Nini umuhimu wa ziara ya Rais Samia Ufaransa?

tre bien wenzetu walinyolewa sisi tutie maji kwa maana ya kuweka mikataba ya maslahi bora kwa Nchi yetu, ufaransa sasa hivi inajitafuta na hii ni fulsa kwetu, wachimbe ulanium mikoa ya kusini ambayo mwamerika ameweka kama reserve wakati sisi tuna njaa ya pesa mjazano wa nikeli kababnga na herium Rukwa, hatupashwi kuwa Nchi ya kulia lia wakati tuko matajiri hivi.
 
Ni kweli, hata kama wafaransa wanataka Uranium, tusiingie kichwa kichwa, tuweke vipaumbele vya nchi na biashara kwa faida yetu.
 
Usiwe mwepesi wa kuabudu!! Diplomasia siyo jambo la kupuyanga, ni akili!!!

Tulisafiri sana kwenda Nchi za Kiarabu, kila mtu na dunia inajua kwamba tayari Tanganyika imepoteza kipande chake cha ardhi!! Endeleeni kupuyanga mtuletee dhahama nyingine
 
Shida ya umaskini na kukosa mikakati ya kujitegemea, Samia hana jipya
 
Je ni mikataba mingapi? ya kuuza rasilimali kaenda kusaini

Labda makamba atusaidie kujibu
 
Samia ameona Dubai na arabuni pamejaa maji sasa anahamia ulaya.

Ni hatari nchi kuongozwa bila katiba ukitegemea utashi wa kiongozi
 
Usiwe mwepesi wa kuabudu!! Diplomasia siyo jambo la kupuyanga, ni akili!!!

Tulisafiri sana kwenda Nchi za Kiarabu, kila mtu na dunia inajua kwamba tayari Tanganyika imepoteza kipande chake cha ardhi!! Endeleeni kupuyanga mtuletee dhahama nyingine
hapo unamtetea kibaraka wa mabwenyenye wa magharibi sio? kwamba anawategemea mabwenyenye kuvuruga nchi 🀣

Nchi hii itaendelea kuongozwa kwa weledi na watu wa chama makini, wachapa kazi wazalendo wanaozingatia katiba na sheria za kitaifa na kimataifa, kwa maslahi mapana ya waTanzania wote πŸ’

Rais yupo nje ya nchi kwa maslahi mapana ya waTanzania wote πŸ’

Kibaraka anaropoka ropoka ndani na nje ya chama chake kwa maslahi ya mabwenyenye yanayomfadhili na kumtuma πŸ’
Huuo papets anavaa ma culture culture
ili eti aonekane ni msela wa Tz πŸ’
 
Wazalendo wakipatikana wanapigwa vita vya wazi na vya chini kwa chini ili wapotee ulingoni !!

Uzalendo wa kwanza ni kudai Katiba mpya bora !!

Itakayozuia madudu yooooteee !!

Sio Katiba mpya tu !
Bali iwe ni Katiba mpya BORA ! πŸ™πŸ™
kibaraka ndio awe kiongozi wa kudai katiba, kweli?πŸ’
 
Ni sawa mkuu, lakini ukiona mwezio aliyenyolewa bila makali, kama nchi za Afrika Magharibi, jiweke vizuri na wembe wako mwenyewe!
kwamba Ufaransa atume mapuppets waje kutuvuruga πŸ’

unaelewa huko nchi za magharibi viongozi wa kuu wa nchi walikua na ideology na interests tofauti na kiongozi mwingine πŸ’

mathalani mkuu wa majeshi ana interest kufanya kazi na Urusi, Rais hataki, huku nae huyo Rais ana interest ya kufanya kazi na Ufaransa, huku mkuu wa majeshi hataki.

unakuta tena makamu wa Rais na mkuu wa majeshi lao moja. kwa style hiyo mnaeezaje kuongoza nchi πŸ’

hapa kwetu kajitokeza kibaraka na anaonekana vizuri sana, na interests zake ni zipi, katumwa na nani inajulikana πŸ’

kumdhibiti ni rahisi lakini kumkabili ni kwepesi zaidi πŸ’
 
Watu wataendelea kutumia kuni na mkaa bila yeye
 
Sasa hivi watu hawadanganyiki tena wanajua pumba na mchele ni upi !

Wanachokisubiri ni muda tu wa kufanya maamuzi yao na ni muhimu yakaheshimiwa !!

Propaganda za zamani hazina nafasi !
Watu wameshaosha macho !

Makonda alijaribu kuonyesha angalau Uzalendo wake πŸ˜… if you may call it ni Uzalendo ! πŸ˜…

Lakini all of a sudden amefungwa Speed gavana Chap kwa haraka kama ile ya Vodabima. πŸ˜…πŸ˜…πŸ™πŸ™ !
 
tunahitaji uzalendo, tunahitaji watu wazalendo wa maneno na vitendo angalau wa kutetea maslahi ya taifa na kukemea matumizi yasiyofaa ya fedha za serikali kwa maana ya matumizi yasiyozingatia vipaumbele vya taifa.
Katiba mpya bora ni muhimu !
 
Huu ndio upeo wa elimu ya Watanzania! Eti puppets wa Magharibi hawawezi kufanya chochote Tanzania! Huyo anayesema hivyo hajui hata Tanzania inapata asilimia ngapi katika dhahabu yake inayoibiwa. Na jee, Tanzania inatoa kiasi gani cha dhahabu kwa mwaka? Hata Samia hajui.
Capt Ibraim Traore wa Burkina Fasso amewafukuza wachimbaji wote wa kigeni nchini mwake: Wafaransa, Warusi, Wa Canada....kwa kugundua nchi yake inapoteza dola milioni 16 kwa mwezi kutokana na mchezo wa watu hawa. Milioni 16 ni zaidi ya bajeti ya mwaka ya Wizarara ya Elimu ya Burkina Fasso (nadhani hata Tanzania)! Moja ya mbinu ni pamoja na kusafisha dhahabu nje ya nchi (ambayo bado inaendelea Tanzania), kughushi uzito wa mzigo na kukwepa kodi. Yote haya yanaenderlea Tanzania, hadi Umoja wa Mataifa hivi karibuni umetoa wito kwa Tanzania kuweka mkazo zaidi katika kudhibiti utajiri wake wa madini! Halafu wewe (nadhani chawa au mtendaji) waja hapa kupiga porojo!
Hebu jaribu tu kuiuliza serikali: tunatoa tani ngapi za dhahabu (tu) kwa mwaka? Katika dhahabu hiyo, kiasi gani tunakiweka hifadhi ili kuzaziti sarafu yetu? Kisha uje uandike hapa!
 
Tutaona faida ya vitu hivyo pale tu tutakapofikia ujuzi wa kuchimbua sisi wenyewe. Sijui kwa nini ni vigumu kwa vichwa vya viongozi wetu kusomesha watu wa kutosha kwa miaka kumi na kuleta zana na kuweka mazingira ya nidhamu na udhibiti....tukaweza kufanya wenywe. Mbona Burkina Fasso sana inachimba, kusafisha, na kuuza dhahabu yake juzi juzi tu baada ya kuwafukuza wachimbaji wote wageni? Sasa imeanza kupata mara tatu ya ilivyokuwa inapata!
Miaka 63 ya Uhuru? Yaani mpaka miaka 200 ndiyo tuweze kufukua udongo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…