Umeme wa maji ndio wenye gharama ndogo kushinda umeme wa aina yoyote duniani hata marekani wana mabwawa mengi ya kuzalishia umeme fuatilia utaona, gesi uzalishaji wake ni gharama kubwa.Mataga umechanganyikiwa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umeme wa maji ndio wenye gharama ndogo kushinda umeme wa aina yoyote duniani hata marekani wana mabwawa mengi ya kuzalishia umeme fuatilia utaona, gesi uzalishaji wake ni gharama kubwa.Mataga umechanganyikiwa
Ana mashine ya kusaga nyumbani mkuu usishangaeWastani wa unit 14 kila siku, si mchezo.
Jukwaa pana sana hili. Tumo wenye maisha tofauti tofauti sana. Unit 4 kwa siku kwangu naona bado ni nyingi.Ana mashine ya kusaga nyumbani mkuu usishangae
Ya kupikia yenyewe ni changamotoAnza hata leo gesi asilia kwenye gari lako
Wewe na elimu yako umechambua wapi wataalamu wa tz mnajua kukosoa zaidi kuliko kuplan na kuvumbua ?Electrical engineering analysis inafanywa kisiasa jukwaani hapa huo uliofanya ni uhuni na kudharau taaluma zetu tuliokaa darasani 4 years
Inawezekana darasani ukikaa kupasha kiti moto tu, toa na wewe modalities zako tuone utopolo ulio kichwani kwako.Electrical engineering analysis inafanywa kisiasa jukwaani hapa huo uliofanya ni uhuni na kudharau taaluma zetu tuliokaa darasani 4 years
For how long can that dam supply 2115 MW in a year? (I am asking maximum water holding period), Because here is where enguneerig starts..NINI TAFSIRI YA MEGAWATTS 2,115 ZA UMEME WA BWAWA LA MWALIMU NYERERE (Stiglers Gorge)?
Wengi tunaona na kusikia kuhusu habari ya utekelezaji wa mradi mkubwa wa uzalishaji umeme wa maji wa Megawatts 2115 kutoka kwenye Mto Rufiji, mradi uliobuniwa na Mwalimu Nyerere toka mwaka 1975 na sasa unatekelezwa na Rais wa awamu ya 5 Dkt John Pombe Magufuli.
Tumesikia habari ya ukubwa wake huo mradi, gharama ya utekelezaji wa mradi wenyewe, umeme unaoenda kuzalishwa na mambo mengine mengi sana kuuhusu mradi huo wa Stieglers Gorge (Bwawa la Mwalimu Nyerere). Sasa leo ngoja tuumulike kidogo mradi huu wa umeme, tujue idadi ya namba zilizoko za gharama na Megawatts zinazoenda kuzalishwa hapo na tafsili yake kwa Watanzania na uchumi wetu.
Kwanza kuingia kwa Serikali ya awamu ya 5 kulifungua ukurasa mpya wa utekelezaji wa maono ya Baba wa Taifa ya toka mwaka 1975 ya kutaka kuzalisha umeme kwenye bonde la Mto Rufiji kupitia mradi huo mkubwa kabisa namba 4 wa uzalishaji wa umeme barani Afrika unaoenda kuzalisha Megawatts 2115 kwa gharama ya Trillion 6.5 tena kwa fedha zetu za ndani.
Adhima ya utekelezaji wa mradi huo inakuja wakati nchi ikiwa kwenye ujenzi wa uchumi wa viwanda ambao kwa kiwango kikubwa unategemea sana nishati umeme ya kuwezesha viwanda kupata nishati ya kutosha ili iweze kuzalisha vya kutosha na muhimu kwa gharama nafuu. Viwanda ni umeme na umeme ni viwanda.
Lakini licha ya yote ni wangapi tunaelewa tafsiri halisi ya Megawatts 2,115 za umeme zinazoenda kuzalishwa pale Mto Rufiji? kwa sisi watu wa kawaida ambao si wataalamu wala wahandisi tunaelewa nini kuhusu Megawatts 2115? twende sawa hapo chini.
