Nionesheni bodaboda aliyeagiza gari Japan au China kwa kipato cha bodaboda niache kazi ya utumishi wa umma ndani ya saa 24

Nionesheni bodaboda aliyeagiza gari Japan au China kwa kipato cha bodaboda niache kazi ya utumishi wa umma ndani ya saa 24

Na mimi kama bodaboda nasema nionesheni mwalimu anayeweza kunywa bia kwa cash tena kwa kuzungusha siku 10 mfululizo baada ya kupata mshahara.
 
Mkuu kuwajibu boda boda ni kupoteza muda wako,hiyo kazi wanaifanya kwa sababu hakuna mbadala,maneno wanayotoa kukashifu watumishi wa umma kama walimu ni kujifariji tu...boda boda tuko nao humu mtaani na tunayajua maisha yao...huwezi mzarau mtu mwenye uhakika na wa mshahara,bima ya Afya na hata anaweza pata mkopo....tuishi nao tu hawa ndugu zetu,wacha wajifariji kwa hayo maneno.
 
Afisa Utumishi anakipwa take home 470,000/-
Bodaboda 35000 Kwa siku, Jumla 900,000/-
Watumishi wa Halmashauri nyie Hamuwatishi bodaboda Kwa kipato
Watumishi wanaowatisha/kuwazidi bodaboda kwa kipato ni WA Tanroads, EWURA, EGA,tpdf, Tra, Tcra,latra, TPA, TANAPA nk
Mh bodaboda gani analaza 35000 per day maisha sio rahisi kiasi hicho.
 
Mh bodaboda gani analaza 35000 per day maisha sio rahisi kiasi hicho.
Bodaboda anaefanya delivery. Anahudumia maduka hata 10 tofauti. Anapeleka mzigo na analeta hela kutoka kwa mteja hadi 2m bila shida.
 
NI kweli walimu nchini kwetu wanalipwa kipato kidogo kisichoendana na wakati uliopo lakini kauli ya bodaboda si kiungwana hata kidogo Mimi Nina imani na wao wanasikia tu kupitia kwenye vyombo vya habari jinsi walimu wetu kupitia vyama vyao vya wafanyakazi malalamiko yao juu ya kipato kidogo na mazingira magumu ya kazi lakini hii haitoshi kuwadharau walimu bado wana unafuu mkubwa kuliko bodaboda kuanzia kwenye upatikanaji wa huduma ya afya,mikopo kwa ajili maendeleo, uhakika wa kipato nk
 
Naomba mje na hoja nzito nyie walimu Mnaoshindia chai na kalimati

Naona mnajisifiasifia tu mara bima6 mara Eti wakuonyeshe bodaboda mwenye nyumba ya 20m uzile kufundisha

Hoja yangu[emoji1484]

We mwalimu unalipwa shingapi kwa mwezi kwamaana mimi naingza zaidi ya 35k Kwa siku
 
Maisha ya mbuzi yana dharau sana kula yake ya kupewa kamba, kula yake kila siku ya kukisiwa lakini anakunya mavi madogo madogo ila anataka kuishi kwenye banda kubwa🤣
🤔🤔🤔🤔 #killa cam we akili kubwa, inatakiwa kuumiza kichwa kupata hii falsafa yako
 
Namm nooneshwe mwalimu au afisa wa juu wa serekalin aliaagiza gari jipya kutoka Japan ,

Wengi wenu mnaendesha magari used
Wakt boda boda wote Wana vyuma vipya

Hi Kaz siyo laana narudia siyo laana Ni Kaz Ni ofc za watu na familia zao waheshimiwe Hawa watu na waawezeshwe

