Huku nyamongo, kuna shida kubwa sana, ndani ya mwaka huu, wameshauawa watu zaidi ya kumi,kuna dada alikutwa amepigwa risasi, kuna wengine wawili walichomwa na visu kwenye uke katika matukio tofauti,wakafa kwa kupoteza damu nyingi.. kuna mwingine aliuliwa mgodini kwa kupigwa risasi, kuna mwingine alikutwa amejinyonga, lakini watu wanasema kuwa alipigwa na mume wake mpaka akafa,.. kuna wengine waliuliwa wawili kwa wakati mmoja.... Kuna mwingine aliuliwa kwa kusingiziwa kuwa ni mwizi, kumbe hakuwa mwizi..... Na katika matukio hayo yote ni mawili tu, watu walikamatwa, na walikamatwa kwa sababu za kisiasa, vinginevyo wangekuwa mtaani...
Watoto wa kike wanatahiriwa, na watu wanafanya sherehe adharani, hamna polisi anayewakamata..huku, kutembea na bastola ni ubishoo, kwa hiyo matumizi ya silaha ni ya kiholela kabisa
Polisi wapo, lakini RUSHWA ndio imewatawala,,, yaani huku wageni tunaishi kama tupo sudani, au afriganistani,.. so sad kwa kweli