Kuzielewa Megawatts 2115 na ukubwa wake ni rahisi ukipitia na kujua matumizi ya umeme na mahitaji ya umeme kwa taifa letu. Mfano mwepesi tu ni kwamba mahitaji halisi ya umeme kwa mikoa kama ya Mtwara na Lindi ili umeme usikatike hata sekunde ni Megawatts 22 hadi 30 tu, ina maana katika zile Megawatts 2,115 tunakuwa na chenji kama ya Megawatts 2,085.
Tanzania ina Mikoa 31, hivyo ukifanya kila mkoa upate Megawatts 50 tu kama makadirio ya juu kabisa hata kwa mikoa isiyozidi matumizi hayo maana yake ni sawa na kupeleka bahari ya umeme kila mkoa na bado matumizi tutaishia Megawatts 1,550 na bado zitabaki Megawatts 565 kama akiba ya umeme tuliyoiweka kibindoni. Bado hiyo Megawatts 50 kiwastani hata ukijumlisha mikoa yenye viwanda vingi na vikubwa kama Pwani, Dar es Salaam, Arusha, Tanga na Mwanza bado ni kubwa sana. Nimeweka kwa kiwango cha Juu saana usisahau matumizi ya Mtwara na Lindi ni Megawatts 22- 30 tu.
Ina maana hapo tunaenda kuua kabisa stori za mgao wa umeme na mambo ya umeme kukatikakatika. Hapo wenye viwanda vikubwa, vya kati na vidogo kabisa watazalisha bidhaa zao bila tatizo na zaidi kwa gharama nafuu kutegemea na urahisi wa gharama kwa umeme wa maji.
Umeme wa Kinyerezi ambao ndiyo tunaojivunia kwa sasa kuwa ni mradi mkubwa wa umeme kiwango chake cha mwisho cha kuzalisha umeme ni Megawatts 1,560 tu ina maana Bwawa la Mwalimu Nyerere pekee yake linaenda kutupa umeme wa uhakika tena wa maji ambao ni rahisi zaidi kuliko aina yoyote ile ya umeme duniani ukiachana na wa jua, upepo, nyuklia, makaa ya mawe, mafuta na gesi.
Tukumbuke umeme unaozalishwa na maji ndio umeme wa gharama nafuu na rahisi zaidi kuliko umeme wowote ule duniani. Kumbuka uniti 1 inayozalishwa na maji ni shilingi 36 tu wakati umeme wa nyuklia ni shilingi 65 kwa uniti, umeme wa jua shilingi 103.05, upepo 103.05, makaa ya mawe 118, gesi asilia 147 na mafuta ni 426. Hivyo tunaenda kushusha maradufu bei ya umeme kwa watumiaji hivyo kuhimili mfumuko wa bei wa bidhaa za viwandani.
Hii tafsili yake kukamilika tu kwa Bwawa la uzalishaji wa umeme la Mwalimu Nyerere kutashusha kwa kiwango kikubwa sana gharama ya umeme mpaka shilingi 36 tu kwa uniti hivyo kutoa nafasi kwa bidhaa zetu za viwanda nazo kushuka sana. Hapo mpaka kwenye matumizi ya kawaida nyumbani yatashuka na hata kwa watanzania watakaofungua viwanda vidogo kwa vikubwa watanufaika sana na gharama ndogo ya uzalishaji wa bidhaa itakayoleta neema na nafuu mpaka kwa sisi watu wa hali ya chini kabisa, machinga, mama nitilie, wajasiriamali na makundi mengine.
Unapokuwa na umeme wa uhakika, lakini sio wa uhakika tu tena na wa gharama nafuu ya bei tayali unavutia wawekezaji wengi zaidi kuja kujenga viwanda hapahapa. Suala la uhakika wa umeme na nafuu yake ni mambo ya msingi sana kwa mwekezaji anayefikiri kwenda kuwekeza sehemu yoyote ile kwasababu kiwanda ni nishati.
Vipi umefikilia hizo Megawatts zingine zaidi ya 565 ambazo tunakuwa tumezitia kibindoni baada kujihakikishia uhakika wa umeme nchi nzima? hapo tunaweza kuamua kuuza kwa majirani zetu hapo Kenya, Malawi, Uganda au Msumbiji ambako tunajua bado hawana uhakika wa umeme. Hapo unazungumza kuhusu umeme wa Rufiji tu, hujaenda Kinyerezi, Kidatu, Mtera, Nyumba ya Mungu na kwingine ambako umeme unaendelea kuzalishwa.
