 tu ina maana Bwawa la Mwalimu Nyerere pekee yake linaenda kutupa umeme wa uhakika tena wa maji ambao ni rahisi zaidi kuliko aina yoyote ile ya umeme duniani ukiachana na wa jua, upepo, nyuklia, makaa ya mawe, mafuta na gesi.

Tukumbuke umeme unaozalishwa na maji ndio umeme wa gharama nafuu na rahisi zaidi kuliko umeme wowote ule duniani. Kumbuka uniti 1 inayozalishwa na maji ni shilingi 36 tu wakati umeme wa nyuklia ni shilingi 65 kwa uniti, umeme wa jua shilingi 103.05, upepo 103.05, makaa ya mawe 118, gesi asilia 147 na mafuta ni 426. Hivyo tunaenda kushusha maradufu bei ya umeme kwa watumiaji hivyo kuhimili mfumuko wa bei wa bidhaa za viwandani.

Hii tafsili yake kukamilika tu kwa Bwawa la uzalishaji wa umeme la Mwalimu Nyerere kutashusha kwa kiwango kikubwa sana gharama ya umeme mpaka shilingi 36 tu kwa uniti hivyo kutoa nafasi kwa bidhaa zetu za viwanda nazo kushuka sana. Hapo mpaka kwenye matumizi ya kawaida nyumbani yatashuka na hata kwa watanzania watakaofungua viwanda vidogo kwa vikubwa watanufaika sana na gharama ndogo ya uzalishaji wa bidhaa itakayoleta neema na nafuu mpaka kwa sisi watu wa hali ya chini kabisa, machinga, mama nitilie, wajasiriamali na makundi mengine.

Unapokuwa na umeme wa uhakika, lakini sio wa uhakika tu tena na wa gharama nafuu ya bei tayali unavutia wawekezaji wengi zaidi kuja kujenga viwanda hapahapa. Suala la uhakika wa umeme na nafuu yake ni mambo ya msingi sana kwa mwekezaji anayefikiri kwenda kuwekeza sehemu yoyote ile kwasababu kiwanda ni nishati.

Vipi umefikilia hizo Megawatts zingine zaidi ya 565 ambazo tunakuwa tumezitia kibindoni baada kujihakikishia uhakika wa umeme nchi nzima? hapo tunaweza kuamua kuuza kwa majirani zetu hapo Kenya, Malawi, Uganda au Msumbiji ambako tunajua bado hawana uhakika wa umeme. Hapo unazungumza kuhusu umeme wa Rufiji tu, hujaenda Kinyerezi, Kidatu, Mtera, Nyumba ya Mungu na kwingine ambako umeme unaendelea kuzalishwa.

Rais Magufuli na Serikali yake baada ya kugundua hatuna umeme wa kutosha na wenye bei nafuu kwa wananchi wake ndiyo ikaja na suluhisho hilo la Bwawa la Mwalimu Nyerere. Nini tena sasa? Tusiposema sisi kwa haya yanayofanyika basi hata mawe yatapiga kelele siku moja.
IMG-20201008-WA0359.jpg
 
Asante sana, uchambuzi maridhawa kabisa , Sasa naomba uchambue kuhusu gesi, tuliaminishwa hivyo hivyo.
Shida ya kwenye gas, ni kwamba badala ya kuweka gas turbines sehemu zote zenye majenereta, wao wameweka mashine zinazochoma gas kama unavyochoma petroli. Gharama ingekuwa rahisi kidogo kwa turbines kuliko ilivyo sasa. Kama kwenye maji, baada ya turnine, tungekuwa bado tuna gas kwa matumizi mengine.
 
Bei ya umeme ikishushwa itawezesha hata kilimo cha umwagiliaji pakubwa sana.
 
Kwa nyongeza zaidi kitakwimu, kwa wale maTomaso, wanaobeza kuwa huo mradi ni maendeleo ya vitu, mimi natumia wastani wa unit 420 kwa mwezi wa gharama ~ 150,000/-.

Umeme wa Bwawa la Nyerere ukikamilika nitakuwa nalipa chini ya 20000/- kwa mwezi. Hii ina maana nitakuwa na salio la 130,000/- ambayo nitaitumia kwa maendeleo yangu (mtu).

Hiki ni kiasi cha 1,560,000/- kwa mwaka ambacho si haba maana kinatosheleza kwa elimu ya watoto/wajukuu wangu (maendeleo ya watu) au kulipia bima ya afya (maendeleo ya mtu), na kadhalika
 
Asante sana, uchambuzi maridhawa kabisa , Sasa naomba uchambue kuhusu gesi, tuliaminishwa hivyo hivyo.
Ok, soon utaupata uchambuzi. Hii ni baadhi ya mitambo ya gesi asilia (Methane) inayopatikana Tabata Kinyerezi inayopokea gesi asilia kutoka Madimba Natural Gas pPocessing Plant, Mtwara na Songosongo, Lindi.

