Nionesheni bodaboda aliyeagiza gari Japan au China kwa kipato cha bodaboda niache kazi ya utumishi wa umma ndani ya saa 24

Afisa Utumishi analipwa take home 470,000/-
Bodaboda 35000 Kwa siku, Jumla 900,000/-
Watumishi wa Halmashauri nyie Hamuwatishi bodaboda Kwa kipato
Watumishi wanaowatisha/kuwazidi bodaboda kwa kipato ni wa Tanroads, EWURA, EGA, TPDF, TRA, TCRA, LATRA, TPA, TANAPA nk
 
Kwani Kwa take home ya 470,000/- ya Afisa Utumishi, anaweza kukopa milioni 20? Bodaboda wako juu ww
 
Bodaboda, walimu na wengine wote nmekosa kuheshimiana na kuthaminiana.
Mtu mwenye akili zake timamu hawezi kukaa kuchangia mada za kibaguzi na majigambo kama hizi.
Pambaneni kuziweka familia zenu vzuri kiuchumi na kiroho na si huu upuuzi.
 
Ubaya mnakutana na bodaboda ambao majukumu ndo yamewapeleka kwenye kazi so kila anachokipata kinaishia kusogeza familia, na ambao hawana majukumu hawajajua jinsi ya kuhandle maisha. Kusave pesa ni suala lingine.
 
NIMETAFAKARI KIDOGO ALITOA HUU UZI ANAWEZA KUCHAFUA HALI YA HEWA
1.HOJA YAKO INALETA MATABAKA
2.SIO KWELI KUWA MTUMISHI ANAZIDIWA KIPATO NA BODA BODA ALIYEMUAJILI
3.UNATAKIWA UHIMILI CHANGAMOTO NA MALUMBANO HASA YA MITANDAO KWANI MTU ANAWEZA KUONGEA CHOCHOTE KWA SABABU HATUJUANI
4. UNAFIKIRIA ALIYEKWAMBIA BODA BODA ANAPESA MTOTO WAKE AKITAKA KUOLEWA NA BODABODA AU MTUMISHI ATAKIMBILIA WAPI JIBU UNALO JAPO UKWELI MCHUNGU
5 MASUALA MENGINE NI YAKIJINGA NI BAAZI YA WATU KUTAKA KUCHAFUA HALI TU..
6. MIMI NI MWALIMU WA MSINGI NA BODA BODA NINAZO MBILI ILA HUWEZI KUNIAMBIA NIACHE UALIMU NIKAJIAJIL KUWA BODA BODA RASMI
7...NIKIFIKIRIA BASI TU ILA KAMA VIP ACHANA NA MAMBO YA KULUMBANA KWA NAMNA HII HAKUNA TIJA MTAA UNAJIELEZA WENYEW
 
Issue ni kusave na kuwekeza, boda boda yoyote atakayeweza hili ewe mtumishi wa umma unayelipwa chini ya milioni kaa nae mbali sio saizi yako.
 
Eti boda kalinganishwa na mwalimu hizi dharau acheni boda ni kazi Kama kazi zingine lakini sio za kulinganishwa na mwalimu Wala maisha ya walimu sio magumu Kama vile watu mnavyojadili humu.
 
Kweli kuna tofauti ya elimu na akili, unaweza kuwa na elimu ila usiwe na akili na unaweza ukawa na elimu na ukawa na akili tena nyingi mara nyingi mwenye elimu na akili na kipato hana sababu ya kujivimbisha watu wajue bali ni standard yake au class yake alizike nayo na si kushindana iyo ndo tofauti ya elimu na akili tujitaidi kukombolewa na elimu zetu tupatazo jamani bila ivo kutakuwa hakuna tofauti ya bodaboda na mwenye elimu ikiwa kila mwenye elimu akajiona ni bora kuliko hao wasio katika mfumo rasmi wa ajira.
 
Achome ofisi?
 
Acha waendeshe bodaboda mpaka viuno vilegee. Mimi nitaendelea kutafuna wake wao.
 
Acha jazba, tafuta mtaalamu wa hesabu akupigie kipato cha bodaboda kwa mwezi uangalie na kipato cha mwalimu kwa mwezi. Tatizo tu la bodaboda sio kazi ya kudumu na ni riski. Akithubutu na kama hataugua, aanza kazi wakati mmoja na mwalimu mpaka wakati wa mwalimu kustaafu nae bodaboda Mungu amfikishe hapo. Hakika bodaboda atampita mwalimu kwa kipato.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…