Rais Magufuli na Serikali yake baada ya kugundua hatuna umeme wa kutosha na wenye bei nafuu kwa wananchi wake ndiyo ikaja na suluhisho hilo la Bwawa la Mwalimu Nyerere. Nini tena sasa? Tusiposema sisi kwa haya yanayofanyika basi hata mawe yatapiga kelele siku moja.View attachment 1597580
Ita supply continuously kwa sababu hakuna limit ya water flow and it will depend na ENVIRONMENTAL CONSERVATION itakavyokuwa.For how long can that dam supply 2115 MW in a year? (I am asking maximum water holding period), Because here is where enguneerig starts..
Mbona unaanza matusi?.Inawezekana darasani ukikaa kupasha kiti moto tu, toa na wewe modalities zako tuone utopolo ulio kichwani kwako.
Hapana ndugu, ya kupikia ni nyingi sana.Ya kupikia yenyewe ni changamoto
Bei ya umeme kuwa juu, ina husika vipi na kilimo cha umwagiliaji kuwa juu?? Naomba ufafanuzi hapo!!!Bei ya umeme ikishushwa itawezesha hata kilimo cha umwagiliaji pakubwa sana.
Ili kuweza kuibadili gas Yetu iwe katika kimiminika na kusafirishwa kwa njia ya mitungi, Project inaweza kugharimu kiasi gani cha fedha? Kwasababu hili likiwezekana ni hakika tutaifaidi Gas hii maradufuHapana ndugu, ya kupikia ni nyingi sana.
kwa sasa Tanzania tunatumia LPG - Liquified Petroleum Gas, yaani ni Petroleum or Gasoline inakuwa converted into gas. Hii ni tofauti na Natural Gas (Methane, CH4) ambayo hii inaweza kutumika kama gas ya kupikia na kwenye magari as FUEL. Na mpango wa TPDC kupitia GASCO -Gas Supply Company wanafanya Project ya DOWNSTREAM kwa ameneo mengi ya Dar es salaam kama masaki, mikocheni na maeneo mengine kuunganisha pipe za gas kwenye nyumba za watu kwa matumizi ya nyumbani.
I remember to have read similar arguments kama hii, ambayo pia Lissu na mabeberu wengi wamekuwa wakizitumia kupinga mradi huo wa Rufiji ikiwa ni pamoja na uharibifu wa mazingira na kutumia vibaya Mbuga ya Selous! What a joke!..wachumi wana msemo wao wanasema, " CETERIS PARIBUS. "
..maana yake ni all other FACTORS remaining constant.
..sasa ni kweli kwamba gharama umeme wa maji, ceteris paribus, ni ndongo kuliko umeme wa vyanzo vingine.
..lakini kwa hapa Tz siyo kweli kwamba factors zote zitakuwa constant.
..Kwa mfano kama tumechukua MKOPO WA KIFISADI kwa ajili ya ujenzi wa mradi basi umeme utakaozalishw utakuwa wa gharama zaidi.
..Kama hatukuzingatia taarifa za mazingira kabla hatujaanza ujenzi basi tutaingia gharama wakati wa uendeshaji wa mradi.
..Kama tukishindwa kutunza mazingira ktk VYANZO VYA MAJI ktk mradi huo gharama zitaongezeka.
..Kama tuna miradi mingine mibaya isiyo na ufanisi ya kuzalisha umeme, then bei ya umeme kwa ujumla itaathirika.
..Stieglers gorge sio mradi wa kwanza wa umeme wa maji hapa nchini. Tayari tuna miradi kama Kidatu, Mtera, Pangani, etc etc lakini nayo ina changamoto zake.
Kuna micro irrigation schemes kibao hapa kanda ya kati zinazotumia umeme kusukuma maji toka visimani kujaza kwenye matanki kisha kumwagilia mazao. Hizo ndizo zinazoathiriwa na bei ya umeme kuwa juu.Bei ya umeme kuwa juu, ina husika vipi na kilimo cha umwagiliaji kuwa juu?? Naomba ufafanuzi hapo!!!