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
NIMETAFAKARI KIDOGO ALITOA HUU UZI ANAWEZA KUCHAFUA HALI YA HEWA
1.HOJA YAKO INALETA MATABAKA
2.SIO KWELI KUWA MTUMISHI ANAZIDIWA KIPATO NA BODA BODA ALIYEMUAJILI
3.UNATAKIWA UHIMILI CHANGAMOTO NA MALUMBANO HASA YA MITANDAO KWANI MTU ANAWEZA KUONGEA CHOCHOTE KWA SABABU HATUJUANI
4. UNAFIKIRIA ALIYEKWAMBIA BODA BODA ANAPESA MTOTO WAKE AKITAKA KUOLEWA NA BODABODA AU MTUMISHI ATAKIMBILIA WAPI JIBU UNALO JAPO UKWELI MCHUNGU
5 MASUALA MENGINE NI YAKIJINGA NI BAAZI YA WATU KUTAKA KUCHAFUA HALI TU..
6. MIMI NI MWALIMU WA MSINGI NA BODA BODA NINAZO MBILI ILA HUWEZI KUNIAMBIA NIACHE UALIMU NIKAJIAJIL KUWA BODA BODA RASMI
7...NIKIFIKIRIA BASI TU ILA KAMA VIP ACHANA NA MAMBO YA KULUMBANA KWA NAMNA HII HAKUNA TIJA MTAA UNAJIELEZA WENYEW
Mwalimu wa wapi ambae unaandika herufi kubwa tu unafundisha watoto ujinga boda boda anakuzidi maisha
 
Kuna walimu wengi nawajua wanaendesha bodaboda tena muda wa kazi na wana njaa kwelikweli hawaachi hata 100 kuna siku watabakwa huko vichochoroni wanakowapeleka abiria
 
Sijaelewa Mkuu kuagiza gari ndio mafanikio makubwa ya Watanzania? Serikali Punguzeni kodi japo Kidogo watu waweze kuagiza magari yao maana huku sokoni yanapigwa na Vumbi tuu ukilipia gari wauzaji wanashukuru kweli tena halina ile mikodi ya kuuana...
 
Hii sasa ni too much

Unamfananishaje mtu anayekufa kama nzi hapa jijini Dar es Salaam na mtumishi wa umma?

Unamfaninishaje bodaboda ambaye akipata ajali kubwa tu anakimbizwa Kijijini kwa mama yake akafie huko na mtumishi wa umma ambaye ana bima ya watu 6?

Mtu akistaafu anakunja mpaka milioni mia moja leo hii unamfananisha na Bodaboda ambaye hata nywele kuchana ni mtihani.

Nionesheni bodaboda mwenye nyumba angalau ya milioni 20 ambayo Kajenga kwa kazi ya kubeba watu?

Sasa hivi muda wa kazi ukipita ofisi za umma zikiwemo shule za msingi Dar es salaam utakutana na gari namba C,D na E nyingi za walimu na hazijawahi kukosa mafuta hata siku moja.

Na service zinafanyiwa kwa wakati. Bodaboda akiharibikiwa cylinder head ya 35 anahangahika kama kaibiwa figo
Aisee
 
Tunaishi na boda boda wengi tu huku mtaani

Wengi wao ni-

Wanywa viroba

Wanagonga Malaya mtaani.

Wanabaka wanafunzi wa sekondari

Wanatembeanna wake za watu

Wanavaa mavazi ya kihuni milegezo na kunyoa viduku Haiba za kihuni kabisa.

Matapeli na wanashiriki kuwachorea Ramani majambazi wapi wakaibe

Wezi wa piki piki wanazopewa na watumishi.

Wako wavuta bangi , watumiaji wa MADAWA ya kulevya na Ile harufu ya Petrol ndio kabisa wanawehuka akili.

Wanakufa sana kwa ajali kwa sababu za kijinga na kipuuzi kabisa.

Boda boda sio kazi ya kujivunia ni vile tu hawana options.

Hata walio smart still Wana struggle kutoboa kwenye maisha maana kufikisha rejesho ni kisanga kizito.

Waache kutunisha vifua na kutumika kisiasa.
 
Back
Top Bottom