Gesi asilia imeshaanza kutumika maeneo mengi mkoani mtwara na Lindi na Dar es salaam ikiwa ni pamoja na Serena Hotel, kiwanda cha saruji cha Dangote. Lakini pia mfumo wa Magari yanayotumia gesi asilia yaana CNG - Compressed Natural Gas upo pale DIT na magari mengi yanatumia mfumo wa CNG. CNG inatumia gharama ndogo sana ukilinganisha na diesel au petrol.

Mfumo huu wa CNG hauondoi mfumo wa zamani wa gari yako kutumia diesel au petrol isipokuwa unakuwa na mifumo yote na unachagua kwa wakati huu utumie upi.
 

Attachments

  • IMG-20201012-WA0048.jpg
    IMG-20201012-WA0048.jpg
    152.2 KB · Views: 3
  • IMG-20201012-WA0067.jpg
    IMG-20201012-WA0067.jpg
    125.9 KB · Views: 3
  • IMG-20201012-WA0059.jpg
    IMG-20201012-WA0059.jpg
    124.8 KB · Views: 3
  • IMG-20201012-WA0058.jpg
    IMG-20201012-WA0058.jpg
    114.4 KB · Views: 3
Mkuu huu uchambuzi wako ni wa kisiasa zaidi sio kitaalam Kwa sababu zifuatazo:-

1. Mikoa uliotolea mfano wako hawana matumizi ya umeme kabisa Kwa kuwa hawlkuna viwanda vingi wala migodi.
2. Wananchi wa mikoa hiyo wengi ni maskini na hawana umeme na matumizi Yao mengi ni kuwasha taa.
3. Jenho moja kubwa hapa Dar kama Viva tower au Mkapa tower lina matumizi sawa na mkoa wa Lindi.
4. Mgodi wa madini kama Bulyankulu unaweza kutumia Hadi megawat 300 au zaidi.
Hivyo mkuu wangu hizo hesabu zako zina ukakasi tu.
 
..wachumi wana msemo wao wanasema, " CETERIS PARIBUS. "

..maana yake ni all other FACTORS remaining constant.

..sasa ni kweli kwamba gharama umeme wa maji, ceteris paribus, ni ndongo kuliko umeme wa vyanzo vingine.

..lakini kwa hapa Tz siyo kweli kwamba factors zote zitakuwa constant.

..Kwa mfano kama tumechukua MKOPO WA KIFISADI kwa ajili ya ujenzi wa mradi basi umeme utakaozalishw utakuwa wa gharama zaidi.

..Kama hatukuzingatia taarifa za mazingira kabla hatujaanza ujenzi basi tutaingia gharama wakati wa uendeshaji wa mradi.

..Kama tukishindwa kutunza mazingira ktk VYANZO VYA MAJI ktk mradi huo gharama zitaongezeka.

..Kama tuna miradi mingine mibaya isiyo na ufanisi ya kuzalisha umeme, then bei ya umeme kwa ujumla itaathirika.

..Stieglers gorge sio mradi wa kwanza wa umeme wa maji hapa nchini. Tayari tuna miradi kama Kidatu, Mtera, Pangani, etc etc lakini nayo ina changamoto zake.
 
Kwa nyongeza zaidi kitakwimu, kwa wale maTomaso, wanaobeza kuwa huo mradi ni maendeleo ya vitu, mimi natumia wastani wa unit 420 kwa mwezi wa gharama ~ 150,000/-. Umeme wa Bwawa la Nyerere ukikamilika nitakuwa nalipa chini ya 20000/- kwa mwezi. Hii ina maana nitakuwa na salio la 130,000/- ambayo nitaitumia kwa maendeleo yangu (mtu). Hiki ni kiasi cha 1,560,000/- kwa mwaka ambacho si haba maana kinatosheleza kwa elimu ya watoto/wajukuu wangu (maendeleo ya watu) au kulipia bima ya afya (maendeleo ya mtu), na kadhalika
Bwala la Ethipia lilichukua miaka mimgapi
 
Story tu hizo mpaka siku nitakapoanza kuhutumia ndio nitaamini
 
Kwa nyongeza zaidi kitakwimu, kwa wale maTomaso, wanaobeza kuwa huo mradi ni maendeleo ya vitu, mimi natumia wastani wa unit 420 kwa mwezi wa gharama ~ 150,000/-. Umeme wa Bwawa la Nyerere ukikamilika nitakuwa nalipa chini ya 20000/- kwa mwezi. Hii ina maana nitakuwa na salio la 130,000/- ambayo nitaitumia kwa maendeleo yangu (mtu). Hiki ni kiasi cha 1,560,000/- kwa mwaka ambacho si haba maana kinatosheleza kwa elimu ya watoto/wajukuu wangu (maendeleo ya watu) au kulipia bima ya afya (maendeleo ya mtu), na kadhalika
Future impossible tense.
Sasa hivi tunanunua unit sh ngapi wakati tunatumia gas na maji.
 
Back
Top Bottom