Sasa naomba unieleweshe Kama tutauza hizo megawatts 500 ...tutajuaje Kama ni megawatts 500 zimeenda huko...je hawatakula nyingi tukajikuta tuko kwenye shida tena?NINI TAFSIRI YA MEGAWATTS 2,115 ZA UMEME WA BWAWA LA MWALIMU NYERERE (Stiglers Gorge)?
Wengi tunaona na kusikia kuhusu habari ya utekelezaji wa mradi mkubwa wa uzalishaji umeme wa maji wa Megawatts 2115 kutoka kwenye Mto Rufiji, mradi uliobuniwa na Mwalimu Nyerere toka mwaka 1975 na sasa unatekelezwa na Rais wa awamu ya 5 Dkt John Pombe Magufuli.
Tumesikia habari ya ukubwa wake huo mradi, gharama ya utekelezaji wa mradi wenyewe, umeme unaoenda kuzalishwa na mambo mengine mengi sana kuuhusu mradi huo wa Stieglers Gorge (Bwawa la Mwalimu Nyerere). Sasa leo ngoja tuumulike kidogo mradi huu wa umeme, tujue idadi ya namba zilizoko za gharama na Megawatts zinazoenda kuzalishwa hapo na tafsili yake kwa Watanzania na uchumi wetu.
Kwanza kuingia kwa Serikali ya awamu ya 5 kulifungua ukurasa mpya wa utekelezaji wa maono ya Baba wa Taifa ya toka mwaka 1975 ya kutaka kuzalisha umeme kwenye bonde la Mto Rufiji kupitia mradi huo mkubwa kabisa namba 4 wa uzalishaji wa umeme barani Afrika unaoenda kuzalisha Megawatts 2115 kwa gharama ya Trillion 6.5 tena kwa fedha zetu za ndani.
Adhima ya utekelezaji wa mradi huo inakuja wakati nchi ikiwa kwenye ujenzi wa uchumi wa viwanda ambao kwa kiwango kikubwa unategemea sana nishati umeme ya kuwezesha viwanda kupata nishati ya kutosha ili iweze kuzalisha vya kutosha na muhimu kwa gharama nafuu. Viwanda ni umeme na umeme ni viwanda.
Lakini licha ya yote ni wangapi tunaelewa tafsiri halisi ya Megawatts 2,115 za umeme zinazoenda kuzalishwa pale Mto Rufiji? kwa sisi watu wa kawaida ambao si wataalamu wala wahandisi tunaelewa nini kuhusu Megawatts 2115? twende sawa hapo chini.
Kuzielewa Megawatts 2115 na ukubwa wake ni rahisi ukipitia na kujua matumizi ya umeme na mahitaji ya umeme kwa taifa letu. Mfano mwepesi tu ni kwamba mahitaji halisi ya umeme kwa mikoa kama ya Mtwara na Lindi ili umeme usikatike hata sekunde ni Megawatts 22 hadi 30 tu, ina maana katika zile Megawatts 2,115 tunakuwa na chenji kama ya Megawatts 2,085.
Tanzania ina Mikoa 31, hivyo ukifanya kila mkoa upate Megawatts 50 tu kama makadirio ya juu kabisa hata kwa mikoa isiyozidi matumizi hayo maana yake ni sawa na kupeleka bahari ya umeme kila mkoa na bado matumizi tutaishia Megawatts 1,550 na bado zitabaki Megawatts 565 kama akiba ya umeme tuliyoiweka kibindoni. Bado hiyo Megawatts 50 kiwastani hata ukijumlisha mikoa yenye viwanda vingi na vikubwa kama Pwani, Dar es Salaam, Arusha, Tanga na Mwanza bado ni kubwa sana. Nimeweka kwa kiwango cha Juu saana usisahau matumizi ya Mtwara na Lindi ni Megawatts 22- 30 tu.
Ina maana hapo tunaenda kuua kabisa stori za mgao wa umeme na mambo ya umeme kukatikakatika. Hapo wenye viwanda vikubwa, vya kati na vidogo kabisa watazalisha bidhaa zao bila tatizo na zaidi kwa gharama nafuu kutegemea na urahisi wa gharama kwa umeme wa maji.
Umeme wa Kinyerezi ambao ndiyo tunaojivunia kwa sasa kuwa ni mradi mkubwa wa umeme kiwango chake cha mwisho cha kuzalisha umeme ni Megawatts 1,560 tu ina maana Bwawa la Mwalimu Nyerere pekee yake linaenda kutupa umeme wa uhakika tena wa maji ambao ni rahisi zaidi kuliko aina yoyote ile ya umeme duniani ukiachana na wa jua, upepo, nyuklia, makaa ya mawe, mafuta na gesi.
Tukumbuke umeme unaozalishwa na maji ndio umeme wa gharama nafuu na rahisi zaidi kuliko umeme wowote ule duniani. Kumbuka uniti 1 inayozalishwa na maji ni shilingi 36 tu wakati umeme wa nyuklia ni shilingi 65 kwa uniti, umeme wa jua shilingi 103.05, upepo 103.05, makaa ya mawe 118, gesi asilia 147 na mafuta ni 426. Hivyo tunaenda kushusha maradufu bei ya umeme kwa watumiaji hivyo kuhimili mfumuko wa bei wa bidhaa za viwandani.
Hii tafsili yake kukamilika tu kwa Bwawa la uzalishaji wa umeme la Mwalimu Nyerere kutashusha kwa kiwango kikubwa sana gharama ya umeme mpaka shilingi 36 tu kwa uniti hivyo kutoa nafasi kwa bidhaa zetu za viwanda nazo kushuka sana. Hapo mpaka kwenye matumizi ya kawaida nyumbani yatashuka na hata kwa watanzania watakaofungua viwanda vidogo kwa vikubwa watanufaika sana na gharama ndogo ya uzalishaji wa bidhaa itakayoleta neema na nafuu mpaka kwa sisi watu wa hali ya chini kabisa, machinga, mama nitilie, wajasiriamali na makundi mengine.
Unapokuwa na umeme wa uhakika, lakini sio wa uhakika tu tena na wa gharama nafuu ya bei tayali unavutia wawekezaji wengi zaidi kuja kujenga viwanda hapahapa. Suala la uhakika wa umeme na nafuu yake ni mambo ya msingi sana kwa mwekezaji anayefikiri kwenda kuwekeza sehemu yoyote ile kwasababu kiwanda ni nishati.
Vipi umefikilia hizo Megawatts zingine zaidi ya 565 ambazo tunakuwa tumezitia kibindoni baada kujihakikishia uhakika wa umeme nchi nzima? hapo tunaweza kuamua kuuza kwa majirani zetu hapo Kenya, Malawi, Uganda au Msumbiji ambako tunajua bado hawana uhakika wa umeme. Hapo unazungumza kuhusu umeme wa Rufiji tu, hujaenda Kinyerezi, Kidatu, Mtera, Nyumba ya Mungu na kwingine ambako umeme unaendelea kuzalishwa.
Rais Magufuli na Serikali yake baada ya kugundua hatuna umeme wa kutosha na wenye bei nafuu kwa wananchi wake ndiyo ikaja na suluhisho hilo la Bwawa la Mwalimu Nyerere. Nini tena sasa? Tusiposema sisi kwa haya yanayofanyika basi hata mawe yatapiga kelele siku moja.View attachment 1597580
Safi sana..tatizo tuombe tusipate ukame tu wa maji na mvua na vyanzo vya maji vibaki constant la sivyo work done will be equal to ZERO.
Tuwaamini wataalamu wetu wanaohusika na ujenzi wa Bwawa la Nyerere kwan kuzingatiwa athari na matokeo yake ya kijamii, kisiasa, mazingira na kiteknolojia (rejeeni EIA na SIA ya huo mradi).Haikuwepo na haja ya kujenga bwawa jipya Hali ya zamani yangeweza boreshwa, kwa kuondoa michanga na matope mabwawani pia kubadili injini za zamani na kufunga za kisasa maji kidogo speed kubwa umeme mwingi
Ukipata nafasi na ukiona ni muhimu pitia ripoti iliyoambatanishwa hapa kuhusu mradi wa gesi na matumizi yakeView attachment Oil and Gas Masterplan.pdfIli kuweza kuibadili gas Yetu iwe katika kimiminika na kusafirishwa kwa njia ya mitungi, Project inaweza kugharimu kiasi gani cha fedha? Kwasababu hili likiwezekana ni hakika tutaifaidi Gas hii maradufu
Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app